Thursday, November 28, 2013

ZITTO KABWE APONZWA NA WALAKA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema kimesema kwamba kilifikia uamuzi wa kumvua nyadhifa zake, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe kutokana na sababu moja tu ya kuhusika katika Waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013.

TANZANIA, BURUNDI DRC ZAUNDA UMOJA



Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao. Katika siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano hasa wa kiuchumi.

Tanzania, Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri wa maji katika Ziwa Tanganyika.

Sunday, November 24, 2013

TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB) KUHUSU KUVULIWA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA CHANGU CHA CHADEMA

1. Utangulizi

i. Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 ­ 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu . Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa.

Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.

ii. Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba

ZITTO KABWE AIGOMEA KAMATI KUU


MBUNGE wa Chadema ambaye pia ni Naibu kiongozi wa kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe amefunguka na kusema hayupo tayari kuondoka katika chama hicho hadi watakapoanza wao kuondoka.

Zitto ameyazungumza hayo leo jioni katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumzia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya chama hicho kumvua nafasi zake zote za uongozi yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati kuu ya chma hicho Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba.

Zito amedai hakuhusika wala kujua waraka wa siri ambao ndio uliosabababisha kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuunasa waraka huo.

Tuesday, November 19, 2013

WABUNGE EALA MATATIZO NCHI ZA MAZIWA KUPATA SULUHISHO


WABUNGE wanaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wamesema suluhisho la matatizo ya nchi za Maziwa Makuu yatapata ufumbuzi wa kudumu iwapo kutakuwa na utaratibu wa kukaa meza moja kwa pande zote husika na kufanya mazungumzo ya kuleta amani.

Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wabunge hao, Adam Kimbisa wakati akizungumza na waandishi

wa habari jijini Dar es salaam ambapo pia alipongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alioitoa Bungeni Dodoma Novemba 7 mwaka huu juu ya Jumuiya hiyo.

“Sisi tunaamini amani ni jambo la msingi katika Afrika Mashariki na hasa katika nchi zilizo katika Maziwa Makuu. Tunawapongeza wanajeshi wetu na wanajeshi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri walioifanya iliyowezesha mafanikio kupatikana” alisema.

Akielezea juu ya baadhi ya nchi wanachama wa EAC ambao ndio waanzilishi wa vurugu mbalimbali na migogoro Mwenyekiti huyo alisema kuwa Tanzania imekomaa kisiasa hivyo hawawezi kuwaondoa wale wanaoleta chokochoko kwa kuwa dawa ni kuzungumza na sio kuwatoa.

Mtangamano

Aidha Kimbisa amesema misingi ya Utengamano wa kiuchumi ikijengeka vizuri na kufanya kazi ipasavyo wananchi wote wa Afrika Mashariki watafaidika na hivyo suala la kuruka hatua yoyote ni jambo lisilokubalika.

“Tunaungana na kauli ya Rais kwamba Tanzania ni kati ya nchi zinazotaka ngazi zote za mchakato wa Mtangamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka hatua yoyote. Hatua ya kwanza ni Umoja wa Forodha inafuata soko la Pamoja kasha Umoja wa Fedha na hatimaye shirikisho la Kisiasa” alisema.

Alisema hadi sasa ni hatua mbili zilizotiwa saini na mchakato wa kuweka saini Umoja wa fedha unatarajiwa kutiwa saini baada ya kikao cha Juu cha Marais kinachotarajiwa kufanyika mjini Kampala Novemba 30 iwapo masuala yote muhimu ya mchakato huo yatakuwa yamekamilika.

“Jambo la msingi ambalo hata Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya imesema wazi kwamba Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi kwa manufaa ya wananchi na isiwe ya viongozi. Wananchi washirikishwe katika kila hatua na kila ngazi ili iweze kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao” alisema.

Kuhusu VISA alisema kuwa wao wanaruhusu nchi nyingine kuendelea lakini Tanzania bado hawajafikia muafaka kwa kuwa wanaangalia maslahi ya nchi kwanza. Katika Hatua nyingine, Wabunge hao walimpongeza Rais Kikwete kupeleka kikosi cha Wanajeshi katika Brigedia Maalum iliyoundwa na Umoja wa Mataifa ili kuongeza nguvu ya kudhibiti waasi Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Thursday, November 14, 2013

WATAKAOVUJISHA TAALIFA ZA SIMU KUKAMATWA

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za simu za mikononi, zimewataka wateja watakaokumbwa na tatizo la kuvujishwa kwa taarifa za simu, kuripoti kwenye vyombo vya dola ili hatua zichukuliwe.

Aidha imeelezwa kuwa ingawa kumekuwa na mashine za kuzuia taarifa za siri za simu za mikononi kutovuja, baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za simu wasio waaminifu wamekuwa wakihujumu wateja kinyume cha sheria kwa kuchezea teknolojia isivyopaswa.

Hadhari hiyo imekuja kukiwa na wimbi la matumizi mabaya ya simu za mkononi nchini, ikiwemo matumizi ya teknolojia kutoa hadharani mawasiliano ya siri ya watu.

Miongoni mwa matukio ya hivi karibuni, ni taarifa zilizoanikwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Kabwe Zitto, zikionesha mawasiliano ya siri anayodaiwa kufanya na watu mbalimbali yakidaiwa kuwa ni ya kuhujumu chama chake.

Tuesday, November 12, 2013

MKUU WA SHULE ABAMBWA AKIVUJISHA MAJIBU YA MTIHANI

MKUU wa Shule ya Sekondari ya Nkinto wilaya ya Mkalama, Monica Sebastian (30) na mwalimu wa kawaida wa shule hiyo, Agaloslo Otieno (32), wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kuvujisha matihani wa kidato cha nne unaoendelea kufanyika hivi sasa nchini kote.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa tatu usiku, katika shule hiyo kata ya Mwangeza tarafa ya Kirumi wilayani humo.

Alisema kuwa Mwalimu Agaloslo akiwa anasimamia mtihani katika Shule ya Sekondari Mwangeza, alikuwa anaandika baadhi ya maswali ya Kiswahili na Civics kwenye simu yake ya kingajani na kumtumia Mwalimu Monica, akiwa shuleni kwake Nkinto.

Kamwela alisema baada ya Monica kupata maswali hayo, alikuwa anayatafutia majibu akiwa chooni na wanafunzi walikuwa wanamfuata huko huko chooni ili awapatie majibu hayo.

"Lengo lao ilikuwa ni kuwasaidia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika mtihani wao wa kidato cha nne mwaka huu. Wanafunzi waliambiwa kuwa wawe wanadanganya kwamba wanaenda kujisadia chooni ili wakapatiwe majibu na mkuu wa shule," alisema kamanda huyo na kuongeza; "Uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwa, uvunjishaji huo ulifanyika kwa nyakati tofauti kati ya Mkuu wa Shule Monica na Mwalimu Agaloslo akiwa anasimamia mtihani huo katika shule nyingine.
“Baada ya Mwalimu Monica kutumiwa maswali alikuwa anajificha chooni na wanafunzi kwa nyakati tofauti huomba ruhusa kwa wasimamizi kwenda chooni kwa nia ya kujisaidia, ambapo humkuta mwalimu huyo na kuwapa maelekezo ya namna ya kujibu maswali hayo," alisema.

