Sunday, September 1, 2013
WEMA SEPETU AMTOA MACHOZI MAMA KANUMBA
BAADA ya mama Kanumba Bi. Flora Mtegoa kutunzwa kitita cha sh. laki tano na msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, kitendo hicho kilimtoa machozi mama huyo na kudai kuwa kila anapokutana na baadhi ya wasanii anajikuta kumkumbuka mtoto wake.
Kitendo hiko kilitokea mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa Filamu ya Elizabeth Michael iliyopewa jina la Foolish Age katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo mama Kanumba alijikuta akitokwa na machozi mfululizo mara baada ya kukutana na msanii huyo.
Mama huyo ambaye alijikuta akivutiwa na uchezaji wa Wema ukumbini hapo wakati bendi ya Machozi ikitumbuiza aliamua kumfuata na kutaka kumtunza kutokana na uchezaji wake.
RED CARPERT YA UZINDUZI FILAMU FOOLSH AGE
Msanii wa filamu Rose Ndauka
Msanii wa filamu Chuchu Hansi
Msanii wa filamu Rose Ndauka pamoja na Chuchu Hansi
Msanii wa filamu Wolpa
Msanii wa filamu Wema Sepetu
Mtangazaji wa chanel Ten Salma Msangi
Msanii Kajala Masanja
Msanii wa filamu Chuchu Hansi
Msanii wa filamu Rose Ndauka pamoja na Chuchu Hansi
Msanii wa filamu Wolpa
Msanii wa filamu Wema Sepetu
Mtangazaji wa chanel Ten Salma Msangi
Msanii Kajala Masanja
Tuesday, August 27, 2013
WAKAZI WA MIVINJENI WASHINIKIZA MALIPO YAO
WAKAZI wa Mivinjeni Kurasini wanaotakiwa kuhama kupisha mradi wa uwekezaji wa EPZ wamefunga barabara kuishinikiza Serikali kuwalipa hundi zao na si viwanja. Hali hiyo ilijitokeza leo jijini Dar es Salaam Majira ya Saa tano asubuhi ambapo wananchi walijipanga barabarani na kuzuia magari kupita kuishinikiza serikali kuwalipa fidia ili waweze kuondoka katika eneo hilo.
Akizungumza katika eneo hilo Katibu anayefutilia malipo ya wakazi hao Judith George alisema kuwa wakazi hao wamelala barabarani kutokana na serikali kuwapiga dana dana kulipwa hundi za nyumba zao ili waweze kuhama.
Alisema kuwa Viongozi wa Serikali pamoja na Mwekezaji (EPZ) walifika katika eneo hilo March 13 mwaka huu na kufanya mkutano na wananchi kuhusu uwekezaji katika eneo hilo.
Akizungumza katika eneo hilo Katibu anayefutilia malipo ya wakazi hao Judith George alisema kuwa wakazi hao wamelala barabarani kutokana na serikali kuwapiga dana dana kulipwa hundi za nyumba zao ili waweze kuhama.
Alisema kuwa Viongozi wa Serikali pamoja na Mwekezaji (EPZ) walifika katika eneo hilo March 13 mwaka huu na kufanya mkutano na wananchi kuhusu uwekezaji katika eneo hilo.
WANAFUNZI WOTE WAMEFELI LINERIA
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu. Waziri wa elimu wa Liberia amesema ameshinda kufahamu ni kwa nini hakuna wanafunzi hao wamefeli kiasi hicho.
Zaidi ya wanafunzi elfu ishirini na watano walianguka mtihani huo ambao ungewapa fursa ya kujiunga na chuo kikuu cha Liberia ambacho ni moja ya vyuo vikuu vinavyoendesha na serikali.
Lakini wasimamizi wa chuo hicho wameiambia BBC kuwa wanafunzi hao hawakuwa makini na ufahamu mzuri wa lugha ya Kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini. Taifa la Liberia linaendelea kujinasua kutokana na athari za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyomalizika zaidi ya miaka kumi iliyopita.
