Friday, October 8, 2010

MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIWETE ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA IKULU.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata keki wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuzaliwa kwake pembeni yake ni Mkewe Mama salma Kikwete na mjukuu wao Karima wakishuhudia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlisha kipande cha keki mkewe Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwake miaka 60 iliyopita.Sherehe hizi zilifanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mmoja wa wajukuu zake kwenye hafla ya kuzaliwa kwake iliofanyika katika viwanja vya taasisi ya WAMA.,kulia kwake ni Mama Salma Kikwete.
Rais Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitakiana afya njema kwa kucheeers mbele ya wageni waalikwa usiku wa kuamkia leo,Rais Kikwete alikuwa akisherehekea siku yake maalum ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 60.
Mh.Jakaya Kikwete akitoa shukurani kwa wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo na kwa waandaaji pia wa shughuli nzima kwa usiku huo.
Mtoto wa Rais Kikwete,Ridhiwani Kikwete akimpa zawadi baba yake na pia kumpongeza kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake,kwenye hafla fupi iliofanyika usiku katika viwanja vya taasisi ya WAMA na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimpa zawadi Mumewe,Mh Kikwete.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh Ally Hassan Mwinyi akiwa ameongoza na Mh Pius Msekwa wakimpa mkono wa pongezi Mh Jakaya Kikwete kwa kutimiza miaka 60 tangu kuzaliwa kwake.
Mh.Jakya Kikwete akiwa karibu na Mh.Iddi Azzan pamoja na wageni waalikwa wakiburudika na makamuzi live ya wana Sikinde.


MH.IDDI AZZAN AITEKA KATA YA MZIMUNI

Mh.Iddi Azzan akiwapa sera wananchi wa kata ya Mzimuni katika uwanja wa Mtambani.
Katibu wa Vijana Mkoa wa Dar-es-salaam akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan katika Uwanja wa Mtambani kata ya Mzimuni.
Mh.Iddi Azzan akimnadi Diwani wa Kata ya Mzimuni Ndugu Mohammed Chambuso wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Mtambani katika kata hiyo.
Chipukizi Mtoto ambaye anaitwa Mohamed akitoa Ujumbe kwa Wananchi akiwataka wakipe  kura nyingi chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani.
Mgombea Udiwani Ndugu Mohammed Chambuso akiwa pamoja na kada wa CCM Ndugu Macdonald wakati wa kampeni  zilizofanyika uwanja wa Mtambani kata ya Mzimuni.
Mh.Iddi Azzan na Katibu wa Vijana na viongoze wangine wakiwa wanafurahia maigizo yaliokuwa yakionyeshwa mbele yao.
Muigiza wa kikundi cha Maigizo cha Mizengwe akitoa  mkono wa salamu kwa wagombea na viongozi wa chama. wakati wa kampeni zilizokuwa zinaendela kataka uwanja wa Mtambani kata ya Mzimuni.
Watu walikuwa wengi uwanjani.
ilikuwa hapatoshi mpaka kwenye miti Watu walipanda.
Wingi wa wananchi na wana CCM wakiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Mtambani, kata ya Mzimuni.

MH.JAKAYA MRISHO KIKWETE AITEKA ZANZIBAR KATIKA KAMPENI ZAKE.

Mh.Jakaya Mrisho Kikwete mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi akihutubia maelfu ya wananchi na wana CCM wa Zanzibar katika uwanja wa Demokrasia (zamani kibanda maiti) huko Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume akipiga chapuo kukiombea ushindi chama cha CCM kwenye mkutano huo wa kampeni wa JK katika uwanja wa Demokrasia, Unguja.
Wasanii maarufu Mh. Temba na Chegge wa TMK Family walikuwepo kumtambulisha JK kwa wananchi wa Unguja.
Uwanja wa Demokrasia ulikuwa mdogo kutokana na wingi wa watu.
Waangalizi wa kimataifa, akiwemo ankal Paschal Mayalla.
Radio Zenj FM ilikuwepo kurusha laivu tukio hili la Mkutano wa JK kisiwani hapo.
Watu walikuwa nyomi uwanja wa Demokrasia, Unguja.
Marlaw naye akipiga honi kwa wapinzani
Barbara na Lilian walikuwepo pia
Msanii aliye juu kabisa visiwani kwa sasa akitumbuiza
wana CCM wakiwa kwenye  skuta zao wakimsubiri JK akitokea Pemba.
Mh.Jakaya Kikwete akiaga uwanja wandege wa Pemba baada ya kumaliza mkutano wake kisiwani hapo.
Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kiwete akisalimiana na mgombea ubunge jimbo la Wawi Mh. Daudi uwanja wa Pemba