Alisema baada ya polisi kupata taarifa ya siri kutoka kwa wasamaria wema, waliweka mtego shuleni Nkinto na kufanikiwa kumkamata Mwalimu Monica, huku simu yake ikiwa na baadhi ya maswali ya mtihani.

Alisema polisi inaendelea na upelelezi zaidi, na kwamba mara utakapomalizika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.

Friday, November 8, 2013

HOTUBA YA RAIS KIKWETE JANA

Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu;
Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri;
Mheshimiwa Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni;
Waheshimiwa Wabunge;
Mabibi na Mabwana;

Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kukubali ombi langu na kutenga muda wenu ili niweze kuzungumza na Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuhusu masuala muhimu kwa uhai, ustawi na maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Mheshimiwa Spika;
Nimeambiwa kuwa taarifa ilipotolewa kuwa ninaomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge, kumekuwepo na dhana mbalimbali. Wapo waliodhani kuwa nakuja kuzungumzia mchakato wa kuunda Katiba mpya na hasa matukio ya wiki chache zilizopita. Wapo waliodhani nakuja kuzungumzia “Operesheni Tokomeza”. Tena wapo waliokwenda mbali na kufikiria kuwa nakuja kuwakaripia Waheshimiwa Wabunge waliotoa maoni yao kuelezea kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni hii muhimu. Na wapo pia waliodhani ninakuja kuzungumzia ushiriki wa majeshi yetu ya Tanzania katika Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa nchini Kongo.

Wednesday, November 6, 2013

MFANYAKAZI TBC AUWAWA

Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Nchini TBC, pichani,RAMADHAN GIZE ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la UBUNGO Maziwa Jijini DSM.


Tukio hilo limetokea baada ya watu hao kuvamia duka moja katika eneo hilo la UBUNGO MAZIWA kwa lengo la kupora, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MWARAMI RAJABU amejeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu hao wanaosaidiwa kuwa majambazi.

Tuesday, October 29, 2013

KINANA AZIMA MAPINDUZI



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alilazimika kuzima mapinduzi yaliyokuwa yamepangwa kuwang’oa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (UVCCM), Sadifa Juma Khamis na makamu wake, Mboni Muhita.

Jana Kinana akifungua mkutano wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo, aliweka bayana kuwa mkutano huo haukuwa kwa ajili ya “kuibomoa UVCCM, bali kuijenga”, kauli ambayo inatajwa kuwa iliwavunja nguvu wajumbe waliokuwa wamepanga kuanzisha harakati za kuwatoa madarakani viongozi hao.

Habari zaidi kutoka Dodoma zilisema kauli ya Kinana iliongeza nguvu harakati za kujinasua za Sadifa ambaye usiku wa kuamkia jana, alikesha akifanya vikao vya kuwaomba radhi wenyeviti wa UVCCM wa mikoa na baadaye wajumbe wote wa Baraza Kuu.

“Hatua hiyo nadhani imemsaidia sana maana wenzake ndani ya umoja huo hawaridhiki na jinsi mambo yanavyokwenda, pamoja na uongozi wake. Wanaona kama hakidhi standards (viwango) zao,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya mkutano huo.

MWANAFUNZI AJIUA KUONDOKA NA AIBU

MWANAFUNZI wa Darasa la tano Katika Shule ya Msingi Kitanda katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru aliyefahamika kwa jina la Faudhia Suleiman Ally Kawalula (14) amejinyonga hadi kufa kwa madai ya kuondokana na aibu ya tukio la Wizi.

Mashuhuda wa Tukio hilo walisema kuwa Mwanafunzi huyo alikutwa akiwa aejinyoga kwa kutumia kamba asubuhi ya kuamkia oktoba 27 mwaka huu nda ya chumba alicho kuwa akilala nyumbani kwao.

Wakizungumzia chanzo cha tukio hilo kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kuchukua maamuzi hayo alituhumiwa kuiba Tsh. 5000 kwa muuza duka jirani na nyumba yao .

Walisema baada ya tukio hilo ambalo lilidaiwa kufanyika kwa ustadi mkubwa na alipo guindulia tayali akuwa amekwisha nunua nguo za ndani, mafuta ya kupaka na sabuni vitu ambavyo muuza duka huyo alivitaka
apewe ili aviuze kwa ajili ya kufidia fedha yake hali ambayo ilimuweka binti huyo katika aibu na kumfanya achukue hatua hiyo.

Monday, October 28, 2013

VIONGOZI CHADEMA WAZIPIGA KAVUKAVU

Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.

Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa uongozi kwa muda usiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na viongozi hao wa Chadema kufikishana polisi.

Alikutwa na zahama hiyo mbele ya viongozi wakuu wa Chadema Taifa, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei katika Hoteli ya Coridal Spring.

Saturday, October 19, 2013

TLC KUZINDUA FILAMU

Kundi la TLC linatalajia kufanya uzinduzi ya filamu yao mpya inayojulikana kwa jina la CrazySexyCool.

TLC inatarajia kuizindua filamu hiyo wiki ijayo ambapo teyari wameshaanza kuonesha baadhi ya vipande vya filamu hiyo.

MECHI YA YANGA NA SIMBA ULINZI WAIMARISHWA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vimejipanga ipasavyo kuakikisha Ulinzi unakuwepo Uwanja wa Taifa  wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Kamishina Suleiman Kova alisema  mchezo wa leo utakuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki wa Tanzania na wale wa nchi za Afrika Mashariki tutokana na hali hiyo jeshi la Polisi limejipanga kupambana na hali yoyote ya uvunjifu wa amani itakayo jitokeza katika mchezo huo.

"Tunaomba wananchi wasiwe na shaka yeyote ya kiusalama na pia watupe ushirikiano wa kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi kwa jambo lolote wanaloisi linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa ndani ya uwanja au nje."alisema Kova.

Wednesday, October 16, 2013

WAZEE YANGA YAJITAMBA KUINGO'A SIMBA

WAZEE wa Club ya Yanga wametamba kuwafunga watani wao wa jadi Simba katika mechi yao ya kesho kutwa inayotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo wamedai kuwa mnyama lazima afe.

Akizungumza kwa niaba ya wazee hao na Waandishi wa Habari Dar es Salaam Katibu wa Baraza la Wazee Ibrahim Akilimali alidai kuwa  timu hiyo ndiyo inaanza kucheza mchezo wao wa ligi rasmi huku wakijitapa kumuua mnyama kutokana na maandalizi yao ambapo kikosi cha Yanga kitapanda dimbani huku kukiwa hakuna majeruhi.

Friday, October 4, 2013

SERIKALI KUBORESHA ELIMU NCHINI

SERIKALI inatakiwa kuboresha kwanza maslahi ya walimu na vifaa mashuleni ili kupatikane na matokeo makubwa (Big Result Now)

Hayo alisema Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika wakati akikabidhi madawati 120 yenye thamani ya shmilioni 12 katika shule zilizoko Kata ya Manzese ambao walikuwa na uhaba wa madawati na kusababisha wanafunzi kukaa chini .

Alisema kuwa walimu wamekuwa wakililia maslahi yao kila siku lakini serikali haiwasikilizi hivyo itasababisha matokeo mabya ya mitihani kila siku.

COKE STUDIO YAZINDULIWA AFRIKA

KIPINDI cha muziki kinachojulikana kwa jina la Coke  studio Afrika chazinduliwa rasmi jana huku kikiwa na lengo la kuuboresha muziki wa Afrika uwe wa kisasa na unaolenga vijana.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja bidhaa wa Coca Cola Tanzania, Maurice Njowoka aliweka wazi kuwa studio hiyo inathamini nguvu ya muziki katika kuwaleta watu pamoja bila kujali jinsia, lugha, dini na nchi.

Alisema kuwa kipindi hicho cha runinga kinachojumuisha nchi za Afrika Mashariki, kati na Magharibi kitawahusisha wanamuziki wa miondoko ya aina tofauti tofauti kutoka sehemu mbalimbali ili kupata mchanyato wa kisasa wenye asili ya Afrika.

Tuesday, October 1, 2013

WANAWAKE WAANDAMANA

NCHI ya Nigeria inakumbwa na uhaba wa wanaume wanaohitaji kuoa hali iliyosababisha wanawake zaidi ya elfu nane kuandamana.

Lengo la maandamano yao ni kushinikiza serikali kuwasaidia waolewe kutokana na uhaba wa wanaume hao uliojitokeza nchini humo.

Maandamano hayo yaliyofanyika nchini humo yalikuwa na nia ya kutatua tatizo hilo ingawa haikuweka wazi ni njia gani zitakazotumika kutatua uhaba huo wa wanaume.

Wanawake wengi walijitokeza katika maandamano hayo ambapo jumla ya wanawake 5380 waliopewa talaka, 2200 wajane, 1200 yatima, na 80 wengine kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.

Wanawake hao walidai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku hali inayopelekea kuhitaji kuolewa ili waweze kupata msaada kutoka kwa wanaume hao.

MAHALI YA WANAWAKE INAONGEZA UKATILI

IMEELEZWA kuwa  ukatili dhidi ya wanawake  katika ndoa unatokana na  kigezo cha
kulipiwa mahali ambayo imekuwa ikigeuka  kuwa ni adhabu  na chanzo cha mateso.

Hali hiyo imebainika kuwa  haitoi usawa  ndani ya jamii  kwani  mwanaume anaonekana yupo  juu na mwanamke kuwa chini  kutokana na wanaume kuwaona wanawake ni  mali yao Hayo yalielezwa jana na mwezeshaji  Fortunata Makafu  wakati akizungumza kwenye mafunzo ya siku mbili wilayani Chamwino yaliyoandaliwa na Wowap kwa kushirikiana na shirika la Tunaweza na oxfam kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali, dini, watmaalufu, polisi na watendaji wa kata na vijiji.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa shirika hilo limekuwa likitoa elimu kwa jamii ilkuepuka ukatili huo  na mafanikio mbalimbali yamenza kuzaa matunda.Alisema kuwa hivi sasa  kuna unafuu mkubwa  katika  kushughulikia  ukatili wkijinsia  kutokana na jeshi hilo  kuweka dawati la jinsia.

MTOTO WA MIAKA MIWILI AJIFUNGUA

MTOTO wa miaka miwili wa nchini China, amejifungua baada ya madktari kugundua kuwa anamimba isiyokuwa.

Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Xiao Feng alijifungua kwa njia ya upasuaji mara baada ya madkati hao kugundua kuwa anaujauzito huo usiokuwa.

Xiao alipelekwa hospitali mara baada ya tumbo lake kuwa kubwa hali ambayo ilimsababishia matatizo ya upumuaji ndipo madktari walipoamua kumfanyia uchunguzi.

MSHITAKIWA AACHIWA HURU KWA FAINI YA 1000

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemlipisha faini ya Sh.1000 raia wa Kenya Joshua Mulundi baada ya kumtia hatiani katika kesi ya kuidanganya polisi kuhusika kumteka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka iliyokuwa ikimkabili.

Shauri hilo jana lililetwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Aloyce Katemana, kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali ambapo baada ya kusomewa maelezo hayo na upande wa mashtaka, Mhindi alikiri kutenda kosa na mahakama kumpa adhabu hiyo au kifungo cha miezi sita gerezani.

Hakimu Katemana aliieleza Mahakama hiyo kuwa baada ya mshtakiwa kukiri maelezo yote ya kosa,inamtia hatiani na kumsomea hukumu pamoja na adhabu.

Akisoma hukumu hiyo,alisema amezingatia maelezo ya upande wa mashtaka na maelezo ya mshtakiwa alipokuwa akiililia mahakama na hivyo kumpa adhabu ya kulipa faini ya Sh.1000 au kwenda gerezani miezi sita.

Saturday, September 28, 2013

JA RULE KURUDI KWA KISHINDO


Rapa wa Marekani Ja Rule, amejichimbia kwenye studio akirekodi nyimbo mbili tofauti ambazo amejipanga kuziachia kabla ya mwisho wa mwaka.

Rapa huyo ambaye yupo bize na muziki wakati wote hadi kushindwa kuzungumza na watu pamoja na vyombo vya habari akidai kwamba muda wa kufanya hivyo utakapowadia atafanya hivyo.

Pamoja na hayo habari zinadai kuwa tayari amesharekodi singo yake ya pili kwa kipindi cha muda mfupi tangu alipoachiwa kutoka jela.

Friday, September 27, 2013

NGASSA KUWALIPA SIMBA MWENYEWE


Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Mrisho Ngassa ameamua kulipa mwenyewe deni lake la Sh45 milioni anazotakiwa kuilipa klabu ya Simba baada ya kuhukumiwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Awali Ngassa alikuwa ameweka ‘ngumu’ kulipa fedha hizo na kuzua tafrani kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kuhusiana na adhabu yake ya kulipa fidia iliyotolewa na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi ya Wachezaji ya TFF.

Kamati hiyo ilimfungia Ngassa kucheza mechi sita, adhabu ambayo amekwisha itumikia na kilichobakia sasa ni kulipa fedha hizo ili aweze kucheza mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

LUGHA YA MATUSI YAUPOTEZA MUZIKI WA MDUARA

Muimbaji wa bendi ya Njenje 'Wananjenje' John Kitime ameweka wazi sababu zinazopelekea muziki wa mduara kukosa soko na kushindwa kupata nafasi ya kupigwa kwenye vyombo vya habari.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii aliweka wazi kuwa sababu moja wapo ya nyimbo za mduara kukosa soko ni kutokana na maneno ya matusi yanayotumika katika nyimbo hizo.

Alisema baadhi ya wasanii waliowengi waliojiingiza katika muziki huo wamekuwa wakitumia lugha yenye maneno ya kificho 'matusi' hali inayopelekea kushindwa kupigwa katika redio mbalimbali nchini.

Alisema kuwa waimbaji wanaoibukia hivi sasa wanapoteza maana halisi ya muziki huo wa mduara hali inayopelekea muziki huo kukosa soko.

TUME YA WARIOBA YAANIKA MAZITO

Wakati wananchi wa kada mbalimbali wakishinikiza Rais Jakaya Kikwete kutokusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, kwa maelezo kuwa una kasoro, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye amesema sheria ina upungufu.

Warioba alisema jana kwamba ni jambo la kushangaza sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, wakati huohuo ikieleza kuwa itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni.

Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa Katiba Mpya.

Sheria hiyo ambayo Warioba amesema ina upungufu, muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa wa wabunge Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, ikiwa ni baada ya kubadilishwa kwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema: “Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni?”

KENYA YAMSAKA MWANAMKE ALIYEONGOZA UGAIDI

Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.

Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.Bi Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005 anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.

Polisi wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.

Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.

MSANII JELA KWA KUIMBA MATUSI


Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa muziki wake.

Mahakama ilitupilia mbali kesi yake ya rufaa baada ya yeye na mwanamuziki mwenzake kupatikana na hatia mwezi jana ya kuwatusi maafisa wakuu katika tamasha la muziki eneo la Hammamet.

Wawili hao awali walihukumiwa bila ya wao kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miezi 21 lakini hukumu hiyo iliondolewa. Weld El 15, aliyepatikana na kosa kwa kuimba wimbo wake huo, kuwa 'Ploisi ni Mbwa', hakukata rufaa na sasa yuko mbioni.

Hata hivyo Kaly BBJ lisema kuwa wimbo wao ulikuwa unaelezea hali ilivyo nchini Tunisia na kuhusu serikali.
Muungano wa vyama unaoongozwa na chama cha wanasiasa waisilamu wenye msimamo wa kadri, Ennahda, uliingia mamlakani baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Zine el-Abidine Ben Ali mwezi Januari mwaka 2011 na uchaguzi kufanyika baadaye mwaka huo.
Klay anasemekana kuambia mahakama kuwa wimbo wao unakosoa hali ya sasa serikalini na kote nchini Tunisia tu.

Wednesday, September 25, 2013

MISS TANZANIA AGEUKIA FILAMU


HATIMAYE aliyekuwa Miss Tanzania 2011 Salha Israel ameamua kujitosa katika fani ya uigizaji ambapo teyari ameshaanza kuonekana kwenye moja ya filamu mpya iliyopo chini ya kampuni ya Ray, 'RJ'.

Salha ameonekana katika baadhi ya picha zilizotumwa kwenye mtandao wa Instagram zilizokuwa zikimuonesha akiwa 'location' akirekodi filamu hiyo ambayo amecheza kama mlinzi wa mtoto wa rais.

Akizungumza na jarida hii Jaqueline Massawe 'Wolper' ambaye amecheza kwenye movi hiyo kama mtoto wa rais aliweka wazi kuwa movi hiyo ilimuhitaji mtu anayefanana kama yeye ndiye maana chaguo la kwanza likamdondokea miss huyo.

Alisema kuwa Salha ameweza kuvaa huhusika katika movi hiyo na kuonesha uzoefu kucheza na kamera kama vile alishawahi kuigiza hapo mwanzo.

Salha amecheza kwenye filamu hiyo kama mlinzi wa mtoto wa rais, huku Wolper akicheza mtoto wa rais jina la filamu hiyo bado halijawekwa wazi na siku ya kutoka bado haijajulikana ingawa inasemekana kutoka hivi karibuni.

NDOVU 81 WAUWAWA


Maafisa wa wanyama pori nchini Zimbabwe wamesema kuwa takriban ndovu 81 wameuawa kutokana na sumu ilio mwagwa katika eneo la malisho ya ndovu hao. Tangazo hilo linajiri baada ya maafisa kuzuru mbuga ya wanyama pori ya Hwange mwishoni mwa juma lililopita.

Sumu hiyo ambayo hutumiwa katika migodi ya dhahabu ilimwagwa katika eneo hilo na wawindaji haramu. Tayari wawindaji haramu 9 wamekamatwa. Zaidi ya ndovu 40 walipataikana wameuawa katika mbuga hiyo mwezi uliopita.

KENYA YAOMBOLEZA SIKU 3


Kenya inaanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi. Rais Uhuru Kenyatta pia ameseama kuwa bendera zitapepershwa nusu mlingoti kwa heshima ya waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo.

Watu 67 wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka. Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa wanaungana na wale wa Kenya kujaribu kuondoa mili ambayo imenaswa kwenye vifusi vya jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka jana, nia ni kujaribu pia kutambua uraia wa washambulizi hao.

Baraza la usalama wa kitaifa linatarajiwa kukutana leo kudadisi yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kigaidi.

MWANAMKE AONGOZA SHAMBULIZI LA KIGAIDI


Huku mapambano yakiwa yamepamba moto, anayedaiwa kuwa Kiongozi wa kundi la magaidi lililovamia jengo la kibiashara la Westgate, Samantha Lewthwaite inadhaniwa kuwa ameuawa. Lewthwaite, ambaye anaitwa kwa jina la utani la ‘Mjane Mweupe’ anadaiwa kuongoza shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 62 na kujeruhi wengine 170 mjini Nairobi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mwanamke huyo inasemekana aliuawa juzi usiku na wanajeshi wa Kenya wanaoshirikiana na maofisa wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) na wale wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).

Gazeti hilo lilieleza kuwa mwanamke huyo ambaye ni mjane wa mlipuaji wa kujitoa muhanga, Jermaine Lindsay, aliuawa pamoja na magaidi wengine watatu. Kitendo cha kukutwa kwa mwanamke aliyevalia hijab ndicho kilichowafanya maofisa wa usalama kuamini kuwa mwanamke huyo ameuawa.

Tuesday, September 24, 2013

MAGAIDI WAWILI WAUAWA, IDADI YA VIFO YAFIKIA 62


Wakati magaidi wawili wakiwa wameuawa, Serikali ya Kenya imesema idadi ya watu waliokufa katika tukio la kigaidi kwenye maduka makubwa ya Westgate, Nairobi imefikia 62.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mchana, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph Ole Lenku alisema watu waliojeruhiwa ni 175 baada ya magaidi hao kuvamia eneo hilo la maduka tangu Jumamosi iliyopita.

Ole Lenku alisema pia kuwa askari 10 wamejeruhiwa katika operesheni hiyo inayowahusisha maofisa wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad), wale wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI). Alisema askari waliojeruhiwa na raia wanatibiwa katika hospitali mbalimbali za Nairobi. Magaidi wawili wauawa

Alisema magaidi wawili waliuawa na vikosi vya usalama huku mapambano yakiendelea. Alisema waasi hao wamebanwa baada ya vikosi vya ulinzi na usalama kudhibiti sehemu kubwa ya jengo hilo.

Magaidi hao wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi la Al-Shabaab la Somalia walivamia jengo hilo la ghorofa nne ambalo lina maduka ya kifahari na kuua, kujeruhi na kuwashikilia wengine mateka.

BENDI YA KALUNDE KUVAMIA TEGETA, BOKO


BENDI ya muziki wa dansi nchini inayokuja kwa kasi ya Kalunde, ikiwa katika harakati zake za kuipua albamu yake ya tatu, sasa itakuwa ikitumbuiza katika viwanja vya Tegeta na Boko.Kalunde kwa sasa iko kambini ikijiandaa na albamu yao ya tatu, baada ya zile za Hilda na Imebaki stori ambazo zinatesa katika anga za muziki nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana Rais wa bendi hiyo, Deo Mwanambilimbi alisema wameamua kucheza na viwanja vya Tegeta na Boko kwa kuwa kwa sasa wapo kambini kujiandaa na albamu hiyo mpya. "Tunataka kuwapa vitu adimu wakazi wa maeneo ya Tegeta na Boko kwa kuwa wengi wao wanashindwa kuja katika shoo zetu kutokana na umbali, lakini sasa wana kila sababu ya kujidai," alisema Mwanambilimbi.

Alisema kila Alhamisi kwa sasa watakuwa wanatumbuiza katika Ukumbi wa Hisege ulioko Boko Magengeni na kila Jumamosi uhondo utapatikana kwenye Ukumbi wa Nyama Chabisi Tegeta.

VIKOSI VYA KENYA VADHIBITI JENGO WESTGATE


Hatimaye vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema vimelidhibiti jengo zima la Westgate mjini Nairobi, ikiwa ni zaidi ya siku tatu baada ya jengo hilo kuvamiwa na wanamgambo Milipuko ikifuatiwa na milio ya risasi imesikika kutoka ndani ya jengo hilo asubuhi ya leo huku duru zikisema kuwa vikosi vya usalama vinaelekea kukamilisha operesheni hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, magaidi sita waliokuwa wamesalia wameuawa huku wengine watatu wakiuawa hapo jana.Serikali imesema zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa katika shambulio hilo ambalo Al shabaab imekiri kulitekeleza.

Wizara ya mambo ya ndani imesema wanajeshi wanaendelea kulisaka jengo zima la Westgate kutoka gorofa moja hadi nyingine kuhakikisha kwamba hakuna mateka aliyesalia

Monday, September 23, 2013

HALI ILIVYOKUWA NCHINI KENYA

September 21, ni tarehe ambayo Kenya haitoisahau kamwe. Ni baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab lilipoishambulia mall ya Westgate maarufu kwa kuwa na wateja matajiri jijini Nairobi na kuwashikilia watu mateka, kuwaua na kuwajeruhi wengine.

HALI TETE KUOKOA MATEKA JENGO LA WESTGATE KENYA

HUKU  hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na migahawa zaidi ya themanini.

Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani bado, waliokuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Inaarifiwa kuwa  kuna miili ya watu kumi waliopoteza maisha katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo, aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wapo ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.

Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora. Wapo baadhi ya wakenya  waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi.

Sunday, September 22, 2013

VYAMA VYA UPINZANI VYATIKISA DAR


Vyama vya upinzani jana vilifanya mkutano mkubwa kuwashawishi wananchi kupinga kile walichokiita kuhujumiwa kwa mchakato wa Katiba Mpya, wakitangaza Oktoba 10 kuwa siku ya Watanzania wote kushiriki katika maandamano kushinikiza wapewe haki ya kuandaa Katiba yao.

Wakizungumza kwa kupokezana katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam jana, wenyeviti wa vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF, walieleza kuwa wataendelea kushirikisha taasisi za kiraia kupinga hujuma dhidi ya mchakato wa Katiba Mpya na kwamba hawatakubali endapo Rais Jakaya Kikwete atasaini Muswada wa Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Akizungmza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba alisema chama chake hakitakubali endapo Rais Kikwete atasaini muswada huo kwa kuwa una lengo la kupata Katiba Mpya isiyokuwa na tija kwa taifa. Alisema kuwa Katiba inayoandaliwa ni kwa ajili ya Watanzania wote na siyo kundi la watu, hasa CCM na kwamba mchakato wa kuwapata wajumbe 166 wa Bunge la Katiba kutoka makundi mbalimbali siyo sahihi.

“Haiwezekani kila taasisi ikateuwa wajumbe tisa ambao majina yao yatakwenda kuchakachuliwa na usalama wa taifa, kisha kupata majina ya watu wanaowataka wao, kitu hiki kama CUF hatutakubali,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:

“Hatutarudi nyuma na kukubali kuendelea na mchakato huu endapo Rais atasaini muswada huu. Tutaendeleza harakati za kupinga kwani bila hivyo tutapata Katiba Mpya isiyokuwa na tija.”

Friday, September 20, 2013

IDD AZZAN AWAASA WAHITIMU DARASA LA SABA


MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan amewataka wanafunzi waliomaliza elimu ya darasa la saba wasijidumbukize katika makundi ya madawa ya kulevya na badala yake waendelee na masomo ili wapate mafanikio hapo baadaye.

Hayo alisema juzi katika mahafali ya pili ya darasa la saba katika shule ya msingi ya hekima iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna ushawishi mkubwa wa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kuingia katika vishawishi vya uvutaji wa madawa ya kulevya kwa sababu wanamuda mrefu wanakuwa nyumbani hivyo hujifunza vitu mbalimbali ambavyo vingine ni kujiingiza katika makundi yasiyofaa.

Hivyo aliwataka wazazi na walezi wawapeleke watoto wao shule hata kama hajabahatika kuchaguliwa kujiunga  kidato cha kwanza.

HAKIMU ACHOMWA KISU


Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.

Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia kuwepo mahakamani.

Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000.

Awali, ilielezwa kwamba baada ya tukio hilo la wizi lililotokea Agosti Mosi, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane, mshtakiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi namba 460 ya 2013 kabla ya kuachiwa kwa dhamana Agosti 23, mwaka huu huku kesi yake ikiendelea na pande zote mbili zilitoa maelezo.

WAZIRI SITTA ATEMBELEA KIWANDA CHA BIA SERENGETI



Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisikiliza maelezo kutoka kwa Packaging Manager wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) kilichopo jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea kiwanda hicho kujionea uzalishaji unaofanya pamoja na changamoto zinazozikumba kiwanda hicho.

Thursday, September 19, 2013

KESI YA DAWA ZA KULEVYA YAWATOA JASHO MAWAKILI



Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila au Naima Mohammed Nyakiniwa na wenzake wanane, imeendelea kugubikwa na utata wa kisheria na kuzua mvutano uliosababisha iahirishwe kwa mara nyingine ili kusubiri uamuzi wa Mahakama Jana, Mahakama Kuu ilitengua hoja iliyozua mvutano mkubwa juzi kwa kuruhusu upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi muhimu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Eva Mamuya jambo lililopingwa na upande wa utetezi.

Mbali ya Mama Leila, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Anthony Arthur Karanja na Ben Ngare Macharia (wote Wakenya). Wengine ni Watanzania watano, Sarah Munuo, Almas Said, Yahya Ibrahim, Aisha Kungwi, Rajabu Juma Mzome na John William. Wakati upande wa utetezi ukipinga uamuzi huo wa jana, upande wa mashtaka ulitoa hoja nyingine ya kuongeza shahidi wa pili, ASP Neema na kuibua mvutano mkali wa kisheria uliomlazimu Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo, kuiahirisha hadi Ijumaa wiki hii atakapotoa uamuzi kama upande wa mashtaka ulikuwa sahihi au la kuwasilisha notisi hiyo mahakamani kabla ya uamuzi wa jana.

Ubishi ulianza mapema mahakamani wakati Jaji Mwakipesile alipokuwa akijiandaa kusoma uamuzi wake juu ya maombi ya upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi. Wakili wa utetezi, Yassin Member alisimama na kumwomba jaji kutokusoma uamuzi wake kwani tayari walikuwa na notisi ya upande wa mashtaka ya kuongeza ushahidi wakati ni kinyume cha sheria.

Wednesday, September 18, 2013

MSEMAJI WA BROTHERHOOD AKAMATWA


Msemaji rasmi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood amekamatwa nchini Misri. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali. Gehad al-Haddad alikamatwa akiwa na mwanachama mwingine mmoja wa vuguvugu hilo katika nyumba moja mjini Cairo.

Serikali ya Misri imekuwa ikifanya msako dhidi ya makundi ya kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi Julai.Bwana Haddad aliwahi kuhudumu kama afisa wa ngazi ya juu wa naibu mkuu wa majeshi, Khairat al-Shater, wa vuguvugu hilo na kawaida alizungumza na vyombo vya habari vya kigeni.

Awali, mahakama ya uhalifu mjini Cairo, iliamua kuwa mali zote za viongozi wa vuguguvu hilo pamoja na lile la Gamaa Islamiya kupigwa tanji. Viongozi wa mashtaka waliwaekea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Brotherhood akiwemo, Mohammed Badie, Shater na wengine wengi mnamo mwezi Julai.

SERIKALI KUTOA BARUA KWA BALOZI WA CHINA


Dar es Salaam. Serikali imesema mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanapaswa kutambua kuwa, wanawajibika kuheshimu Mkataba wa Kimataifa wa Vienna unaoainisha taratibu za diplomasia. Pia, inasema inajiandaa kumwandikia barua Balozi wa China nchini, Lu Younqing kutokana na hatua yake ya kujihusisha na mambo ya siasa.

Wiki iliyopita, Balozi Lu alijitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mkoani Shinyanga, huku akiwa amevalia moja ya sare za chama hicho, hatua ambayo imezusha mjadala miongoni mwa vyama vya siasa na wachunguzi wa mambo ya kidiplomasia. Akizungumzia kitendo hicho jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, alisema Serikali inajiandaa kumwandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kwamba itafanya hivyo baada ya kukusanya taarifa zake.

Hata hivyo, Mahadhi alisema Tanzania na China zitaendelea kuwa marafiki wanaoshirikiana kwenye nyanja mbalimbali kwa shabaha ya kuwaletea maendeleo wananchi wake. “Hizi taarifa za balozi kuwa kwenye mkutano wa CCM nami zimezisikia na kuziona kwenye vyombo vya habari, tunachokifanya sasa wataalamu wetu wanaendelea kuzifanyia kazi, baadaye tutamwandikia barua kumkumbusha wajibu wake,” alisema.
Alisema siyo vyema kwa mabalozi kushiriki mambo ya kisiasa, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na Mkataba wa Vienna ambao ndiyo unaotoa mwongozo. Pia, Mahadhi aliasa vyama vya siasa kutoachia majukwaa yao yakitumiwa na wanadiplomasia, akieleza kuwa navyo vinawajibika kuheshimu mkataba huo.
Alisema iwapo pande zote zitaheshimu mkataba huo, hakutakuwa na kurushiana lawama.

MABANDA YA KUONESHA VIDEO MTAANI YANACHOCHEA UBAKAJI


IMEBAINIKA kuwa uwepo wa mabanda ya kuoneshea video mitaani ambayo hayapo kisheria, kumechangia vitendo vya ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo ambao ni wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii mjini Kibaha, umebaini kuwa watoto hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo nyakati za usiku, wanapokuwa wamekwenda kuangalia video ambapo waoneshaji wa video hizo huonesha picha chafu za ngono.

Mabanda hayo ambayo mengi yamejengwa kwa mbao au mifuko ya sandarusi na kuezekwa na makuti au nyasi na yasiyo na mvuto yamekuwa yakionesha picha hizo maarufu kama pilau, kachumbari na ubwabwa na majina mengine ambayo kwa mtu wa kawaida si rahisi kujua maana yake.

Baadhi ya wakazi ambao wamelaani mabanda hayo, ambayo huanza kuonesha video majira ya asubuhi hadi usiku na kusababisha baadhi ya wanafunzi kushinda humo, huku wakiwa wameaga wanakwenda shule na kuishia mabandani na endapo wazazi hawatafuatilia kuna hatari ya wanafunzi kutohudhuria darasani kabisa.

Walilielezea njia wanazotumia wabakaji hao ni kuwalipia kiingilio cha kuangalia picha ambacho ni sh. 500 kwa filamu zitakazooneshwa kwa siku hiyo, ambazo huoneshwa kwa awamu na huchukua kila awamu zaidi ya saa tatu, kisha kubadili picha zingine.

SERIKALI YASHINDWA NA UHALIFU WA TINDIKALI


Matukio ya kumwagiwa tindikali yameendelea kukithiri huku Serikali ikiendelea kutoa ahadi za kudhibiti bila mafanikio. Hivi karibuni baada ya raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali Zanzibar, Serikali iliweka mikakati mikali ya kudhibiti matumizi ya kemikali hiyo, lakini bado matukio hayo yameendelea kuwepo.

Tukio la kumwagiwa tindikali kwa Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang’amba ni mwendelezo wa uhalifu huo ambao Serikali imeshindwa kabisa kuudhibiti. Akieleza jinsi tukio hilo lilivyotokea, Padri Mwang’amba anasema alikuwa nje ya duka linalotoa huduma za mawasiliano ya mtandao (Sun Shine Internet Caffee) liliopo eneo la Mlandege Wilaya ya Mjini Unguja, ndipo alipotokea kijana mmoja na kumwagia tindikali.

Wakati Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na Serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.

Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi. Kwa upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.

Tuesday, September 17, 2013

WABADILISHA JINSIA, WAFUNGA NDOA


UKISTAAJABU ya Mussa unatashangaa kwa yale ya filauni baada vijana wawili waliobadili jinsia zao kuamua kuwa wapenzi. Vijana hao ni kati watu waliojibadili jinsia, 'transgender' wapatao laki tisa nichini Marekani. Kijana Arin Andrews alizaliwa katika jinsia ya kiume, wakati binti Katie Hill alizaliwa katika jinsia ya kike.

Hivi karibuni, Arin alifanyiwa upasuaji wa kuondoa matiti yake (mastectomy) na kuanza kutumia vichocheo vya hormone za kiume (testosterone) ili kujenga umbo la kiume kama anavyoonekana sasa. Alipoulizwa ikiwa hakujali kuwa na makovu kifuani mwake kwa ajili ya kuondoa matiti, alisema alikuwa radhi aishi na makovu kuliko kubeba matiti.

Akizungumza hali hiyo, Arin ambaye awali alitambulika kwa jina la Emerald, alisema asingeweza kufikia hapo ikiwa asingepata upendo na ushirikiano kutoka kwa mpenzi wake, Katie ambaye anayeelewa fika yanayoendelea kwenye kichwa chake. Katie ambaye awali alitambulika kwa jina la Lucas, sasa hunyoa miguu yake ili isiwe na vinyweleo vingi kama mwanaume, jambo ambalo alisema lilimkosesha raha kila mara alipojitizama kwenye kioo kwa kujiona mbaya na asiyevutia.

Mwaka jana, wazazi wa watoto hao wawili waliwakutanishwa, na hapo ndio mapenzi baina yao yalipowaka moto mpaka sasa.

