Hayo alisema Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika wakati akikabidhi madawati 120 yenye thamani ya shmilioni 12 katika shule zilizoko Kata ya Manzese ambao walikuwa na uhaba wa madawati na kusababisha wanafunzi kukaa chini .
Alisema kuwa walimu wamekuwa wakililia maslahi yao kila siku lakini serikali haiwasikilizi hivyo itasababisha matokeo mabya ya mitihani kila siku.
"Big Result Now inatakiwa kwanza mwalimu aboreshewe maslahi yake ili aweze kutulia kazini na kusababisha hayo matokeo makubwa kwa wanafunzi"alisema Mnyika.
Alisema walimu peke yao ndio watakaowezesha matokeo makubwa kwa wanafunzi hivyo wanatakiwa kuwezeshwa ili wafanye kazi kwa uhakika.
Naye Kaimu afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Doreen Lutahanamilwa alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa shule za kata ya manzese walikuwa na uhaba wa madawati lakini hivi sasa watakuwa na upungufu wa madawati 690 tu .
Alisema kuwa wanafunzi ni lazima wasome katika mazingira mazuri ya kusomea ili waweze kuelewa kile wanachofundishwa kutoka kwa mwalimu wao.
"Mazingira ambayo si rafiki wa elimu yanamfanya mwanafunzi asielewe kile anachofundishwa darasani"alisema Lutahanamilwa
Hivyo amewataka wadau mbalimbali waweze kuchangia madawati na hata vifaa vya shuleni ili wanafunzi waweze kufanya masomo yao vizuri
Madawati hayo yamekabidhiwa katika shule nne ambazo ni Ukombozi,Manzese,Kilimani na Uzuri.
No comments:
Post a Comment