Wednesday, October 16, 2013

WAZEE YANGA YAJITAMBA KUINGO'A SIMBA

WAZEE wa Club ya Yanga wametamba kuwafunga watani wao wa jadi Simba katika mechi yao ya kesho kutwa inayotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo wamedai kuwa mnyama lazima afe.

Akizungumza kwa niaba ya wazee hao na Waandishi wa Habari Dar es Salaam Katibu wa Baraza la Wazee Ibrahim Akilimali alidai kuwa  timu hiyo ndiyo inaanza kucheza mchezo wao wa ligi rasmi huku wakijitapa kumuua mnyama kutokana na maandalizi yao ambapo kikosi cha Yanga kitapanda dimbani huku kukiwa hakuna majeruhi.


Alisema kuwa maandalizi yao yamekamilika huku viongozi wa matawi, baraza la wazee  kuhakikisha ushindi huku kambi ya visiwani Pemba kuendelea vizuri.

"Sisi hatusuwisui  Yanga ndio inaanza ligi na kama tunaanza tunaahadi, sisi tulifungwa goli 5,  na nikatangaza kuwa hatulipi goli 5 kwa mfululizo kama tulivyofungwa, ila tutalipa goli 5 mara 5 kumfunga Simba" alitamba Akilimali.

Wachezaji hao ambao kwa sasa wapo kambini huko Visiwa vya Pemba, Akilimali aliweka wazi kuwa kikosi hicho kimekamilisha maandalizi yao na watapanda dimbani huku kukiwa hakuna majeruhi hata mchezaji mmoja.

Na kwa upande wake Katibu wa Vijana Bakiri Makele, alitoa wito kwa waamuzi watakao chezesha mchezo huo kufuata sheria 17 za mpira ili kuondoa migogoro isiyokuwa na tija.

Huku akiwataka mashabiki pamoja na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi huku wakionesha nidhamu pamoja na kukubaliana na matokeo ya aina yote kwani mwaamuzi wa mpira huo ni dakika 90.

Timu za Simba na Yanga teyari zimeshacheza michezo nane huku wakiwa wametofautiana kwa pointi tatu ambapo Simba ndio inaongoza ligi kwa pointi 18, huku Yanga wakishika nafasi ya nne kwa point 15.






1 comment:

  1. Dear Users.
    I need some help from u. i want to broadcast online channel from my own PC. can any one
    provide me any information about this.

    thanks and waiting for reply.

    smartcric.com >>>
    Fottball.com live >>>
    khantv.com cricket>>
    ptv sports Live>>>

    ReplyDelete