Tuesday, July 30, 2013

PINDA KORTINI ALHAMISI


KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetangaza kumburuta Mahakamani siku ya Alhamisi asubuhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa kile kinachodaiwa amekaidi kufuta kauli yake ya kuruhusu vyombo vya usalama kupiga wananchi wanaokaidi amri za vyombo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi na mwanasheria wa LHRC , Harold Sungusia, alisema wanamfungulia shtaka Waziri Mkuu Pinda, kesi ya kimkakati inayomlazimu ajibu mbele ya mahakama msimamo wa serikali unaomsababisha atoe kauli hiyo.

KESI YA JAYDEE YASOGEZWA MBELE

Mwanamuziki Judith Wambura akiongozana na msanii mwenzie Professa Jay wakitoka Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kusikiliza kesi inayomkabili iliyofunguriwa na mkurugenzi mtafiti na maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kukashfu uongozi huo, kesi hiyo imepigwa kalenda hadi Agosti 2 mwaka huu

Monday, July 29, 2013

Sakata dawa za kulevya: Mbunge CCM ajisalimisha Polisi, ataka achunguzwe


MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Idi Azzan, amejilisalimisha' polisi na kutaka jeshi hilo, kufanyia uchunguzi tuhuma za kuhusishwa na biashara za dawa za kulevya na iwapo itabainika anahusika, hatua za kisheria zichukue mkondo wake.

Mbunge huyo alifikia hatua hiyo jijini Dar es Salaam jana baada ya barua zilizoandikwa na watu wanaodai ni wafungwa wa Tanzania wanaotukia adhabu zao mjini Hong Khong, nchini China, kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimhusisha yeye (Azzan) kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo akiwatumia vijana hao. Wafungwa hao wanadaiwa kuwa wanatumikia adhabu zao baada ya kupatikana na makosa ya dawa za kulevya.

Mbunge huyo alisema alienda kutoa taarifa hizo mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaa.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainika na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azza, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana.

Azzan alibainisha kuwa ameamua kwenda kutoa taarifa polisi ili waanze uchunguzi wao. Alisema barua hizo ambazo hazina anuani ya eneo zilipotoka wala majina ya waandishi wake zina lengo baya dhidi yake na kutaka kuposha umma.

"Mimi sipo juu ya sheria itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza;

"Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao."

Mwishoni wiki hii katika mitandao mbalimbali ya kijamii ziliwekwa barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa waliokamatwa na dawa za kulevya nchini China zikimhusisha mbunge huyo na biashara hiyo.

Barua hizo pia zinawataja baadhi ya viongozi wa serikalini kuwa wanajihusisha na mtandao wadawa za kulevya, lakini hazikuainisha majina yao.


Ajali ya basi yawaua 38 nchini Italy



Waokoaji kusini mwa Italy wamesema kuwa takriban watu 38 wameuawa baada ya basi moja waliokuwa wakisafria kutumbukia mita thelathini ndani ya mtaro.

Abiria wengine walipelekwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya.






Basi hilo lilikuwa limebeba abiria waliokuwa wakirudi mjini Napoli kutoka jimbo la kusini la Campania.

Hatahivyo haijabainika kiini cha ajali hiyo iliohusisha magari kadhaa.

Basi hilo liligonga magari kadhaa kabla ya kuanguka ndani ya mtaro mjini Avellino.

Takriban watu 10 wamejeruhiwa baadhi wakipata majeraha mabaya sana, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Italia.

Basi hilo liliwa limewababa abiria hamsini ikiwemo watoto waliokuwa wanarejea Naples baada ya kufanya hija.

Picha zilionyesha miili ya watu iliyokuwa imetapakaa kando ya barabara pamoja na magari yaliyokuwa yameharibiwa kwenye ajali hiyo.

Dereva wa basi hilo ni miongoni mwa wale waliofariki.

Waathiriwa kadhaa hata hivyo hawakuweza kutambulika , kwa mujibu wa msemaji wa polisi akisema kuwa wangali wanatoa miili katika magari yaliyoharibiwa.

Tuesday, July 23, 2013

WIZI WATIKISA BENKI AFRIKA

Utafiti umegundua kuwa benki zilizopo kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki zinapoteza wastani wa sh. bilioni 80 kila mwaka kutokana na wizi wa mitandao.

Utafiti uliofanywa na kampuni ya Deloitte mwaka 2012 unaonyesha kuwa benki za kibiashara kwenye nchi za Afika Mashariki zinapoteza takriban zaid ya sh 80 bilioni

Hayo yalibainishwa na Rais wa Taasisi huru ya kimataifa isiyokuwa ya kiserikali inayohusika na kusimamia na kutoa mafunzo na maarifa ya mifumo ya mitandao (ISACA), Boniface Kanemba wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kanemba  alisema kuwa wizi wa mtandao umekuwa ukifanyika sana katika benki na taasisi mbalimbali zisizokuwa za serikali ambapo kiasi hicho cha fedha huwa zinaibiwa kila mwaka.

