Sunday, September 19, 2010

Iddi Azzan akihutubia katika kampeni Viwanja vya kata ya Ndugumbi

MH:IDDI AZZAN NA MGONJA WASEMA WATAENDELEA KULETA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA WAKISHIRIKIANA MH: JAKAYA KIKWETE.

Mh: Iddi Azzan akielezea sera zake kwa wananchi wa Kata ya Ndugumbi, aidha aliwaeleza wananchi wa Ndugumbi kuwa atahakikisha wanapata maisha bora akishirikiana na Mgonja ambaye ni Diwani wa kata hiyo pamoja na Mh: Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi.
Mh:Salum Londa ambaye ni mjumbe wa halimashauri kuu akimtambulisha Mh:Iddi Azzan  baada ya kupanda kizimbani muda mfupi tu kabla ya kupewa nafasi ya kueleza sera zake.
Mgombea Udiwani kata ya Ndugumbi kupitia chama cha CCM Ndungu Mgonja akielezea sera zake kwa wananchi wa Ndugumbi wakati wakampeni za Jimbo la Kinondoni, kampeni hizo zilianza jana katika viwanja vya kata ya Ndugumbi.
Ndugu Mgonja mgombea Udiwani kupitia chama cha CCM akiwapa mikono viongozi baada ya kumaliza kutoa sera zake kwa wananchi wa Ndugumbi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Ndugu Asha Baraka akiwaombea kura viongozi wa Chama Cha Mapinduzi  CCM  ambao ni Mh: Jakaya Kikwete katika nafasi ya Urais, Mh: Iddi Azzan katika nafasi ya Ubunge Jimbo la Kinondoni na Mgonja katika nafasi ya Udiwani kata ya Ndugumbi wakati wa kampeni zilizofanyika katika Viwanja vya Ndugumbi.
Mgombea Ubunge Jimbo la kinondoni Mh: Iddi Azzan na Mgombea Udiwani kata ya Ndugumbi Ndugu Mgonja wakipokelewa na Umati wa watu wakati wa kampeni zilizofanyika katika viwanja vya Ndugumbi.
 Mh: Iddi Azzan na Ndugu Mgonja wakikaribishwa katika uwanja wa kampeni wa Ndugumbi. wana wandugumbi wakiimba kwa shangwe wakati wa makaribisho hayo.
Wanachama na wananchi wa Ndugumbi wakishangiri na kucheza huku wakiwa teyari kwa kumpokea Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni na Mgonja Mgombea Udiwani kata hiyo ya Ndugumbi.
Wananchi wakishangaa chereko chereko za Upokezi wa Mgombea Ubunge Mh: Iddi Azzan na Mgombea Udiwani Ndugu Mgonja. katika uwanja wa Ndugumbi.
Wanachama wakiwa teyari kuwapokea wagombea

Gari likiwa limerembwa na Picha za Viongozi wa Chama Cha Mapinduizi CCM, hili ni Moja ya magari yaliyokuwepo katika msafara wa kuelekea kwenye kampeni za Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni na Mgombea Udiwani Kata ya Ngumbi.

Iddi Azzan azinduwa Tawi jipya la Umoja wa Wazazi TZ, K/Mikoroshini

MH: iddi Azzan katika mkutano wa UWT na Mama Salma Kikwete

MH:IDDI AZZAN AZINDUWA TAWI LA UMOJA WA WAZAZI TZ, KINONDONI MIKOROSHINI

Mh: Iddi Azzan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Umoja wa Wazazi Tz muda mfupi tu kabla ya kuelekea kwenye kampeni zake katika Uwanja wa Ndugumbi.
Mmoja kati ya wanachama wa Tawi hilo la Umoja wa Wazazi akisoma risala fupi mbele ya Mh: Iddi Azzan.
Mh:Iddi Azzan akipandisha bendera juu kuashiria kuwa Tawi hilo limefunguliwa rasmi.

 
Mh: Iddi Azzan akimpa mkono Mwenyekiti kuashiria kuwa uzinduzi wa tawi hilo umekamilika. 

Mh: Iddi Azzan akigawa kadi kwa mmoja wa wanchama wapya wa Tawi hilo la Umoja wa Wazazi TZ lilopo Kinondoni Mikoroshini

Tawi hili limezinduliwa na Mh: Iddi Azzani Muda mfupi tu akiwa anelekea katika uwanja wa kampeni wa Ndugumbi.
Mh: Iddi Azzan akikaribishwa katika tawi jipya la Umoja wa Wazazi Tz kwa ajili ya kulizinduwa tawi hilo lilopo kinondoni Mikoroshini.


Wanachama wa CCM wakimpokea Mh: Iddi Azzani wakati wa Kufungua tawi jipa la Umoja wa Wazazi lilopo Jimbo la Kinondoni Mikoroshini.
Tawi jipya la Umoja wa Wazazi TZ lilopo Jimbo la Kinondoni Mikoroshi lazinduliwa na Mh: Iddi Azzan kabla ya kwenda kwenye kampeni zake katika uwanja wa kata ya Ndugumbi.