MWEKEZAJI AHADI USALAMA UWANJA WA NDEGE
Dar es Salaam. Mwekezaji Sheikh Salim Abdullah ametangaza kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JNIA) kwa kufunga mashine za kisasa, ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Sheikh Abdullah ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Maendeleo na Uwekezaji ya Al-Harathy ya Oman, alitangaza hatua yake hiyo jana, baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huo, ambapo alisisitiza mashine zilizopo uwanjani hapo kwa sasa uwezo wake kiutendaji na kiusalama ni mdogo. “ Mashine hizi uwezo wake ni mdogo, dunia tunayoishi sasa imetawaliwa na magaidi uwanja wa ndege ni eneo muhimu ambalo linapaswa kulindwa kwa uhakika, mizigo inabidi kukaguliwa kwa umakini zaidi kwani wanaweza kuweka mabomu au vitu vingine vya hatari wakasababisha madhara makubwa alisema na kuongeza:
“Nimekuja kuwekeza hapa kwa kuitikia mwito wa Rais Jakaya Kikwete, amechoka sana inabidi sisi tumsaidie, ana nia nzuri ya kuhakikisha nchi hii inakuwa kiuchumi inabidi tumsaidie kuwekeza katika maeneo kama haya” alisema. Katika hatua nyingine mwekezaji huyo ametangaza kuwekeza ndege nane kwenye Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), mradi ambao unatarajiwa kugharimu dola za Marekani 100 milioni.
“ Tunanunua ndege nane ambapo nne ni aina ya Embraer ERJ-175 za Brazil na nyingine nne aina ya Mbombardier,kwa kuanzia tunapeleka vijana 10 wa kitanzania kwenda kusomea jinsi ya kuongoza ndege hizo” alisema. Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro, alieleza kuwa hatua hiyo ni faraja kubwa kwao na wana tumaini itatumiwa vyema kwa manufaa ya kukuza uchumi .
Kwa upande wake,, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema Serikali imefanya kazi kubwa kuvutia wawekezaji hao, ikiwa ni pamoja na kusafisha madeni yaliyokuwepo awali
“Nimekuja kuwekeza hapa kwa kuitikia mwito wa Rais Jakaya Kikwete, amechoka sana inabidi sisi tumsaidie, ana nia nzuri ya kuhakikisha nchi hii inakuwa kiuchumi inabidi tumsaidie kuwekeza katika maeneo kama haya” alisema. Katika hatua nyingine mwekezaji huyo ametangaza kuwekeza ndege nane kwenye Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), mradi ambao unatarajiwa kugharimu dola za Marekani 100 milioni.
“ Tunanunua ndege nane ambapo nne ni aina ya Embraer ERJ-175 za Brazil na nyingine nne aina ya Mbombardier,kwa kuanzia tunapeleka vijana 10 wa kitanzania kwenda kusomea jinsi ya kuongoza ndege hizo” alisema. Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro, alieleza kuwa hatua hiyo ni faraja kubwa kwao na wana tumaini itatumiwa vyema kwa manufaa ya kukuza uchumi .
Kwa upande wake,, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema Serikali imefanya kazi kubwa kuvutia wawekezaji hao, ikiwa ni pamoja na kusafisha madeni yaliyokuwepo awali
WANAJESHI WA UN WASOMBWA NA MAJI DARFUR
Wanajeshi wanne wa kutunza amani wa Umoja katika eneo la Darfur nchini Sudan hawajulikani waliko baada ya kusombwa na mafuriko. Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa, Rania AbdulRahman, amesema kuwa wanajshi hao walikuwa wakisindikiza msafara wa magari ya kutoa misaada, wakati waliposombwa na maji.
Afisa huyo amesema kuwa wanajeshi wengine wawili walipatikana wakiwa hai na kundi la uokoaji Shirika la Umoja wa Mataifa wa Afya Duniani WHO, limesema kuwa zaidi ya watu laki tatu nchini Sudan, wameathiriwa na mafuriko na zaidi ya watu hamsini wamefariki mwezi huu.
Shirika hilo limesema kuwa eneo linalokaribia mji mkuu wa Khartoum ndilo limeathirika zaidi na mafuriko hayo ambayo ndiyo mabaya zaidi kuwahi kukumba eneo hilo kwa zaidi ya miaka ishirini na mitano iliyopita.
Wanajeshi wakwama kwenye mto
Kikosi cha Umoja wa Mataifa na kile cha Muungano wa Afrika katika eneo hilo la Darfur, UNAMID, ndilo kubwa zaidi duniani na lina zaidi ya wanajeshi elfu ishirini.
Wanajeshi hao wa kutunza amani walikuwa wakielekea eneo la Misterei, takriban kilomita hamsini, Kusini Magharibi mwa mji mkuu wa eneo hilo Geneina, na msafara wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, wakati msafara wao uliposomba na mafuriko.
Msemaji wa WFP Amor Almagro amethibitisha kuwa wafanyakazi wa shirika hilo la WFP waliokuwa kwenye msafara huo, watano kati yao raia wa Sudan na wawili wa mataifa ya Kigeni wako salama. Umoja wa Mataifa haujatoa majina au uraia wa wanajeshi hao ambao hawajulikani waliko.
Mwaka uliopita, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, alilieleza baraza la usalama la Umoja huo kuwa wanajeshi watatu kutoka Tanzania walizama majini baada ya gari lao la kijeshi, kukwama katika mto mmoja nchini Sudan.
Katibu huyo mkuu vile vile alilieleza baraza hilo kuwa kikosi chake nchini Sudan kinakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kutosha na vya kisasa, hali ambayo inaadhiriwa juhudi zao za kutunza amani katika eneo hilo la Darfur.
Wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa, wako katika eneo hilo la Darfur, kujaribu kumaliza mzozo uliodumu kwa miongo kadhaa kati ya wanajeshi wa serikali na waasi. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu laki tatu wameuawa kwenye mzozo huo wa Darfur.
CCM YAMTIMUA UWAKILISHI MANSOUR
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), jana iliridhia kumvua uanachama, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mansour Yussuf Himid kutokana na kukiuka miiko ya chama hicho. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa Mansour ambaye hivi karibuni alikuwa waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), amefukuzwa uanachama kutokana na kukiuka mambo matatu.
Aliyataja mambo hayo kuwa ni kushindwa kutimiza malengo ya CCM na kutekeleza malengo ya uanachama, kushindwa kutekeleza wajibu wa uanachama na kukiuka maadili ya uongozi, kuikana na kuisaliti Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015. Kutokana na uamuzi huo, Nape alisema Mansour hatakuwa na nafasi ya kukata rufani mahali popote kwa kuwa uamuzi uliofikiwa jana ni wa kikao cha juu cha mwisho.
URUSSI YAONYA MASHAMBULIZI
Serikali za Urussi na Uchina, kwa mara nyingine tena zimetoa onyo dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa la Syria. Onyo hilo limetolewa huku Marekani na washirika wake wakijadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria, kujibu shambulio lililotokea wiki iliyopita.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urussi amesema, jaribio lolote la kutoshirikisha baraza la usalama la Marekani na kubuni kila alichokitaja kama visingizio ambavyo havina msingi, litakuwa na athari kubwa katika mzozo huo.
Wednesday, August 21, 2013
BROTHERHOOD YALAANI KUKAMATWA KWA KIONGOZI WAKE
Vugu vugu la Muslim Brotherhood limelaani kukamatwa kwa kiongozi wake Mkuu Mohammed Badie, kwa tuhuma za kuchochea ghasia na mauaji.Msemaji wa kundi hilo amesema kukamatwa kwa kiongozi huyo ni njama ya kulipiza kisasi mapinduzi ya umma yaliyomuondoa madarakani Rais wa zamani Hosni Mubarak mwaka wa 2011. Badie alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka makaazi yake karibu na kitovu cha maandamano ya wafuasi wa Brotherhood Mjini Cairo.