LWAKATARE KUTIBIWA NJE


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imempa kibali Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, akatibiwe nje ya nchi.
Lwakatare ambaye anasumbuliwa na maumivu ya shingo, kwa sasa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa uangalizi maalumu na kufanya mazoezi, alipata kibali hicho kwa kuwa anakabiliwa na kesi ya kula njama za kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
Wakili wake, Nyaronyo Kicheere alililiambia gazeti hili nje ya mahakama kuwa Lwakatare anatarajiwa kupelekwa India, lakini akasema tarehe ya kusafirishwa inategemea na kukamilika kwa taratibu za hospitali alikolazwa, na kule anakopelekwa.
Mahakama hiyo ilitoa kibali ili akatibiwe nje ya nchi, baada ya Kicheere, kuiomba mahakama hiyo impe kibali ili akatibiwe nje kama ilivyopendekezwa na madaktari wake.

WALIOUWAWA DARFUR JK ATOA TAMKO


Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya kutoa heshima zake kwa wapiganaji saba wa Tanzania waliokuwa Darfur, Sudan katika operesheni ya kulinda amani ya UN na Afrika (Unamid) ambao waliuawa na kundi linalodaiwa la wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na Serikali ya Sudan inayoongozwa na Rais Omar al-Bashir.
Wapiganaji waliouawa ni Oswald Chaula kutoka 42KJ Chabruma, Songea, Peter Werema (44KJ Mbeya), Fortunatus Msofe (36KJ Msangani, Pwani), Rodney Ndunguru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ- Upanga).

FAMILIA YA KIFALME UINGEREZA YAPATA MTOTO WA KIUME


Ujumbe wa heri njema umeendelea kutolewa  kote duniani baada ya Kate na Prince William ambaye atakuwa wa tatu kwenye foleni katika kurithi ufalme wa Uingereza.Mwanamfalme William na mkewe Kate ,wameamkia hospitalini asubuhi ya leo mjini London baada ya kupata mtoto wao wa kwanzaJumatatu jioni.

Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na takriban kilo tatu na nusu atafahamika kama mwanamfalme wa Cambridge, lakini hajapewa jina.

Katika taarifa fupi William,amesema wana furaha isiyo na kifani.Baadaye leo jeshi la Uingereza linatarajiwa kutoa heshima kwa kuzaliwa mwanamfalme huyo kwa kurusha mizinga 40 hewani huko London na kengele la kanisa la Westminster Abbey zitalia.

Thursday, July 18, 2013

MSWAADA WA SHERIA KENYA KUWANUFAISHA WANAWAKE


Mswaada unaolenga kuoanisha sheria za ndoa nchini Kenya umewasilishwa bungeni.Baadhi ya mabadiliko yaliopendekezwa katika mswada huo ni pamoja na kuhalalisha ndoa za wake wengi mbali na kuziimarisha sheria zote saba za ndoa.

Mapendekezo mengine ambayo huenda yakazua hisia kali ni yale ya kugawa mali iliochumwa katika ndoa pamoja na adhabu ya wanaume ambao huvunja ahadi zao za kuwaoa akina dada.

Licha ya kuwa ndoa za WAKE wengi hutekelezwa na jamii nyingi nchini kenya, bado hazijahalalishwa.lakini katika mswada huu mpya ,ndoa hizo zimependekezwa.Hatahivyo mwanamume ambaye angependa kuingia katika ndoa hizi ni sharti aweke wazi majina yote ya wake zake mbele ya msajili wa ndoa pamoja na rukhsa aliyopata kutoka kwa wake hao.Hatahivyo akina dada wana kibarua cha kuthibitisha mahakamani iwapo ahadi hiyo ilitolewa na kuvunjwa.

MANDELA ATIMIZA MIAKA 95


LEO ni kumbukumbu ya kuzaliwa Mzee Nelson Rolihlahla Mandela, ambapo anatimiza miaka 95 toka azaliwe, sherehe ya kuzaliwa kwa rais huyo zinafanyika leo hafla  itakayoambatana na shughuli za kusaidia wasiojiweza ndani ya jamii na ulimwenguni kote.

Mandela leo anatimiza miaka 95 ingawa bado yupo mahututi katika hospitali mjini Pretoria, Afrika Kusini akisumbuliwa na matatizo ya kupumua.Shilika la Umoja wa Mataifa mwaka 2010 lilitangaza siku ya kuzaliwa kwake Mandela kwa kuadhimisha kila mwaka kama njia ya kuwahimiza watu kote ulimwenguni kufanya angalau saa moja ya mambo ya kutenda mema.

Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918. Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa
kidemokrasia nchini Afrika Kusini.

SISTA ASHAMBULIWA


Sista aliye mafunzoni ametekwa na kubakwa kwa wiki nzima na kundi la wanaume watatu katika kile kinachohisiwa kuwa ni shambulio la kulipiza kisasi, vyombo vya habari nchini India vimeripoti.

Sista huyo mwenye miaka 22 alidaiwa kutekwa kwenye stesheni ya treni na binamu zake na kisha kushikiliwa mateka na kubakwa kwa zaidi ya siku kadhaa sababu waliishutumu familia yake kwa kifo cha baba yao.

