Monday, January 24, 2011

MHE.IDDI AZZAN MGENI RASMI KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI DHIDI YA WASHIRIKI MISS UTALII 2010/2011

Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azzan akisalimiana na washiriki wa Miss Utalii Tanzania Kaskazini wakati wa Mchezo wa Kirafiki Dhidi ya warembo wa Mashariki.
Washiriki Miss Utalii Tanzania- Kusini na Magharini kabla ya mchezo wao wa mpira wa miguu.
washiriki Miss Utalii Tanzania 2010/2011
wakila tizi katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar.
Washiriki Miss Utalii wakicheza mechi yao wenyewe kwa wenyewe.

Thursday, January 20, 2011

SIMBA UWEZO SAWA NA ATLETICO PARANAENSE YA BRAZILI WATOKA 1-1

Beki wa timu ya Atletico Paranaense,Bruno Costa De Souza akijaribu kuondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake katika mechi iliyochezwa jioni hii dhidi timu ya Simba ya jijini Dar,ndani ya uwanja wa Taifa.hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa ni Simba 1-1 Atletico Paranaense.
Kiungo wa timu ya Simba,Patrick Ochen akiwatoka mabeki wa timu ya Atletico Paranaense katika mchezo uliochezwa jioni hii ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.
 

Wednesday, January 12, 2011

SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MIAKA 47.

Mh.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein akiwahutubia katika sherehe hizo zilizofanyika katika uwanja wa Amani.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakibadilishana mawazo wakati wa kuazimisha sherehe za Mapinduzi miaka 47.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na Rais wa Jamuhuiri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho kikwete wakisimama kwaajili ya kupokea maandamano ya sherehe hizo za Mapinduzi katika uwanja wa Amani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein akikaguwa jeshi la polisi wakati wa sherehe za Mapinduzi zilizotimiza miaka 47.

TWANGA PEPETA NA WAPENZI WAKARIBISHA MWAKA 2011, WAZINDUA VIDEO YAO NA BOZI BOZIANA, MH.IDDI AZZAN AKIWA MGENI RASMI

Mgeni rasmi Mbunge wa Kinondoni Mh.Iddi Azzan (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa bendi ya African Stars, Asha Baraka katika ghafla ya kukaribisha mwaka kwa wadau wa bendi hiyo..

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Da'Asha Baraka akimkaribisha mgeni rasmi, Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan kwenye mnuso huo usiku huu

Mwenyekiti wa African Stars Entertainment (ASET) group Baraka Msiilwa akizungumza machache
Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan
akitoa shukurani zake katika sherehe hiyo.
Mh Iddi Azzan akimlisha ndafu Bw. Baraka Msiilwa wakati Da'Asha Baraka akiendelea kukata minofu huku Mama Baraka (kulia) akiweka ndafu sawa
Kikiwa kimetimia, kikosi cha Twanga Pepeta kikitumbuiza vibao vipya na vya zamani. Toka kuume ni mpiga solo mahiri Adolph Mbinga 'Chinga Boy', Rogart Hegga 'Katapilla', Lwiza Mbuttu, Hamisi Amigoras. Janeth Isinika
Lwiza Mbutu akiongoza mashambulizi
Super Nyamwela (wa pili kuume) akiongoza safu ya uchezaji ya kinakaka

TANZANIA HOUSE OF TALENT (THT) YATIMIZA MIAKA 5

Vijana wa THT wakiburudisha usiku huu kwenye sherehe za miaka mitano ya Tanzania House of Talent ukumbi wa Mlimani City jijini DarDa'Kemi akimuogoza Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr Emanuel Nchimbi wakati wa kuingia ukumbini usiku huu kwa kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 5 ya THT akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa utamaduni Prof Hermus Mwansoko.
Hawa ndio wanaozindua albamu zao kwa pamoja usiku huu,Kutoka kulia ni Linah,Barnaba,Mataluma,Ditto,Mwasiti pamoja na Amin wakiwa katika picha ya pamoja
Waheshimiwa nao walikuwepo kushuhudia burudani kutoka vijana wa THT. Waziri Emmanuel Nchimbi na Mbunge Lowassa na mkewe Regina

Tuesday, January 4, 2011

Remmy Ongala hatimae azikwa.

Mheshimiwa mbunge wa kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwasili katika mazishi ya Mkongwe huyo.
Mheshimiwa Mbunge wa Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwa pamoja na Waziri wa habari na Michezo katika msiba wa Mkongwe huyo Dkt Remmy Ongala
Jeneza la Dkt.Remmy likiwa limewekwa na kuagwa kwa mara ya mwisho.
Mili wa marehemu ukiwasili makaburini.

MAREHEMU NGOSHA AZIKWA DAR.

Wanamuziki katika mazishi ya mwenzao hayati Charles John Ngosha . Toka kulia no Cosmas Chidumule, Mafumu Bilali Bombenfa, Kassim Mapili na aliyejificha kushoto ni Waziri Ally

Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwa ameketi  pamoja na wakongwe wa muziki wa dansi nchini waliokuwa kwenye mazishi ya Charles John Ngosha
Jeneza lenye mwili wa marehemu likipelekwa makaburini MagomeniUmati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,
ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa.
Umati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,
ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa. Umati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,
ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa.
Marehemu Mustafa Ngosha