Tuesday, October 5, 2010

kampeni ya saidia taifa stars ishinde yazinduliwa jana jijini dar

Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Muhammed Seif Khatib akibandika stika kwenye ramani ya Tanzania kuashiria kuwa kampeni kubwa ya kuhamasisha watanzania waweze kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa katika mchezo wake muhimu dhidi ya timu ya timu ya Taifa ya Morocco hapo jumamosi,Oktoba 9 2010 imezinduliwa rasmi.kati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Dada Teddy na Rais wa TFF, Leodga Tenga wakishuhudia tukio hilo mchana huu. 
Rais wa TFF,Leodga Tenga akitoa ufafanuzi kuhusiana na kiingilio cha mchezo huo utakaofanyika siku ya jumamosi,mbali ya hiyo Tenga amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo na kuwapa moyo wachezaji wa timu ya Taifa na hatimaye kushinda.

Monday, October 4, 2010

MH.IDDI AZZAN AWAOMBA WANANCHI WA HANANASIF WACHAGUE MAFIGA MATATU, KINONDONI

Mh.Iddi Azzan mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia chama cha Mapinduzi akitoa sera zake kwa wananchi wa kata ya Hananasif, akiwaomba wamchague awe mbunge wa Jimbo hilo la Kinondoni ili wapate maisha bora, pia aliwataka wamchague Mh.Jakaya kikwete katika nafasi ya Urais ili aweze kushirikiana nae pamoja na Mgombea Udiwani wa kata hiyo Ndugu Tarimba Abbas.
Mh.Iddi Azzan akimnadi mgombea Udiwani Ndugu Tarimba Abbas wa kata ya Hananasif, katika uwanja wa kampeni wa kata hiyo Jana.
Ndugu Tarimba Abbas mgombea nafasi ya Udiwani kata ya Hananasif akitoa sera zake kwa wananchi wa Kata hiyo. awaomba wananchi wampe  kura nyingi sana Mh.Iddi Azzan na Mh.Jakaya Kikwete ili waendelee kuongoza nchi hii na kuwapatia Watanzania maisha bora.
Mh.Iddi Azzan akimkabizi kadi ya chama cha Mapinduzi mwanadada ambaye alijunga na chama hicho hivi karibuni.
Mh.Iddi Azzan akivishwa skafu na Chipukizi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Hananasif.
Mh.Iddi Azzan akiwa amesimama baada ya kukaribishwa kwenye mkutano wa kampeni zake uliofanyika kata ya Hananasif.
Mh.Iddi Azzan akisimama na kujitambulisha kwa wananchi wa kata ya Hananasif baada ya watoto chipukizi kuta afanye hivyo walipokuwa wanawasilisha ujumbe kwake.
Mh.Iddi Azzan akiwaambia wananchi wa kata ya Hananasifu ikifika Tarehe 31 October "wanachukua wanaweka waaaa" baada ya kuambiwa aseme maneno hayo na Watoto Chipukizi.
Chipukizi watoto wakitoa ujumbe kwa wagombea Mh.Iddi Azzan na Ndugu Tarimba Abbas katika uwanja wa Kampeni Hananasif.
Chipukizi watoto wakitoa mkono wa salamu Kwa wagomba na Viongozi wa meza kuu ya mkutano uliofanyika Hananasif.

Kijana Macdonald akitoa mkono wa salamu kwa wagombea baada ya kutoka kuhutubia kwenye jukwaa la kampeni
Wananchi wakiwa wanashangilia juu ya gari katika uwanja wa mkampeni wa kata ya  Hananasif.

