Thursday, October 28, 2010

MHE.ALI HASSAN MWINYI AMNADI MBUNGE WA KINONDONI.

Mhe.Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu akisiitiza kwa Wananchi kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi na Kumchagua Mgombea Urais Mhe.Jakaya Kikwete Gari kubwa, Mbunge na Madiwani katika Mkutano wa kampeni uliofanyika Magomeni makuti viwanja vya CCM. 
Rais Mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan katika kata ya Mgomeni(Uwanja wa Nyumbani) ndiko anakotokea Mhe.Iddi Azzan.
Mgomba Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwahutubia Wananchi na kuwaeleza sera zake ikiwa ni kuboresha Vituo vya Afya,barabara,Elimu,Maji na kujenga Zahanati kwa kila kata. Pia akiwaomba Wananchi Kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi kuanzia Urais Mhe.Jakaya kikwete, Mbunge kwa Jimbo la Kinondoni yeye mwenyewe Mhe.Iddi Azzan na Madiwani wote wa kata zote za Jimbo hilo.
Rais mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi akiwani Wagombea Udiwani kuanzia (Kulia) Mgonja kata ya Ndugumbi, Husna Kata ya Kinondoni na Mwisho (kushoto) Bulembo kata ya Magomeni, akiwaomba Wananchi wa wachague ili waweze kushirikia na Mbunge na Rais.
Mhe.Iddi Azzan akimpa mkono Rais Mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi baada ya kumaliza kuhutubia Wananchi waliohudhuria Mkutano huo wa kampeni.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea ubunge Mhe.Iddi Azzan.

 Mtu nyomiiii.
Wananchi wakiwa wametulia kusikiliza yaliyo anadaliwa.
 Waigizaji wa Mizengwe wakiburudisha...!
 Chipukizi Mohammed akiwaburudisha Wananchi kwa Sera zake za kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi
Kikundi cha wa kina dada kikiburudisha jukwaani kwa nyimbo ya alajiiiii.




DR.GHARIB BILALI AFANYA KAMPENI KIJITONYAMA,DAR

Mheshimiwa DR.Mohammed Gharib bilali akiwahutubia Wananchi katika Viwanja vya Shule Kijitonyaama,sera yake ilikuwa inahusu kutengeneza vitabu vya Sayansi mashuleni ili kuwapa urahisi Wanafunzi kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Pia alimuombea kura Mgombea Urais Mhe.Dr.Jakaya Kikwete, Wabunge na Madiwani. Wote wa CCM.
Mgombea Mwenza Dr.Gaharibu Bilali akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan katika Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Shule Kijitonyama.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwasalimia Wananchi na kugusia sera zake za kuboresha makazi, huduma za afya na Elimu. Aidha aliwaomba Wananchi ridhaa ya kumchagua tena ili kuendelea kuwaletea maisha bora.
Mhe.Dr.Mohammed Gharib Bilali akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Kijitonyama Ndugu Bulembo ili kuweza kuiongoza kata hiyo.
Mke wa mgombea Mwenza, Bi-Zakia Bilali akiwaombea kura Viongozi Wote Wa CCM Kuanzia Urais DR.Jk , Wabunge na Madiwani Wote.
 Bi-Zakia Bilali akiwa amekaa karibu na Mwenyekiti wa Wilaya ya kinondoni wakimsikiliza Mgombea Mwenza Mhe.Dr.Mohammed Gharib Bilali.
Mhe.Iddi Azzan akiwa meza kuu akisikiliza kwa makini Hotuba ya Mhe.Dr.Gharib Bilali.
Wananchi wakisalimiana na Mhe.Iddi Azzan baada ya kumalizika kwa mkutano.
Baadhi ya Vijana wakimweleza kitu Mhe.Iddi Azzan.
Mhe.Iddi Azzan akionekaniwa mwenye furaha wakati akisalimia na Wananchi huku Mhe.Asha Baraka akionekaniwa mwenye kushanga kitu,baada ya kumalizika kwa mkutano wa kamepeni za Mgombea
 mwenza zilizofanyika katika viwanja vya shule Kijitonyama.

Wednesday, October 27, 2010

KATA YA HANANASIF BABU KUBWA KWA MHE.IDDI AZZAN

Mhe.Iddi Azzan akihutubia umati wa Wananchi wa Kata ya Hananasif akiwaeleza sera zake ikiwa ni kuboresha makazi holela, barabara, maji na kusimamia sheria za watoto iliyotungwa mwaka (2009).  
 Mjumbe wa Halimashauri kuu Mzee Hanzuruni akimuombea duwa Mhe.Iddi Azzan.
Mhe.Iddi Azzan akiwa jukwaani akimwaga sera zake kwa Wananchi wa kata ya Hananasifu.
Mmoja wa makada wa CCM Kijana Macdonald akiwahamasisha Wananchi kukipigia kura chama cha Mapinduzi.
Mgeni rasmi Mzee Hanzuruni akigawa kadi ya Chama Cha Mapidunzi kwa Mwanachama mpya katika mkutano huo wa kampeni. 
Mhe.Iddi Azzan akiwasalimia Wananchi wa Kata ya Hananasifu baada ya kuwasili hapo.
Wananchi walivyo furika kata ya Hananasifu. 
Viongozi wachama walizungukwa kila kona....!
Mtu kibaoooo...! 
 Wasaniii wa Fataki wakiburudisha jukwaani
Nafasi kulikuwa hakuna.
Watoto wakigombania kuushika mkono wa Mhe.Iddi Azzan



Watu nyomiiiii

Tuesday, October 26, 2010

MHE.IDDI AZZAN ARUDI KATA YA NDUGUMBI KWA MARA YA PILI.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Mhe.Nape akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Ndugumbi.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwahutubia Wananchi wa Kata ya Ndugumbi wa kati wa mkutano wake wa kampeni.

 Mhe.Nape akimnadi Mgombea Udiwani wa kata ya Ndugumbi Ndugu Mgonja.
 Mjumbe wa Halmashauri kuu taifa Mhe.Nape akiwahutubia Wana ndugumbi katika mkutano wa kampeni.
 Mhe.Nonda akiwahutbia Wananchi wa kata ya Ndugumbi.
 Chipikizi Mohammed akitoa mashairi yake kwa Wananchi wa kata ya ndugumbi.
 Mhe.Iddi Azzan akipeana mikono na Mjumbe wa Halimashauri kuu Mhe.Nape baada ya kuwasili hapo mkutanoni.
Mhe.Nape na Mhe.Iddi Azzan wakionekaniwa kuvutiwa na wasanii waliokuwa wakiburudisha hapo uwanjani.


 Wasanii wa kucheza na nyoka wakiwa uwanjani kuonyesha mbwembwe zao.
 Wananchi wakiwa katika hali ya kuburudika
 Mmoja wa wasambazaji wa Maji yenye Chata la CCM. Ndugu Aisha akiwa uwanjani kusambaza maji hayo.
Wananchi wakimsindikiza Mhe.Iddi Azzan na Ndugu Mgonja katika ofisi ya kata baada ya kumaliza mkutano.

MHE.IDDI AZZAN AFUNGUWA SHINA LA NGUVU KAZI.

Mhe.Iddi Azzan akilifungua shina hili la Nguvu kazi lilopo kata ya Ndugumbi.
Mhe.Iddi Azzan akilifungua shina hilo kwa kuondoa kitambaa ambacho kili funikiwa shina hilo.
Mhe.Iddi Azzan akipandisha bendera baada ya kulifungua shina hilo la Nguvu Kazi.
 Shina likonekaniwa katika mtazamo wake baada ya kufunduliwa rasmi na Mhe.Iddi Azzan.

Mhe.Iddi Azzan akiwa anapewa maelezo mafupi kuhusu shina hilo.