Wednesday, September 15, 2010

Iddi Azzan azinduwa rasmi kampeni zake kinondoni

MH: IDDI AZZAN ASEMA WAPINZANI WASIPEWE NAFASI KATA YA MWANANYAMALA.


Mh: Iddi Azzan akizungumza na wanachama wa CCM wa kata ya Mwananyamala awataka wachague  mafiga matatu ambayo ni Mh: Jakaya Mrisho Kikwete (Nafasi ya Urais), Mh: Iddi Azzan (Nafasi ya Ubunge) na Mwisho wamchaguwe Songoro Mnyonge (Nafasi ya Udiwani) ili kuendelea kuboresha kata hiyo, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Vijan hostel, Kinondoni.
Mh: Iddi Azzan akiwapa mikono wajumbe baada ya kumaliza kuongea na wa wanachama wa CCM kata ya Mwananyamala.
Mwenyekiti wa Jimbo la Kinondoni Mzee Yussuph Sisiyamoto katikati akiongoza mkutano na Kushoto kwake Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni.
Katikati ni Songoro Mnyonge Mgombea udiwani kata ya Mwananyamala akisikilza kwa makini. 

Kada wa CCM na Mkufunzi wa mawakala wa usimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni Faustina Malema akitoa maelekezo mafupi kuhusu suala zima la upigaji kura mwezi October 31. dhumuni kubwa ni kuwataka wanachama wa CCM wasifanye makosa katika upigaji kura huo.

Macdonald ni mmoja kati ya washiriki walioshindwa katika kinyanga' nyiro cha kugombea kiti cha ubunge Jimbo la Kinondoni akiwahamasisha wanachama wa CCM wa kata ya Mwanayamala Kumuunga mkono Mh: Iddi Azzan.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mwananyamala wa kimkaribisha Mh: Iddi Azzan katika ukumbi wa mkutano. Vijana Hostel, Kinondoni.
Wanachama wakimkaribisha Mh: Iddi Azzan alipowasili katika ukumbi wa mkutano wa Vijana hostel, kata ya Mwananyamala.

Mh: Iddi Azzan akipata picha ya pamoja na Mwenyekiti  wa Jimbo la Kinondoni Mzee Yussuph Sisiyamoto wa tatu kutoka kushoto na Katikati ni Mcdonald na wakwanza kulia ni kijana wa Chuo kikuu ambaye anahamasisha vijana katika kampeni za Jimbo la kinondoni za Mh: Iddi Azzan

Mh: Iddi Azzan na M/kiti wa Jimbo la Kinondoni Mzee Yussuph Sisiyamoto wakipata picha ya pamoja na Vijana wa Vyuo vikuu ambao pia ni wanaharakati wa Chama Cha Mapinduzi.

Monday, September 13, 2010

MH: IDDI AZZAN

DR. MRISHO JAKAYA KIKWETE HANA MPINZANI JIMBO LA BUMBULI


Mgombea urais kwa tiketi CCM,Dr. Jakaya Kikwete akipokelewa kwa shangwe na umati mkubwa wa watu na wapenzi wa CCM wa Bumbuli wilani Lushoto Jumatatu jioni katika uwanja wa mkutano wa Togotwe, Bumbuli.

Mgombea ubunge jimbo la Bumbuli January Makamba akimwaga sera baada ya kunadiwa na Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo.

Vilima vyote kuzunguka uwanja wa Togotwe vilifurika watu

Wana Bumbuli wote mkutanoni

 
Wasanii nyota kibao walikuwepo.

Palikuwa hapatoshi Mwanzo Mwisho

MH: IDDI AZZAN ATINGA NDANI YA KATA YA TANDALE LEO.



Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Kinondoni akiwaelezea wanachama wa chama hicho sera na mipango ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika October 31. aidha Mh: Iddi Azzan aliwataka wanachama wa kata hiyo ya Tandale kuwa na Nguvu zaidi, Kasi zaidi ili kuweza kushinda uchaguzi huo. pia aliwaomba kuhakikisha wanachagua Mafiga Matatu yote ya CCM ili kunedeleza kasi ya maendeleo." KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI "
Ndugu Chilumanga Mgombea Udiwani kupitia chama cha Mapidunzi katika kata ya Tandale akijinadi mbele ya wanachama wa chama hicho, Mkutano ulifanyika katika ofisi ya CCM kata ya Tandale.
 
Mzee huyu akiiombea Duwa CCM kisiri siri na kuvuta uradi wakati wa Mkutano wa chama cha Mapidunzi ukiwa unaendelea.

Saturday, September 11, 2010

MH: JAKAYA MRISHO KIKWETE AKISHIRIKI SWALA YA EID, TANGA.


Mh: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa swala ya Eid iliyoswaliwa kwenye Msikiti Mkuu wa Riyadh Mjini Tanga leo asubuhi.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akipeana Mkono wa eid na  Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban Simba wakati wa Swala ya Eid iliyoswaliwa katika Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga.Mzee Mwinyi ndiye mgeni Rasmi katika Baraza la Idd litakalofanyika kitaifa mjini Tanga.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa Swala ya Eid iliyoswaliwa katika Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga.