Friday, September 20, 2013
IDD AZZAN AWAASA WAHITIMU DARASA LA SABA
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan amewataka wanafunzi waliomaliza elimu ya darasa la saba wasijidumbukize katika makundi ya madawa ya kulevya na badala yake waendelee na masomo ili wapate mafanikio hapo baadaye.
Hayo alisema juzi katika mahafali ya pili ya darasa la saba katika shule ya msingi ya hekima iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam.
Alisema kuna ushawishi mkubwa wa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kuingia katika vishawishi vya uvutaji wa madawa ya kulevya kwa sababu wanamuda mrefu wanakuwa nyumbani hivyo hujifunza vitu mbalimbali ambavyo vingine ni kujiingiza katika makundi yasiyofaa.
Hivyo aliwataka wazazi na walezi wawapeleke watoto wao shule hata kama hajabahatika kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza.
HAKIMU ACHOMWA KISU
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.
Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia kuwepo mahakamani.
Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000.
Awali, ilielezwa kwamba baada ya tukio hilo la wizi lililotokea Agosti Mosi, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane, mshtakiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi namba 460 ya 2013 kabla ya kuachiwa kwa dhamana Agosti 23, mwaka huu huku kesi yake ikiendelea na pande zote mbili zilitoa maelezo.
WAZIRI SITTA ATEMBELEA KIWANDA CHA BIA SERENGETI
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisikiliza maelezo kutoka kwa Packaging Manager wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) kilichopo jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea kiwanda hicho kujionea uzalishaji unaofanya pamoja na changamoto zinazozikumba kiwanda hicho.
Thursday, September 19, 2013
KESI YA DAWA ZA KULEVYA YAWATOA JASHO MAWAKILI
Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila au Naima Mohammed Nyakiniwa na wenzake wanane, imeendelea kugubikwa na utata wa kisheria na kuzua mvutano uliosababisha iahirishwe kwa mara nyingine ili kusubiri uamuzi wa Mahakama Jana, Mahakama Kuu ilitengua hoja iliyozua mvutano mkubwa juzi kwa kuruhusu upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi muhimu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Eva Mamuya jambo lililopingwa na upande wa utetezi.
Mbali ya Mama Leila, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Anthony Arthur Karanja na Ben Ngare Macharia (wote Wakenya). Wengine ni Watanzania watano, Sarah Munuo, Almas Said, Yahya Ibrahim, Aisha Kungwi, Rajabu Juma Mzome na John William. Wakati upande wa utetezi ukipinga uamuzi huo wa jana, upande wa mashtaka ulitoa hoja nyingine ya kuongeza shahidi wa pili, ASP Neema na kuibua mvutano mkali wa kisheria uliomlazimu Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo, kuiahirisha hadi Ijumaa wiki hii atakapotoa uamuzi kama upande wa mashtaka ulikuwa sahihi au la kuwasilisha notisi hiyo mahakamani kabla ya uamuzi wa jana.
Ubishi ulianza mapema mahakamani wakati Jaji Mwakipesile alipokuwa akijiandaa kusoma uamuzi wake juu ya maombi ya upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi. Wakili wa utetezi, Yassin Member alisimama na kumwomba jaji kutokusoma uamuzi wake kwani tayari walikuwa na notisi ya upande wa mashtaka ya kuongeza ushahidi wakati ni kinyume cha sheria.
Wednesday, September 18, 2013
MSEMAJI WA BROTHERHOOD AKAMATWA
Msemaji rasmi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood amekamatwa nchini Misri. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali. Gehad al-Haddad alikamatwa akiwa na mwanachama mwingine mmoja wa vuguvugu hilo katika nyumba moja mjini Cairo.
Serikali ya Misri imekuwa ikifanya msako dhidi ya makundi ya kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi Julai.Bwana Haddad aliwahi kuhudumu kama afisa wa ngazi ya juu wa naibu mkuu wa majeshi, Khairat al-Shater, wa vuguvugu hilo na kawaida alizungumza na vyombo vya habari vya kigeni.
Awali, mahakama ya uhalifu mjini Cairo, iliamua kuwa mali zote za viongozi wa vuguguvu hilo pamoja na lile la Gamaa Islamiya kupigwa tanji. Viongozi wa mashtaka waliwaekea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Brotherhood akiwemo, Mohammed Badie, Shater na wengine wengi mnamo mwezi Julai.
SERIKALI KUTOA BARUA KWA BALOZI WA CHINA
Dar es Salaam. Serikali imesema mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanapaswa kutambua kuwa, wanawajibika kuheshimu Mkataba wa Kimataifa wa Vienna unaoainisha taratibu za diplomasia. Pia, inasema inajiandaa kumwandikia barua Balozi wa China nchini, Lu Younqing kutokana na hatua yake ya kujihusisha na mambo ya siasa.
Wiki iliyopita, Balozi Lu alijitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mkoani Shinyanga, huku akiwa amevalia moja ya sare za chama hicho, hatua ambayo imezusha mjadala miongoni mwa vyama vya siasa na wachunguzi wa mambo ya kidiplomasia. Akizungumzia kitendo hicho jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, alisema Serikali inajiandaa kumwandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kwamba itafanya hivyo baada ya kukusanya taarifa zake.
Hata hivyo, Mahadhi alisema Tanzania na China zitaendelea kuwa marafiki wanaoshirikiana kwenye nyanja mbalimbali kwa shabaha ya kuwaletea maendeleo wananchi wake. “Hizi taarifa za balozi kuwa kwenye mkutano wa CCM nami zimezisikia na kuziona kwenye vyombo vya habari, tunachokifanya sasa wataalamu wetu wanaendelea kuzifanyia kazi, baadaye tutamwandikia barua kumkumbusha wajibu wake,” alisema.
Alisema siyo vyema kwa mabalozi kushiriki mambo ya kisiasa, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na Mkataba wa Vienna ambao ndiyo unaotoa mwongozo. Pia, Mahadhi aliasa vyama vya siasa kutoachia majukwaa yao yakitumiwa na wanadiplomasia, akieleza kuwa navyo vinawajibika kuheshimu mkataba huo.
Alisema iwapo pande zote zitaheshimu mkataba huo, hakutakuwa na kurushiana lawama.
Alisema iwapo pande zote zitaheshimu mkataba huo, hakutakuwa na kurushiana lawama.
MABANDA YA KUONESHA VIDEO MTAANI YANACHOCHEA UBAKAJI
IMEBAINIKA kuwa uwepo wa mabanda ya kuoneshea video mitaani ambayo hayapo kisheria, kumechangia vitendo vya ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo ambao ni wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii mjini Kibaha, umebaini kuwa watoto hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo nyakati za usiku, wanapokuwa wamekwenda kuangalia video ambapo waoneshaji wa video hizo huonesha picha chafu za ngono.
Mabanda hayo ambayo mengi yamejengwa kwa mbao au mifuko ya sandarusi na kuezekwa na makuti au nyasi na yasiyo na mvuto yamekuwa yakionesha picha hizo maarufu kama pilau, kachumbari na ubwabwa na majina mengine ambayo kwa mtu wa kawaida si rahisi kujua maana yake.
Baadhi ya wakazi ambao wamelaani mabanda hayo, ambayo huanza kuonesha video majira ya asubuhi hadi usiku na kusababisha baadhi ya wanafunzi kushinda humo, huku wakiwa wameaga wanakwenda shule na kuishia mabandani na endapo wazazi hawatafuatilia kuna hatari ya wanafunzi kutohudhuria darasani kabisa.
Walilielezea njia wanazotumia wabakaji hao ni kuwalipia kiingilio cha kuangalia picha ambacho ni sh. 500 kwa filamu zitakazooneshwa kwa siku hiyo, ambazo huoneshwa kwa awamu na huchukua kila awamu zaidi ya saa tatu, kisha kubadili picha zingine.
SERIKALI YASHINDWA NA UHALIFU WA TINDIKALI
Matukio ya kumwagiwa tindikali yameendelea kukithiri huku Serikali ikiendelea kutoa ahadi za kudhibiti bila mafanikio. Hivi karibuni baada ya raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali Zanzibar, Serikali iliweka mikakati mikali ya kudhibiti matumizi ya kemikali hiyo, lakini bado matukio hayo yameendelea kuwepo.