Monday, September 16, 2013

YANGA YAWASILISHA RUFAA YAKE

Klabu ya Yanga tayari imewasilisha rufaa yake kwa shirikisho la soka nchini TFF juu ya kucheza mchezo wake katika hali isiyokuwa na usalama na kuomba mchezo huo urudiwe katika uwanja wa ugenini kwa timu zote.

Mchezo hu ambao ulitawaliwa na vurugu kutoka kwa washabiki wa Mbeya City ulichezeshwa na mwamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ambaye pia hakutoka maamuzi sahihi kwa kukataa bao halali la mshambuliaji Didier Kavumbagu dakika ya 70 ya mchezo.Mashabiki wa Mbeya City walirusha chupa za bia na mawe kwenye bus la timu ya Yanga na kuvunja kioo cha bus kubwa upande wa dereva na kumjeruhi mkononi hali iliyoplekea wachezaji wa Yanga kucheza kwa hofu katika mchezo huo wakihofia usalama wao.

WALIMU WAGOMA UGANDA

Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini Uganda wamegoma hii leo ikiwa siku ya kwanza ya muhula wa tatu na wa mwisho mwaka huu kwa wanafumzi.
Hii ni baada ya matakwa yao ya kutaka wizara ya elimu kuwalipa mshahara zaidi kugonga mwamba.

Walimu hao wanataka nyongeza ya asilimia ishirini pamoja na kuitaka serikali kuboresha mazingira ya kazi.
Mwalimu wa shule nchini Uganda hulipwa dola 98 kwa mwezi wakati mwalimu wa sekondari anapokea dola 176 kila mwezi.

Duru zinasema kuwa walimu waliamua kuwa watafika madarasnai ingawa hawatawafundisha wanafunzi. Hii ni kutokana na madai kuwa serikali inawatisha kuwafuta kazi walimu watakaoshiriki mgomo huo.

OMMY DIMPOZ APAGAWISHA MASHABIKI

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz akicheza na shabiki wake jukwaani katika ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Saalm katika uzinduzi wa video ya Tupogo

Friday, September 13, 2013

MASOGANGE APANDA KIZIMBANI

Mapema Dar es salaam leo Waziri wanchi ofisi ya waziri Mkuu sera na uratibu wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi alisema Serikali inafuatilia kwa karibu kesi zinazowahusisha Watanzania waliopo nje ya  nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za kulevya wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.

Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu ya watendaji  imetumwa nchini Afrika kusini hivi karibu ili kukutana na kina Masogange kujua undani wa kesi yao na imethibitika kuhusika kweli na tuhuma hizo ambapo inasadikiwa leo  kesi yao imesomwa rasmi na kusubiri hatua zaidi za kisheria.

Akizungumzia  taarifa za kukamatwa kwa mwanamichezo Kaniki na Matumla Lukuvi alisema taarifa  hizo zitatolewa ufafanuzi zaidi na Serikali baada ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka nchini  Ethiopia. Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha kupambana na kudhibiti na dawa za kulevya Godfrey Nzoa alisema kati ya timu waliokwenda Afrika kusini ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye alifanikiwa kukaa kwa karibu na wafungwa hao akiwemo Masogange na kubaini kuna siri nzito mgongoni mwa Mwasogange hivyo inahitaji uchunguzi ili mkono wa sheria uweze kuwagusa wote wanaohusika na kutumia wasanii katika janga hilo.

UN WAISHANGAA TANZANIA KUFUKUZA WAKIMBIZI

Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban wakimbizi elfu 25 kutoka Burundi wameondoshwa Tanzania kwa nguvu katika mwezi mmoja uliopita. Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR amesema malori yanayowasafirisha warundi yamekuwa yakivuka mpaka kila siku , huku wahamiaji haramu wengi wakikosa mahitaji muhimu kama vile maji na chakula

Katika wiki za hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikiwarejesha makwao kwa nguvu wale walioelezwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kwa miaka mingi Tanzania iliwahifadhi mamilioni ya wakimbizi waliokuwa wakiyakimbia mapigano katika nchi jirani . Tanzania kwa upande wake inasema watu hao ni wahamiaji haramu wala sio wakimbizi.

SUALA LA MAPADRI KUOA LAJADILIWA

Suala la mapadri wa Kanisa Katoliki kuoa au la, limeibuka upya na tayari limeanza kuzua mijadala mikali duniani. Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea.

Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.

OMBAOMBA, MACHANGUDOA WAKAMATWA

Ombaomba zaidi ya 200 na wasichana wanaofanya biashara ya ngono maarufu kama ‘dada poa’  usiku wa kuamkia jana walikamatwa kwenye operesheni maalumu ya kuwaondoa katika maeneo mbalimbali ya jiji,iliyofanywa kwa ushirikiano wa Polisi na askari wa jiji.

Ombaomba na kinadada hao walikamatwa kwenye Manispaa ya Kinondoni na Ilala ambapo baadaye walihifadhiwa kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa(Sabasaba) kabla ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Jiji kwa makosa ya uzurulaji.

Wednesday, September 11, 2013

WANAWAKE 26 KILA SIKU KUPOTEZA MAISHA TANZANIA

TWAKIMU za hivi karibuni zinaonesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya vifo votokanavyo na uzazi huku wanawake 26 hupoteza maisha kila siku ambapo vifo hivyo asilimia 19 vinachangiwa na utoaji wa mimba usio salama.

Takwimu hizo ziimetolewa na shirika lisilo la kiserikali Marie Stopes (MST) ambapo iliweka wazi kuwa asilimia 16 tu ya vijana ndio walio katika umri wa uzazi wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango

ASILIMIA 23 YA WANAUME WAKIRI KUBAKA

Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu unyanyasaji dhidi ya wanawake imesema takriban robo ya wanaume wamekiri kubaka japo mara moja.

Hata hivyo kulingana na ripoti hiyo mwanaume mmoja kati ya 10 amekiri kumbaka mwanamke ambaye si rafiki yake. Kwa mujibu wa BBC, Wanaume 10,000 kutoka nchi sita walishiriki katika utafiti huo, nchi hizo ni pamoja na Bangladesh, Sri Lanka, Cambodia, China, Indonesia na Papua New Guinea.

Tuesday, September 10, 2013

ASAP ROCKY AKAMATWA

Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani Asap Rocky amekamatwa na polisi baada ya kumpiga shabiki wake wa kike kwenye tamasha la 'Made in America' lililofanyika huko mjini Philadelphia.

Hayo yametokea baada ya msanii huyo kupita mbele ya mashabiki wake hao waliokuwa wakicheza na kisha mmoja kumshika nguo yake ndipo alipogeuka na kumpiga.

Shabiki huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, amesema ameumizwa na msanii huyo na teyari ameshamfungulia kesi ya kujeruhi mwimbaji huyo

Sunday, September 8, 2013

AZONTO YAWAPAGAWISHA WABONGO


MSANII wa Ghana mwenye maskani nchini Uingereza Fuse ODG, juzi alifanikiwa kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa kufanya shoo ya kihistoria, huku akipandisha mzuka kwa mashabiki waliohudhuria shoo hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ustawi wa Jamii.

Msanii huyo anayetamba na kibao cha Azonto pamoja na Antenna aliweza kuwateka mashabiki wake baada ya kupanda jukwaani hapo na kucheza pamoja na mashabiki miondoko hiyo.

