Wednesday, January 12, 2011

TWANGA PEPETA NA WAPENZI WAKARIBISHA MWAKA 2011, WAZINDUA VIDEO YAO NA BOZI BOZIANA, MH.IDDI AZZAN AKIWA MGENI RASMI

Mgeni rasmi Mbunge wa Kinondoni Mh.Iddi Azzan (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa bendi ya African Stars, Asha Baraka katika ghafla ya kukaribisha mwaka kwa wadau wa bendi hiyo..

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Da'Asha Baraka akimkaribisha mgeni rasmi, Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan kwenye mnuso huo usiku huu

Mwenyekiti wa African Stars Entertainment (ASET) group Baraka Msiilwa akizungumza machache
Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan
akitoa shukurani zake katika sherehe hiyo.
Mh Iddi Azzan akimlisha ndafu Bw. Baraka Msiilwa wakati Da'Asha Baraka akiendelea kukata minofu huku Mama Baraka (kulia) akiweka ndafu sawa
Kikiwa kimetimia, kikosi cha Twanga Pepeta kikitumbuiza vibao vipya na vya zamani. Toka kuume ni mpiga solo mahiri Adolph Mbinga 'Chinga Boy', Rogart Hegga 'Katapilla', Lwiza Mbuttu, Hamisi Amigoras. Janeth Isinika
Lwiza Mbutu akiongoza mashambulizi
Super Nyamwela (wa pili kuume) akiongoza safu ya uchezaji ya kinakaka

No comments:

Post a Comment