Jeshi la Misri lilivunja kambi hizo wiki jana ambapo kulitokea maafa ya raia wengi. Wakati huo huo Aliyekua Makamu wa Rais Mohamed ElBaradei anakabiliwa na mashtaka ya kusaliti imani ya taifa.
Bw ElBaradei aliondoka nchini Misri baada ya kujiuzulu kufuatia hatua ya jeshi kuvunja kambi za wapinzani na kusababisha maafa ya mamia ya watu.Utawala wa mpito umetangaza hali ya hatari nchini Misri na kumekua na operesheni kali dhidi ya wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi.
KENYA YASAINI DOLA BILIONI TANO
Kenya imesaini mkataba na China ambao unatoa dola bilioni tano kuimarisha huduma za Reli,Kawi na Uhifadhi wa Wanyama Pori kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.Makubaliano hayo yaliafikiwa katika ziara ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini China.
Hii ndio ziara ya kwanza ya Rais Kenyatta tangu kuchaguliwa hapo mwezi Machi mwaka huu.Serikali ya Kenya imepongeza mkataba huo na kusema utasaidia nchi kukua kiuchumi na kuboresha maisha ya raia wake.Mwenyeji wa Kenyatta, Rais wa ChinaXi Jinping , ameelezea kuridhishwa kwake na juhudi za serikali ya Bw Kenyatta katika kuimarisha taifa la Kenya.
Tuesday, August 20, 2013
MWANAMKE MWENYE NYWELE NDEFU DUNIANI
MWANAMKE anayetambulika kwa jina la Asha Mandela anaongoza kwa kuwa na rasta ndefu zaidi duniani zenye urefu wa futi 55.
Mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuonywa na madakati juu ya urefu wa nywele zake unaweza kumsababishia tatizo la kupooza Asha amedai hawezi kuzikata nywele hizo.
Mama huyo aishiye Atlanta mwenye umri wa miaka 47 anayeweka rekodi ya kuwa na rasta ndefu duniani ameweka wazi humchukua siku mbili kuosha pamoja na kuzikausha nywele zake.
Katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya mwanamke huyo ameeleza kuwa nywele zake zimekuwa ni sehemu ya maisha yake na hatoweza kuzikata kwani akifanya hivyo ni sawa na kujiuua.
SERIKALI YATOA TAKWIMU WAFUNGWA DAWA ZA KULEVYA
SERIKALI imetoa takwimu za mahabusi waliohukumiwa kwa kesi ya dawa za kulevya ambapo takwimu hiyo inaonyesha jumla ya watu 10 wamehukumiwa kwa kipindi cha mwaka 2010,2012.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo.
Monday, August 19, 2013
MAAFISA 24 WA POLISI WAUWAWA
Takriban maafisa 24 wa polisi kutoka Misri wameuawa kwenye shambulizi la kuvizia katika eneo la Rasi la Sinai. Duru zinaarifu polisi hao walikuwa kwenye msafara wa mabasi mawili yaliyoshambuliwa na kundi la watu waliokua na silaha karibu na mji wa Rafa mpaka na Ukanda na Gaza.
Polisi watatu walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Katika siku za karibuni jeshi la Misri limeimarisha operesheni dhidi ya wanamgambo eneo la Sinai hususan baada ya mashambulizi kuongezeka tangu kuanguka kwa uliokua utawala wa Hosni Mubarak mwaka 2011.
Wednesday, August 14, 2013
"HATUNA IMANI NA UCHUNGUZI KUHUSU PONDA
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania umesema hauna imani na tume iliyoundwa na jeshi la polisi nchini humo kwa ajili ya kuchunguza tukio la kupigwa risasi kiongozi wa kidini Sheikh Ponda Issa Ponda. Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Baruan Muhuza Mratibu wa mtandao huo Onesmo Ole Ngurumwa amewaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam leo kuwa jeshi hilo halina haki ya kujiundia tume ikiwa lenyewe ndiyo linatuhumiwa kumpiga risasi sheikh huyo.
