Sunday, May 22, 2011

MH. IDDI AZZAN AKABIZI MEZA YA SHULE SECONDARI YA KAMBANGWA KINONDONI.

 Mh. Idd Azzan akiongea na wanafunzi kabla hajakabidhi meza hiyo.
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Idd Azzan, amekabidhi msaada wa meza ya maabara katika Shule ya Sekondari Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya ahadi zake alizotoa katika shule hiyo.
Akiongea kabla hajaenda kukabidhi meza hiyo, mbunge huyo alisema kwa muda mrefu alisikia kilio cha wanafunzi wa shule hiyo kuhusu vifaa vya maabara hivyo kwa kuanzia tu ametoa meza yenye vifaa vya maabara yenye thamani ya shilingi milioni 5,950,000/=.
    Naye mkuu wa shule hiyo, Bi Gaudencia Kimario, alimshukuru Azzan kwa msaada wake huo na kumwomba ashughulikie swala la hati ya jengo, umeme na komputer ambapo alikubali ombi hilo na kuahidi kulishughulikia mara moja.   
    Wanafunzi wa kikundi cha ngoma wakitoa burudani.
    Wanafunzi wakimsikiliza Mheshimiwa. 
     Mheshimiwa Iddi Azzan akizindua rasmi meza hiyo
    Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameketi katika meza hiyo kwa kuonyesha utumikaje wake.
    Mwalimu mkuu, Gaudencia Kimario, akikabidhi zawadi kwa Mh. Azzan.

    1 comment:

    1. Ni vizuri unapokumbuka wajibu wako n hongera kwa hilo,mungu akubariki Mh.Azan..!!!

      ReplyDelete