Friday, October 4, 2013

COKE STUDIO YAZINDULIWA AFRIKA

KIPINDI cha muziki kinachojulikana kwa jina la Coke  studio Afrika chazinduliwa rasmi jana huku kikiwa na lengo la kuuboresha muziki wa Afrika uwe wa kisasa na unaolenga vijana.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja bidhaa wa Coca Cola Tanzania, Maurice Njowoka aliweka wazi kuwa studio hiyo inathamini nguvu ya muziki katika kuwaleta watu pamoja bila kujali jinsia, lugha, dini na nchi.

Alisema kuwa kipindi hicho cha runinga kinachojumuisha nchi za Afrika Mashariki, kati na Magharibi kitawahusisha wanamuziki wa miondoko ya aina tofauti tofauti kutoka sehemu mbalimbali ili kupata mchanyato wa kisasa wenye asili ya Afrika.


Aliweka wazi kuwa kwa msimu wa kwanza itawahusisha wasanii nyota wa Afrika ambao ni pamoja na Diamond Platinum, Lady Jaydee hao ni kutoka Tanzania, Salim Keita kutoka Mali, King Sunny Ade Kenya, Hip Hop Panstula kutoka Uganda na wengine kutoka nchi tofauti.

"Coca Cola tunathamini nguvu ya muziki hivyo kupitia Coke Studio tunapata fursa ya kuwaleta kuwakutanisha wasanii wa Afrika pamoja kwa kuboresha muziki wa Afrika uwe wa kisasa na unaolenga vijana, hivyo tunaimani kupata mchanganyiko wa muziki usiosahaulika katika kuimarisha mahusiano na wateja" alisema Njowoka.

Aliongezea kuwa Coke Studio itakuwa inarushwa Kenya, Uganda, Nigeria pamoja na Tanzania ambapo itaenda hewani kwa vipindi vinane vyenye dakika 45, kila kimoja pamoja na masaa mawili ya kipindi maalum cha mwaka mpya.





No comments:

Post a Comment