Ngurumwa amesema kuwa inasikitisha kuona vyombo vya dola vinaendelea na uvunjaji wa sheria kwa kutumia nguvu inayokiuka haki za msingi za binadamu. Msemaji wa Jeshi la polisi nchini humo Advera Senso ameiambia BBC mjini Dar es Salaam kuwa jeshi lake kwa kushirikiana na jukwaa la haki jinai wameunda kikosi kazi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku akikana kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi na polisi.
Senso amewalaumu wafuasi wa Sheikh Ponda kwa kuwazuia askari kumkamata Sheikh huyo kwa kuwarushia mawe, hatua iliyosababisha askari hao kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya na hata hivyo wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha kiongozi huyo wa kidini. Mapema Jumatatu asubuhi Baraza la waisilamu Tanzania-BAKWATA limeunga mkono kauli ya Jumuiya ya taasisi za kisilamu na kuitaka serikali kuchunguza kwa kina tukio lililosababisha kupigwa risasi kwa Katibu huyo wa Shura ya Maimamu nchini humo.
Kaimu Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhad Mussa Salum amezungumza na waandishi wa habari Mjini Dar es Salaam na kusema kuwa japokuwa BAKWATA imekuwa ikipingana na misimamo ya Sheikh Ponda limesema serikali ilikuwa na nafasi ya kumkamata Ponda kwa kufuata mkondo wa sheria. Sheikh Ponda amekuwa katika mivutano ya mara kwa mara na serikali ya Tanzania, anadaiwa kupigwa risasi baada ya kutokea vurugu kwenye mkutano wa mawaidha ya baraza la sikukuu ya Idd el Fitr Jumamosi jioni.
Awali siku ya Jumapili Mwenyekiti wa Shura ya Maimamu Tanzania, Alhajj Mussa Kundecha, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam kuwa endapo serikali haitachukua hatua itakayowaridhisha Waislamu, wataamua kufikiria upya mustakabali wao na serikali ya nchi hiyo.Sheikh Ponda amelazwa katika hospitali ya Taifa, Muhimbili, mjini Dar es Salaam akiuguza jeraha la risasi huku akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu.
Taarifa za jumuiya hiyo ambayo inajulikana zaidi Tanzania kama Shura ya Maimamu zinasema kuwa Sheikh Ponda ambaye polisi wanasema walikuwa wakimtafuta kwa tuhuma za kutoa matamko ya uchochezi, alisafirishwa usiku kutoka mji wa Morogoro hadi Dar es Salaam zaidi ya kilomita 200.Sheikh Ponda kwa sasa anatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja alichohukumiwa mapema mwaka huu baada ya kukutwa na makosa kadhaa ikiwemo uchochezi wa kuharibu mali za watu.
DAKTARI AIBA HEROIN TUMBONI MWA MGONJWA
Polisi nchini Urusi wamemzuilia daktari mmoja mpasuaji kwa madai ya kuiba kifuko kilichokuwa na dawa ya kulevya ya Heroin kutoka tumboni mwa mgonjwa. Polisi katika eneo la Siberian walimtaka daktari kumfanyia upasuaji mshukiwa ili waweze kunasa dawa hiyo ambayo mgonjwa alikuwa ameimeza. Hata hivyo polisi waligundua kuwa seheme ya dawa hiyo iliyotolewa tumboni mwa mshukiwa ilikuwa inakosekana
Maafisa wa utawala wanadai kuwa daktari huyo alikuwa mlevi walipomkamata. Huenda akafungwa jela kwa miaka 15 ikiwa atapatikana na hatia ya wizi wa dawa za kulevya.
Subscribe to:
Posts (Atom)










