Saturday, October 19, 2013

MECHI YA YANGA NA SIMBA ULINZI WAIMARISHWA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vimejipanga ipasavyo kuakikisha Ulinzi unakuwepo Uwanja wa Taifa  wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Kamishina Suleiman Kova alisema  mchezo wa leo utakuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki wa Tanzania na wale wa nchi za Afrika Mashariki tutokana na hali hiyo jeshi la Polisi limejipanga kupambana na hali yoyote ya uvunjifu wa amani itakayo jitokeza katika mchezo huo.

"Tunaomba wananchi wasiwe na shaka yeyote ya kiusalama na pia watupe ushirikiano wa kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi kwa jambo lolote wanaloisi linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa ndani ya uwanja au nje."alisema Kova.


Aliongeza kuwa katika kuakikisha watu wanaingia wakiwa salama tutafanya upekuzi katika milango yote ya kuingilia kwa kutumia mashine za kisasa  na pia kutakuwa na ulinzi mkali katika majukwaa yote kuakikisha usalama unakuwepo kwa kupindi chote.

"Tunawasihi mashabiki wote wasije na vitu vyovyote ambavyo vinaweza kutumika kama silaha mfano soda za chupa,vipande vya chuma,visu,mawe au silaha za moto kwani awataweza kupita nazo getini kutokana na ulinzi mkali,na mashabiki watakao kiuka agizo hili hatua kali zitachukuliwa na kufunguliwa mashtaka."alisema Kova.

Aidha Kamanda aliongeza kuwa barabara ya Uwanja wa Taifa itafungwa kwa muda ili kupunguza foleni zisizokuwa za lazima, pia hakuna magari yatakayoruhusiwa kuegeshwa katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment