Shauri hilo jana lililetwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Aloyce Katemana, kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali ambapo baada ya kusomewa maelezo hayo na upande wa mashtaka, Mhindi alikiri kutenda kosa na mahakama kumpa adhabu hiyo au kifungo cha miezi sita gerezani.
Hakimu Katemana aliieleza Mahakama hiyo kuwa baada ya mshtakiwa kukiri maelezo yote ya kosa,inamtia hatiani na kumsomea hukumu pamoja na adhabu.
Akisoma hukumu hiyo,alisema amezingatia maelezo ya upande wa mashtaka na maelezo ya mshtakiwa alipokuwa akiililia mahakama na hivyo kumpa adhabu ya kulipa faini ya Sh.1000 au kwenda gerezani miezi sita.
Hata hivyo hakimu alipomuuliza mshtakiwa huyo kama ana kiasi hicho cha fedha,alijibu kuwa hana ambapo mwandishi wa habari wa Radio Times FM Chipangula Nandule alijitolea kumlipia faini hiyo.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,Muhindi alidai mahakama ni hapo kuwa alikuja nchini kufanya biashara ya nguo aliyounganishwa na kijana mmoja wa Mjini Arusha ambapo akiwa huko,Juni 27,2012 alitekwa na mtu asiyemjua.
Alisema kuwa mtu huyo alikuwa na siraha na alimpeleka asipo pajua na kumuamrisha kwenda kanisani la Ufufufo na Uzima la Mchungaji Gwajima lililopo Kawe ili akasema kile alichomueleza ambacho ni kuhusu kumteka Dkt Ulimboka .
Alidai kuwa ilimlazimu akubali kusema hivyo kutokana na kuogopa vitisho na baada ya hapo alipelekwa kituo cha Polisi Ostarbey na kusisitizwa kusema kama alivyosema kanisani huku akiahidiwa kupelekwa kwao Kenya na kubadilishiwa maisha yake.
Huku akibugujikwa na machozi,alidai kuwa "Nikiwa polisi Centre ,polisi wakubwa aliniambia niseme vilevile nilivyoambiwa niseme na walinirekodi,nilishangaa kuletwa mahakamani nikidaiwa kutaka kumuua Dkt Ulimboka"
"Sipingani na upande wa mashtaka ,nilivyoletwa nilizani nimeonewa ,nimejifunza kuwa mahakama ni kitu tofauti sana,siilaumu serikali,polisi wala upande wa mashtaka maana hata nisingekubaliana na walioniteka mimi sio bora zaidi ya watu wengine"aliongeza.
Alidai kuwa tukio la kutekwa kwa Dkt Ulimboka lilileta shida nchini,lakini taarifa alitoa kwa hiyari yake kutokana na vitisho na kuokoa maisha yake.
"Mheshimiwa nimekosa mbele ya mungu na mahakama ya Tanzania,ningeomba kwa ubinadamu na upendo pia,nimekaa jera muda mrefu,naomba nipewe adhabu iwe fundisho kwa wengine lakini nipunguziwe adhabu"alidai.
Muhindi alidai yeye ni kijana wa miaka 23,mama yake ni mjane yupo mwenyewe nyumbani kwao hivyo hakimu akiwa kama mazazi amuonee huruma kwani hajui kitakachofanyika kesho.
Awali akisomewa maelezo hayo ya awali na wakili wa serikali Tumaini Kweka alidai kuwa mshtakiwa huyo alikuja nchini akipitia mpaka wa Namanga,Arusha hadi Dar es Salaam na kwenda katika Kanisa hilo.
Alidai kuwa alipofika kanisani hapo mshtakiwa huyo alionana na mchungaji Joseph Kiriba na kumueleza kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliomteka na kumtesa Dkt Ulimboka na kisha kumtupa Mabwepande na taarifa kufika polisi.
Ilidaiwa kuwa,baadaye mshtakiwa huyo alipelekwa kwa mlinzi wa amani ambapo alikanusha taarifa za kumteka Dkta ulimboka.
Alidai kuwa baada ya polisi kufanyia uchunguzi taarifa hizo,ilibaini kuwa kweli hakuhusika na hivyo kumbadilishia mashtaka kutoka shtaka la kumteka na kumjeruhi Dkt Ulimboka hadi shtaka la kutoa taarifa za uongo kwa polisi na kushtakiwa upya.
No comments:
Post a Comment