Tukio la kumwagiwa tindikali kwa Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang’amba ni mwendelezo wa uhalifu huo ambao Serikali imeshindwa kabisa kuudhibiti. Akieleza jinsi tukio hilo lilivyotokea, Padri Mwang’amba anasema alikuwa nje ya duka linalotoa huduma za mawasiliano ya mtandao (Sun Shine Internet Caffee) liliopo eneo la Mlandege Wilaya ya Mjini Unguja, ndipo alipotokea kijana mmoja na kumwagia tindikali.
Wakati Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na Serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.
Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi. Kwa upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.
Tuesday, September 17, 2013
WABADILISHA JINSIA, WAFUNGA NDOA
UKISTAAJABU ya Mussa unatashangaa kwa yale ya filauni baada vijana wawili waliobadili jinsia zao kuamua kuwa wapenzi. Vijana hao ni kati watu waliojibadili jinsia, 'transgender' wapatao laki tisa nichini Marekani. Kijana Arin Andrews alizaliwa katika jinsia ya kiume, wakati binti Katie Hill alizaliwa katika jinsia ya kike.
Hivi karibuni, Arin alifanyiwa upasuaji wa kuondoa matiti yake (mastectomy) na kuanza kutumia vichocheo vya hormone za kiume (testosterone) ili kujenga umbo la kiume kama anavyoonekana sasa. Alipoulizwa ikiwa hakujali kuwa na makovu kifuani mwake kwa ajili ya kuondoa matiti, alisema alikuwa radhi aishi na makovu kuliko kubeba matiti.
Akizungumza hali hiyo, Arin ambaye awali alitambulika kwa jina la Emerald, alisema asingeweza kufikia hapo ikiwa asingepata upendo na ushirikiano kutoka kwa mpenzi wake, Katie ambaye anayeelewa fika yanayoendelea kwenye kichwa chake. Katie ambaye awali alitambulika kwa jina la Lucas, sasa hunyoa miguu yake ili isiwe na vinyweleo vingi kama mwanaume, jambo ambalo alisema lilimkosesha raha kila mara alipojitizama kwenye kioo kwa kujiona mbaya na asiyevutia.
Mwaka jana, wazazi wa watoto hao wawili waliwakutanishwa, na hapo ndio mapenzi baina yao yalipowaka moto mpaka sasa.
Monday, September 16, 2013
YANGA YAWASILISHA RUFAA YAKE
Klabu ya Yanga tayari imewasilisha rufaa yake kwa shirikisho la soka nchini TFF juu ya kucheza mchezo wake katika hali isiyokuwa na usalama na kuomba mchezo huo urudiwe katika uwanja wa ugenini kwa timu zote.
Mchezo hu ambao ulitawaliwa na vurugu kutoka kwa washabiki wa Mbeya City ulichezeshwa na mwamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ambaye pia hakutoka maamuzi sahihi kwa kukataa bao halali la mshambuliaji Didier Kavumbagu dakika ya 70 ya mchezo.Mashabiki wa Mbeya City walirusha chupa za bia na mawe kwenye bus la timu ya Yanga na kuvunja kioo cha bus kubwa upande wa dereva na kumjeruhi mkononi hali iliyoplekea wachezaji wa Yanga kucheza kwa hofu katika mchezo huo wakihofia usalama wao.
Mchezo hu ambao ulitawaliwa na vurugu kutoka kwa washabiki wa Mbeya City ulichezeshwa na mwamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ambaye pia hakutoka maamuzi sahihi kwa kukataa bao halali la mshambuliaji Didier Kavumbagu dakika ya 70 ya mchezo.Mashabiki wa Mbeya City walirusha chupa za bia na mawe kwenye bus la timu ya Yanga na kuvunja kioo cha bus kubwa upande wa dereva na kumjeruhi mkononi hali iliyoplekea wachezaji wa Yanga kucheza kwa hofu katika mchezo huo wakihofia usalama wao.
WALIMU WAGOMA UGANDA
Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini Uganda wamegoma hii leo ikiwa siku ya kwanza ya muhula wa tatu na wa mwisho mwaka huu kwa wanafumzi.
Hii ni baada ya matakwa yao ya kutaka wizara ya elimu kuwalipa mshahara zaidi kugonga mwamba.
Walimu hao wanataka nyongeza ya asilimia ishirini pamoja na kuitaka serikali kuboresha mazingira ya kazi.
Mwalimu wa shule nchini Uganda hulipwa dola 98 kwa mwezi wakati mwalimu wa sekondari anapokea dola 176 kila mwezi.
Duru zinasema kuwa walimu waliamua kuwa watafika madarasnai ingawa hawatawafundisha wanafunzi. Hii ni kutokana na madai kuwa serikali inawatisha kuwafuta kazi walimu watakaoshiriki mgomo huo.
Hii ni baada ya matakwa yao ya kutaka wizara ya elimu kuwalipa mshahara zaidi kugonga mwamba.
Walimu hao wanataka nyongeza ya asilimia ishirini pamoja na kuitaka serikali kuboresha mazingira ya kazi.
Mwalimu wa shule nchini Uganda hulipwa dola 98 kwa mwezi wakati mwalimu wa sekondari anapokea dola 176 kila mwezi.
Duru zinasema kuwa walimu waliamua kuwa watafika madarasnai ingawa hawatawafundisha wanafunzi. Hii ni kutokana na madai kuwa serikali inawatisha kuwafuta kazi walimu watakaoshiriki mgomo huo.
OMMY DIMPOZ APAGAWISHA MASHABIKI
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz akicheza na shabiki wake jukwaani katika ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Saalm katika uzinduzi wa video ya Tupogo
Friday, September 13, 2013
MASOGANGE APANDA KIZIMBANI
Mapema Dar es salaam leo Waziri wanchi ofisi ya waziri Mkuu
sera na uratibu wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi alisema Serikali inafuatilia
kwa karibu kesi zinazowahusisha Watanzania waliopo nje ya nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za
kulevya wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.
Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu ya watendaji imetumwa nchini Afrika kusini hivi karibu ili
kukutana na kina Masogange kujua undani wa kesi yao na imethibitika kuhusika kweli
na tuhuma hizo ambapo inasadikiwa leo
kesi yao imesomwa rasmi na kusubiri hatua zaidi za kisheria.
Akizungumzia taarifa
za kukamatwa kwa mwanamichezo Kaniki na Matumla Lukuvi alisema taarifa hizo zitatolewa ufafanuzi zaidi na Serikali
baada ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka nchini Ethiopia. Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha kupambana na kudhibiti
na dawa za kulevya Godfrey Nzoa alisema kati ya timu waliokwenda Afrika kusini
ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye alifanikiwa kukaa kwa karibu na wafungwa hao
akiwemo Masogange na kubaini kuna siri nzito mgongoni mwa Mwasogange hivyo
inahitaji uchunguzi ili mkono wa sheria uweze kuwagusa wote wanaohusika na
kutumia wasanii katika janga hilo.
UN WAISHANGAA TANZANIA KUFUKUZA WAKIMBIZI
Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban wakimbizi elfu 25 kutoka Burundi wameondoshwa Tanzania kwa nguvu katika mwezi mmoja uliopita. Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR amesema malori yanayowasafirisha warundi yamekuwa yakivuka mpaka kila siku , huku wahamiaji haramu wengi wakikosa mahitaji muhimu kama vile maji na chakula
Katika wiki za hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikiwarejesha makwao kwa nguvu wale walioelezwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kwa miaka mingi Tanzania iliwahifadhi mamilioni ya wakimbizi waliokuwa wakiyakimbia mapigano katika nchi jirani . Tanzania kwa upande wake inasema watu hao ni wahamiaji haramu wala sio wakimbizi.
Katika wiki za hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikiwarejesha makwao kwa nguvu wale walioelezwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kwa miaka mingi Tanzania iliwahifadhi mamilioni ya wakimbizi waliokuwa wakiyakimbia mapigano katika nchi jirani . Tanzania kwa upande wake inasema watu hao ni wahamiaji haramu wala sio wakimbizi.
SUALA LA MAPADRI KUOA LAJADILIWA
Suala la mapadri wa Kanisa Katoliki kuoa au la, limeibuka upya na tayari limeanza kuzua mijadala mikali duniani. Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea.
Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.
Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)