Watoto wakigombania kumsalimia Mh.Iddi Azzan baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Hananasif, Kinondoni.


Saturday, October 2, 2010

MGOMBEA MWENZA URAIS WA CCM DR BILAL AKIHITIMISHA WIKI YA UWT PAMOJA NA KUWANADI WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI WA WILAYA KINONDONI, DAR-ES-SALAAM LEO

Mgombea mwenza Dr. Mohammed Gharib Bilali alihitimisha wiki ya UWT katika viwanja vya Mwinjuma kata ya Makumbusho, Kinondoni.
alisema Chama Cha Mapinduzi kinajivunia umoja huo wa UWT kwani ni moja ya nguzo imara katika chama hicho.
Pia aliupongeza umoja huo kwa juhudi kubwa ya kuwakomboa wakinamama, na kuhakikisha wakinamama wanapata maendeleo na huduma zote muhimu, moja ya huduma hizo ni kupata mikopo yenye masharti ya unafuu zaidi. Na alimpongeza Mh. Jakaya Mrisho kikwete kwa kufungua benki ya wakinamama ili iwasaidie kwa maendeleo yao na kulisimamia taifa lao kwa uzuri zaidi.
Mwisho alimuombea kura Mgombea Urais Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwanadi wagombea Ubunge wote wa wilaya ya kinondoni pamoja na madiwani.
Dr. Mohammed Gharib Bilal akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzan wakati wa kuhitimisha wiki ya UWT.
Mh. Iddi Azzan alipatafursa ya kuwa hutubia wananchi, aidha alimshukuru rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutekeleza ahadi zote alizozitoa kwenye Jimbo la Kinondoni, na kuwataka wananchi wampe tena kura nyingi za ndio ili aendelee kuongoza nchi hii, pia aliwaomba wananchi wamchague yeye kuwa Mbunge wao tena katika Jimbo la kinondoni ili aendelee kushirikiana na kuleta maendeleo kwa wananchi wote. na aliwaombea kura madiwani wote wa CCM katika Jimbo hilo na Wilaya nzima ya Kinondoni.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Mh. Hawa Ngumbi akinadiwa na Dr Mohammed Gharib Bilali katika wiki ya wanawake ya UWT.
Dr. Mohammed Gharib Bilali akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Mh. Angela Kizigha katika katika uwanja wa mkutano wa wiki ya wanawake UWT.
Ndugu Leila Seif ambaye alikuwa Mjumbe wa baraza la wanawake Taifa kupitia Chama cha CUF arudisha kadi CCM kwa Mheshimiwa Dr. Mohammed Gharib Bilal. wakati wa mkutano wa UWT, uliofanyika viwanja vya Mwinjuma, Kinondoni.

Wednesday, September 29, 2010

KATA YA MWANANYAMALA WAMPOKEA KWA KISHINDO MH:IDDI AZZAN.


Mh:Iddi Azzan akimnadi Mgombea Udiwani Ndugu Songoro Mnyonge kwa wananchi wa kata ya Mwananyamala wa kati wa kampeni zilizofanyika hapo jana, aliwaomba wananchi wachague Viongozi wa chama cha Mapinduzi kwa Maisha bora ikiwa nafasi ya Urais Mh:Jakaya Kikwete, Ubunge kwa Jimbo la Kinondoni yeye Mwenyewe Mh:Iddi Azzan na Kata hiyo ya Mwananyamala nafasi ya Udiwani Ndugu Songoro Mnyonge.
Mh:Iddi Azzan Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni akiwa amekaa pamoja na Mgombea Udiwani Ndugu Songoro Mnyonge wakati wa kampeni zilizofanyika kata ya Mwananyamala.
Mh:Iddi Azzan akiwapungia mikono wananchi wa kata ya Mwananyamala wakati akiwasili katika uwanja wa kampeni uliopo katika kata hiyo.
Wananchi wa kata ya Mwananyamala wakimpokea Mh:Iddi Azzan alipokuwa anawasili katika uwanja wa kampeni katika kata hiyo.