Friday, August 5, 2011
Sunday, May 22, 2011
MH. IDDI AZZAN AKABIZI MEZA YA SHULE SECONDARI YA KAMBANGWA KINONDONI.
Mh. Idd Azzan akiongea na wanafunzi kabla hajakabidhi meza hiyo.
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Idd Azzan, amekabidhi msaada wa meza ya maabara katika Shule ya Sekondari Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya ahadi zake alizotoa katika shule hiyo.
Akiongea kabla hajaenda kukabidhi meza hiyo, mbunge huyo alisema kwa muda mrefu alisikia kilio cha wanafunzi wa shule hiyo kuhusu vifaa vya maabara hivyo kwa kuanzia tu ametoa meza yenye vifaa vya maabara yenye thamani ya shilingi milioni 5,950,000/=.
Naye mkuu wa shule hiyo, Bi Gaudencia Kimario, alimshukuru Azzan kwa msaada wake huo na kumwomba ashughulikie swala la hati ya jengo, umeme na komputer ambapo alikubali ombi hilo na kuahidi kulishughulikia mara moja.
Wanafunzi wa kikundi cha ngoma wakitoa burudani.
Wanafunzi wakimsikiliza Mheshimiwa.
Mheshimiwa Iddi Azzan akizindua rasmi meza hiyo
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameketi katika meza hiyo kwa kuonyesha utumikaje wake.Mwalimu mkuu, Gaudencia Kimario, akikabidhi zawadi kwa Mh. Azzan.
Monday, February 14, 2011
VIONGOZI WA NCHI WAKIOMBA DUWA KATIKA KIFO CHA DEREVA WA IKULU...!
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamo wake Mhe.Mohammed Gharib Bilal na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ndugu Rashid Othmani Kushoto kwenye picha wakisoma Dua ya pamoja kwa ajili ya Mwili wa Marehe Ramadhani Said Mkoma aliyefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Ruvu kwenye msafara wa Mama Salma.
Makamu wa Rais Mhe.Mohammed Gharib Bilali akitoa salamu za pole kwa Wafiwa wa Marehemu.
MANDHARI YA BUNGE.
Hivi ndivyo mandhari ya bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania lilivyo huko dodoma, Waheshimiwa Wabunge wakiwa wamekaa kwa utulivu katika viti vyao wakisikiliza Maswali na Majibu, kutoka kwa Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge.
Monday, January 24, 2011
MHE.IDDI AZZAN MGENI RASMI KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI DHIDI YA WASHIRIKI MISS UTALII 2010/2011
Thursday, January 20, 2011
SIMBA UWEZO SAWA NA ATLETICO PARANAENSE YA BRAZILI WATOKA 1-1
Wednesday, January 12, 2011
SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MIAKA 47.
Mh.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein akiwahutubia katika sherehe hizo zilizofanyika katika uwanja wa Amani.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakibadilishana mawazo wakati wa kuazimisha sherehe za Mapinduzi miaka 47.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na Rais wa Jamuhuiri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho kikwete wakisimama kwaajili ya kupokea maandamano ya sherehe hizo za Mapinduzi katika uwanja wa Amani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein akikaguwa jeshi la polisi wakati wa sherehe za Mapinduzi zilizotimiza miaka 47.
TWANGA PEPETA NA WAPENZI WAKARIBISHA MWAKA 2011, WAZINDUA VIDEO YAO NA BOZI BOZIANA, MH.IDDI AZZAN AKIWA MGENI RASMI
Mgeni rasmi Mbunge wa Kinondoni Mh.Iddi Azzan (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa bendi ya African Stars, Asha Baraka katika ghafla ya kukaribisha mwaka kwa wadau wa bendi hiyo..
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Da'Asha Baraka akimkaribisha mgeni rasmi, Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan kwenye mnuso huo usiku huu
Mh Iddi Azzan akimlisha ndafu Bw. Baraka Msiilwa wakati Da'Asha Baraka akiendelea kukata minofu huku Mama Baraka (kulia) akiweka ndafu sawa
Kikiwa kimetimia, kikosi cha Twanga Pepeta kikitumbuiza vibao vipya na vya zamani. Toka kuume ni mpiga solo mahiri Adolph Mbinga 'Chinga Boy', Rogart Hegga 'Katapilla', Lwiza Mbuttu, Hamisi Amigoras. Janeth Isinika
TANZANIA HOUSE OF TALENT (THT) YATIMIZA MIAKA 5
Vijana wa THT wakiburudisha usiku huu kwenye sherehe za miaka mitano ya Tanzania House of Talent ukumbi wa Mlimani City jijini DarDa'Kemi akimuogoza Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr Emanuel Nchimbi wakati wa kuingia ukumbini usiku huu kwa kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 5 ya THT akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa utamaduni Prof Hermus Mwansoko.
Tuesday, January 4, 2011
Remmy Ongala hatimae azikwa.
Mheshimiwa mbunge wa kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwasili katika mazishi ya Mkongwe huyo.
Mheshimiwa Mbunge wa Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwa pamoja na Waziri wa habari na Michezo katika msiba wa Mkongwe huyo Dkt Remmy Ongala
MAREHEMU NGOSHA AZIKWA DAR.
Wanamuziki katika mazishi ya mwenzao hayati Charles John Ngosha . Toka kulia no Cosmas Chidumule, Mafumu Bilali Bombenfa, Kassim Mapili na aliyejificha kushoto ni Waziri Ally
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwa ameketi pamoja na wakongwe wa muziki wa dansi nchini waliokuwa kwenye mazishi ya Charles John Ngosha
Jeneza lenye mwili wa marehemu likipelekwa makaburini MagomeniUmati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,
ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa.

Umati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,
ndugu jamaa na marafiki ulihudhuria. Marehemu Ngosha, aliyefariki juzi akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa mpiga bezi mashuhuri sio tu wa Sikinde bali hata wanamuziki mahili kama Kanda Bongoman walikuwa wakimtumia kutokana na uwezo wake mkubwa. Umati mkubwa wa wanamuziki, wapenzi wa muziki,

Marehemu Mustafa Ngosha |
Subscribe to:
Posts (Atom)