IMEELEZWA kuwa ukatili dhidi ya wanawake katika ndoa unatokana na kigezo cha
kulipiwa mahali ambayo imekuwa ikigeuka kuwa ni adhabu na chanzo cha mateso.
Hali hiyo imebainika kuwa haitoi usawa ndani ya jamii kwani mwanaume anaonekana yupo juu na mwanamke kuwa chini kutokana na wanaume kuwaona wanawake ni mali yao Hayo yalielezwa jana na mwezeshaji Fortunata Makafu wakati akizungumza kwenye mafunzo ya siku mbili wilayani Chamwino yaliyoandaliwa na Wowap kwa kushirikiana na shirika la Tunaweza na oxfam kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali, dini, watmaalufu, polisi na watendaji wa kata na vijiji.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa shirika hilo limekuwa likitoa elimu kwa jamii ilkuepuka ukatili huo na mafanikio mbalimbali yamenza kuzaa matunda.Alisema kuwa hivi sasa kuna unafuu mkubwa katika kushughulikia ukatili wkijinsia kutokana na jeshi hilo kuweka dawati la jinsia.
Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa ukatilii unaoendelea na hata kuenea zaidi ni ule unaotokana na mira na desturi ambapo kuna jamii bado inaona kuwa ni haki kuoa wake wengi na kuwatumikisha kama vibarua wao wa kutafuta mali.Mwezeshaji huyo alisema kuwa kama jamii inatapata elimu na kuelewa madhara
yatokanayo na ukatili wa kijinsia basi kutakuwa kumesaidia wanawake wengi kuishi
maisha yenye sitaha ndani ya familia zao.
Vile vile alisema kuwa katika kutekeleza mradui huo Tunaweza kwa Tanzania inalenga
kuwafikia watu milioni 16 na ujumbe mkubwa ukiwa ni ukatili dhidi ya wabnawake
haukubaliki ambapo kwa mkoa wa Dodoma mradi huo unatekelezwa kwa wilaya za Chamwino,
Kongwa na Bahi.
No comments:
Post a Comment