Tuesday, October 1, 2013

MTOTO WA MIAKA MIWILI AJIFUNGUA

MTOTO wa miaka miwili wa nchini China, amejifungua baada ya madktari kugundua kuwa anamimba isiyokuwa.

Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Xiao Feng alijifungua kwa njia ya upasuaji mara baada ya madkati hao kugundua kuwa anaujauzito huo usiokuwa.

Xiao alipelekwa hospitali mara baada ya tumbo lake kuwa kubwa hali ambayo ilimsababishia matatizo ya upumuaji ndipo madktari walipoamua kumfanyia uchunguzi.


Baada ya jopo la madktari hao kumfanyia uchunguzi ambapo walilazimika kuchukua picha za X- Ray na MRI ndipo walipogundua kuwa mtoto huyo alibeba mimba isiyokuwa na kuamua kumfanyia  upasuaji.

Madkati hao walifanikiwa kuondoa mimba hiyo iliyokuwa na upana wa centiminta 20, iliyokuwa imeanza kukuwa kwa kuonesha vidole vya miguu na mikono.

Madkati hao ambao walidai kuwa mimba hiyo ilitakiwa kuwa pacha wa mtoto huyo, ambapo ilidaiwa kuwa angekuwa ni mtoto wa kiume.

Inasemekana kuwa mapacha hao wanaofanana hutokea pale yai linapojigawa wakati wa urutubishaji na mapacha walioungana hutokea pale yai linaposhindwa kujigawa.







No comments:

Post a Comment