Beki wa timu ya Atletico Paranaense,Bruno Costa De Souza akijaribu kuondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake katika mechi iliyochezwa jioni hii dhidi timu ya Simba ya jijini Dar,ndani ya uwanja wa Taifa.hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa ni Simba 1-1 Atletico Paranaense.Thursday, January 20, 2011
SIMBA UWEZO SAWA NA ATLETICO PARANAENSE YA BRAZILI WATOKA 1-1
Beki wa timu ya Atletico Paranaense,Bruno Costa De Souza akijaribu kuondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake katika mechi iliyochezwa jioni hii dhidi timu ya Simba ya jijini Dar,ndani ya uwanja wa Taifa.hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa ni Simba 1-1 Atletico Paranaense.Wednesday, January 12, 2011
SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MIAKA 47.
Mh.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein akiwahutubia katika sherehe hizo zilizofanyika katika uwanja wa Amani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na Rais wa Jamuhuiri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho kikwete wakisimama kwaajili ya kupokea maandamano ya sherehe hizo za Mapinduzi katika uwanja wa Amani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein akikaguwa jeshi la polisi wakati wa sherehe za Mapinduzi zilizotimiza miaka 47.
TWANGA PEPETA NA WAPENZI WAKARIBISHA MWAKA 2011, WAZINDUA VIDEO YAO NA BOZI BOZIANA, MH.IDDI AZZAN AKIWA MGENI RASMI
Mgeni rasmi Mbunge wa Kinondoni Mh.Iddi Azzan (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa bendi ya African Stars, Asha Baraka katika ghafla ya kukaribisha mwaka kwa wadau wa bendi hiyo..
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Da'Asha Baraka akimkaribisha mgeni rasmi, Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan kwenye mnuso huo usiku huu
Mh Iddi Azzan akimlisha ndafu Bw. Baraka Msiilwa wakati Da'Asha Baraka akiendelea kukata minofu huku Mama Baraka (kulia) akiweka ndafu sawa
Kikiwa kimetimia, kikosi cha Twanga Pepeta kikitumbuiza vibao vipya na vya zamani. Toka kuume ni mpiga solo mahiri Adolph Mbinga 'Chinga Boy', Rogart Hegga 'Katapilla', Lwiza Mbuttu, Hamisi Amigoras. Janeth IsinikaTANZANIA HOUSE OF TALENT (THT) YATIMIZA MIAKA 5
Vijana wa THT wakiburudisha usiku huu kwenye sherehe za miaka mitano ya Tanzania House of Talent ukumbi wa Mlimani City jijini Dar
Da'Kemi akimuogoza Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr Emanuel Nchimbi wakati wa kuingia ukumbini usiku huu kwa kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 5 ya THT akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa utamaduni Prof Hermus Mwansoko.
Tuesday, January 4, 2011
Remmy Ongala hatimae azikwa.
Mheshimiwa mbunge wa kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwasili katika mazishi ya Mkongwe huyo.
Mheshimiwa Mbunge wa Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwa pamoja na Waziri wa habari na Michezo katika msiba wa Mkongwe huyo Dkt Remmy Ongala
MAREHEMU NGOSHA AZIKWA DAR.
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwa ameketi pamoja na wakongwe wa muziki wa dansi nchini waliokuwa kwenye mazishi ya Charles John Ngosha
Jeneza lenye mwili wa marehemu likipelekwa makaburini Magomeni
Umati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa.
Umati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa.
Umati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa.
| Marehemu Mustafa Ngosha |
Tuesday, December 28, 2010
MHE.JAKAYA MRISHO KIKWETE AMUAPISHA JAJI MKUU MPYA.
kuu na wa Mahakama ya Rufaa katika hafla hiyo
MH.IDDI AZZAN ALA KIAPO CHA UTII, BUNGENI DODOMA
Mhe.Iddi Azzan akipewa pongezi na mmoja wa jamaa zake na baadhi ya wanachi walio kuwepo bungeni
Mmoja wa viongozi wa chama cha CCM akimvisha taji Mhe.Iddi Azzan baada ya kumaliza kula kiapo cha kulitumikia taifa.
Mhe.Waziri Mkuu Mizengo pinda na Mhe.Iddi Azzan wakipiga picha ya pamoja na wananchi baada ya kumaliza kula kiapo cha kulitumikia taifa.
Mhe.Iddi Azzan akipokea mkono wa pongezi.
Baadhi ya viongozi wa chama cha CCM wakipiga picha ya pamoja na Mhe.Mbunge Iddi Azzan.
Mhe.Iddi Azzan akiwa na kijjana wake Ahmed.
Mhe.Iddi Azzan akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wananchi.
Tuesday, December 14, 2010
MHE: JAKAYA MRISHO KIKWETE AKABIDHIWA KOMBE LA CECAFA NA KILIMANJARO STAR.
Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshikilia Kombe la Chalenji baada ya kukabidhiwa na wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara `Kilimanjaro Stars` aliowaalika ikulu jijini Dar es Salaam.

kilimanjaro star wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la challengi cup.

kilimanjaro star wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la challengi cup.

Thursday, December 2, 2010
ASAFIRI KWA BAISKELI GEITA-DAR, KUMPONGEZA RAIS MH:JAKAYA KIKWETE!
Rais Dk. Jakaya Kikwete, akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam, Mussa Lunyeka, kutoka kijiji cha Chabulongo, Kata ya Kasamwa, Geita, wakati alipowasili Ikulu kumpongeza Rais kwa kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Kijana huyo mkulima, aliyesafiri kwa baiskeli kutoka Geita kuja Dare s Salaam, alipata wasaa wa kuzungumza na Rais Kikwete ambaye alimpongeza kwa moyo wake wa uzalendo na kuahidi kumpatia msaada wa kuboresha shughuli zake za kilimo.
Friday, November 19, 2010
MHE.IDDI AZZA NDANI YA BUNGE
Mh.Iddi Azzan akiwa na Mhe.Steven Wasira wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa bunge.
Mhe.Iddi Azzan akiwa nje ya ukumbi wa bunge na baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi baada ya kwisha kuapishwa.
Mhe.Iddi Azzan akiwa na kijana wake Ahmed Nje ya Kumbi wa Bunge kabla ya kwenda kuapishwa.
Mhe.Iddi Azzan akimpongeza Mama Anne Makinda baada ya Kuchaguliwa Kugombania nafasi ya Uspika kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Tuesday, November 2, 2010
MHE.IDDI AZZAN ASHINDA KWA KISHINDO JIMBO LA KINONDONI.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi akimkabidhi Cheti Mhe.Iddi Azzan Cha Kuthibitisha kuwa yeye ndio mshindi wa Ubunge Jimbo hilo la Kinondoni. kwa idadi ya kura 51,372, wa pili CHADEMA kwa kura 27,355 wa tatu CUF kwa kura 22,660 na wanne Dp kwa kura 210.
Mhe.Iddi Azzan akiwapa Mikono Viongozi wa Tume ya Uchaguzi
Wana CCM na Wananchi wakisikiliza matokeo ya Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni.
Mhe.Iddi Azzan akiwa amesimama pamoja na watu wake wakaribu wakisubiri kusikiliza matokeo ya Jimbo hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)



