Thursday, September 5, 2013

BUNGE LAGEUKA UWANJA WA VITA

UKUMBI wa Bunge leo uligeuka kuwa ulingo wa ngumi baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kutunishiana misuri na askari wa bunge hilo ambapo Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe alipoamliwa kutoka nje na Naibu Spika Job Ndugai.

Hatua hiyo ilitokana baada ya wabunge hao kupiga kura za kukubali au kukataa kuhusu kupitishwa kwa kujadili Mswaada wa Katiba uliopelekwa Bungeni hapo na Serikali ili kuweza kujadiliwa na bunge hilo.

Wabunge hao wa kambi ya upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe walipinga matokeo hayo na kuamua kusimama na wakati huo huo Spika Ndugai aliwataka kukaa chini ili kuendelea na kuchangia hoja za msingi za kujadili mswaada huo.

Wednesday, September 4, 2013

BINTI AMEZA SIMU

WIVU wa kimapenzi umemuweka matatani msichana anayeishi nchini Brazil, Adriana Andrade baada ya kuamua kumeza simu yake ya mkononi ili kumzuia mpenzi wake asisome 'message' katika simu yake.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 amejikuta akilazimika kuumeza simu hiyo baada ya kugundua alikuwa na message za ajabu ambazo zingezua utata pindi mpenzi wake angezisoma.

Habari zilizoripotiwa na mtandao wa Hispania Yipeta zilieleza kuwa msichana huyo aliamua kumeza simu yake ya mkononi baada ya mpenzi wake kutaka kusoma message zilizomo katika simu hiyo.

Mtandao huo uliendelea kuripoti kuwa baada ya tukio hilo msichana huyo alilazimika kufanyiwa upasuaji ili kutolewa simu hiyo tumboni mwake.

MAHAKAMA YARUKA KUWAACHIA WASHTAKIWA DAWA ZA KULEVYA


Mahakama Kuu imewatetea majaji na mahakimu dhidi ya tuhuma zilizotolewa kwao kuwa waliwaachia kwa dhamana washtakiwa wa dawa za kulevya kinyume cha sheria na kuwafanya watoroke. Jaji Kiongozi, Fakih Jundu amesema mahakama haipaswi kubebeshwa lawama katika hilo, bali ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na kutokutimiza masharti ya kisheria wanapofungua kesi mahakamani.

Kauli ya Jaji kiongozi imekuja baada ya shutuma zilizotolewa dhidi yao baada ya chombo kimoja cha habari (jina tunalo) kuandika habari kwa kuwataja kwa majina baadhi ya majaji na mahakama kuwa wamekuwa wakiwalinda washtakiwa wa dawa za kulevya katika kesi ambazo wamekuwa wakizisikiliza.

Shutuma hizo zilihusiana na tukio la hivi karibuni ambapo raia wawili wa Pakistani waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya dawa za kupewa kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu na zimekuwepo taarifa kuwa wametoroka nchini.

WACHIMBA MIGODI WAANZA MGOMO AFRIKA KUSINI


Takriban wachimba migodi 80,000 wa dhahabu nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kuanza mgomo kudai nyongeza ya mishahara.Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa migodini kinataka waongezwe mishahara kwa asilimia sitini.

Sekta ya madini ya dhahabu ndio moja ya sekta kubwa duniani lakini imekuwa ikikumbwa na misukosuko katika miaka ya hivi karibuni huku ile ya madini ya platinum ikijikwamua kutokana na athari za migomo iliyokumba sekta hiyo mwaka jana.Wafanyakazi hao wiki jana walikataa pendekezo walilopewa la nyongeza ya asilimia 6 ambacho ni kiwango cha mfumuko wa bei kwa sasa.

Inakisiwa kuwa migomo hiyo ya wachimbaji migodi ikiwa itafanyika, itapotezea nchi hiyo zaidi ya dola milioni 30 kila siku.Wamiliki wa migodi wanaonya kuwa migomo hiyo huenda ikasababisha migodi ya dhahabu kufungwa na maelfu kupoteza kazi zao kufuatia kushuka kwa bei ya dhahabu.

Wanasema kuwa gharama za uchimbaji dhahabu zimepanda kwani wamelazimika kutumia pesa nyingi zaidi katika shughuli nzima za uzalishaji, Kwa miezi mingi Afrika Kusini ilikuwa nchi yenye kuzalisha zaidi dhahabu ikiwa inazalisha asilimia 68 ya dhahabu yote duniani katika miaka ya sabini.

PUTIN AMEONYA MAREKANI

Rais wa Urusi Vladimir Putin, ameonya Marekani na nchi za Magharibi dhidi ya kushambulia Syria.Alisema kuwa hatua zozote za kijeshi dhidi ya Syria itakuwa ni uvamizi. Lakini kwenye mahojiano na shirika la habari la Associated Press, kabla ya mkutano wa wiki hii wa G-Twenty mjini St Petersburg, bwana Putin alisema kuwa huenda akaunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa ikiwa kuna thibitisho kuwa silaha za kemikali zilitumiwa dhidi ya raia.Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria baada ya kusema kuwa kuna thibitisho kuwa rais Assad ametumia silaha za kemikali dhidi ya wananchi wake.

Putin pia alipuuza wasiwasi kuwa wanariadha au mashabiki wataadhibiwa ikiwa watatoa matamshi yatakayoonekana kuwa propaganda kuhusu mapenzi ya jinsia moja wakati wa michezo ya olimpiki itakayofanyika nchini humo.

Wakati huohuo , maseneta nchini Marekani wameridhia mswada wa azimio linalompa idhini Rais Barack Obama kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi ya Syria. Mswada huo utapigiwa kura wiki ijayo.

MWANAMKE AMEZA HELA

Mwanamke wa kimarekani amelazwa hospitali baada ya kuumia kooni na tumboni wakati akijaribu kutoa kiasi kikubwa cha fedha alizozimeza kwa kutumia ufagio wa kusafisha choo.

Monday, September 2, 2013

MSHINDI REDD'S PHOTOGENTICS APATIKANA

 Mshindi wa Miss Redd's Photogentics (katikati) akiwa amepozi na washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora ya miss Photogenitics. Kinyanganyiro hicho kilifanyika juzi katika hoteli ya Giraff Dar es Salaam

RICHI AWA KIVUTO UZINDUZI FOOLISH AGE


MSANII wa filamu nchini Single Mtambalike 'Richi Richi' amekuwa kivuto katika uzinduzi wa filamu ya Foolish Age uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, baada ya kupanda jukwaani na 'kummwagia' kitita cha fedha msanii mwenzake Elizabety Michael 'Lulu'.

Richi alijikuta akivutiwa na msanii Lulu mara baada ya kuimba kibao cha Yahaya kilichoimbwa na muimbaji Lady Jaydee, mara baada ya kumaliza kuizindua movi yake hiyo ambapo alitoa fursa kwa mashabiki wake waliohudhuria uzinduzi huo kuiangalia kwa dakika 10.

Richi alishindwa kuvumilia mara baada ya kusikia msanii huyo anaimba nyimbo ambayo kwa upande wake inamvutia, hali iliyopelekea kupanda jukwaani na kumwagia kitita cha fedha huku akionyesha kuifurahia nyimbo hiyo.