Ni tukio la karibu kabisa katika mfululizo wa mashambulio ya ubakaji nchini India mwaka huu tangu mwanafunzi alipobakwa na kundi la wanaume na kufa kutokana na majeraha yake ya kutisha ndani ya basi la Delhi Desemba mwaka jana.Sista huyo aliwaeleza polisi alikuwa akutane na binamu zake kwenye stesheni ya treni karibu na Chennai, huko Tamil Nadu, kusini mwa India, baada ya kudai kwamba mama yao alikuwa anaumwa.

Wednesday, July 17, 2013

BAADHI YA MADEREVA WA MALORI WANACHANGIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Imeelezwa kuwa uchukuzi wa bidhaa kutumia malori kunachangia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini.

Kauli hiyo imetolewa na katibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kupambana na matumizi mabaya ya mali za umma, Andekisye Mwakabalula.

Alisema mara kadhaa madereva hao wamekuwa wakitoa kisingizio cha kuharibikiwa magari kwa waajiri wao waweze kupata muda wa kufanya ngono

Alisema baadhi ya madereva wa malori wamekuwa na familia kubwa katika maeneo mbalimbali wanayoweka kambi hali inayowaweka hatarini kupata maambukizi ya UKIMWI.

Alisema licha ya kuwa na kisingizio cha ugumu wa maisha lakini wanawake hao wamekuwa wakiwakubalia kwa urahisi madereva hao wazae nao wakiamini wana uwezo mkubwa wa fedha

ANYIMWA DHAMANA KWA KOSA LA KUMBAKA MKEWE

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Entebbe nchini Uganda imemnyima dhamana Charles Atayo(33) anayetuhumiwa kumbaka mke wake.

Atayo mkazi wa kijiji cha Nakigalala kilichoko mkoa wa Sisa, wilaya ya Wakiso aliamriwa kurudi katika gereza la kigo baada ya kukataliwa dhamana yake.

Mtuhumiwa huyu anadaiwa kumlazimisha mkewe ambaye hakutajwa jina kufanya naye mapenzi kwa lazima jambo lililotafsiriwa sawa na ubakaji

Katika utetezi wake Atayo alikanusha kumbaka mkewe kwa kuwa walifunga ndoa halali tangu mwka 2000 na kuzaa naye watoto watatu.

Katiba ya Uganda inasema kuwa mtu yeyote yule atakayemlazimisha mwingine kufanya naye mapenzi bila ridhaa yake ni sawa na ubakaji

HALI MBAYA ASKARI MWINGINE JWTZ

Askari mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kati ya 14 waliojeruhuwa katika shambulio la waasi hivi karibuni mjini Darfur, Sudan imezidi kuwa mbaya hivyo kulazimika kukimbizwa Khartoum kwa ajili ya matibabu zaidi.

Msemaji wa JWTZ , Kanali Kapambe Mgawe aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake, alisema askari hao wako Darfur nchini Sudan huku 4 wakiwa chini ya uangalizi maalumu na 9 kupata nafuu huku wakingoja kukamilika kwa Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa (UN) ili taeatibu za kuwaleta nyumbani zifanyike.

Kanali Mgawe alisema wanawasiliana na UN mara kwa mara na kuwa miili hiyo itatua nchini kwa kipindi cha hivi karibuni mara baada ya kukamilika kwa taratibu za Umoja wa Mataifa.

Monday, July 15, 2013

KUNDI LA 'TNG' LAJA KIVINGINE, WAMSHIRIKISHA ROSE NDAUKA KWENYE 'SINGLE' YAO MPYA


HATIMAYE msanii wa filamu nchini Rose Ndauka ameamua kuugeukia muziki wa kizazi kipya kwa kuingiza sauti kwenye nyimbo aliyoshirikishwa inayojulikana kwa jina la 'Crazy Man'.

Rose ameshirikishwa 'single' hiyo na kundi linalojulikana kwa jina la TNG, baada prodyuza wa muziki huo  Paul Matthysse  'P- Funk Majani', kubaini kipaji chake hicho kwenye upande wa kuimba.

Kundi hilo limeundwa na wasanii wawili akiwemo Agustino John 'Latino Man' pamoja na Maliki Bandawe ambaye anamahusiano ya kimapenzi na Rose Ndauka.

JUSTINE BIEBER AMUOMBA MSAMAHA BILL CLINTON MSAMAHA


Baada ya muimbaji nyota wa muziki wa Pop Justine Bieber kuripotiwa kukojoa katika ndoa kwenye mgahawa, muimbaji huyo ameamua kuomba msamaha kwa kitendo hicho alichokifanya

Muimbaji huyo, amempigia simu rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton kumuomba radhi kutokana na kumkashifu baada ya kuonekana katika video akijisaidia kwenye ndoo huku akimkashfu rais huyo.

Bieber alimpigia simu rais huyo kumuomba radhi kwa kumkashifu pamoja na kupulizia rangi picha za rais huyo katika jiko la mgahawa mmoja katika jiji la New York City mapema mwaka huu

PIGO TANZANIA, WANAJESHI 7 WAUWAA NA 14 KUJERUHIWA


Wanajeshi 7 kati ya 36 wameuwa Darfur, mauaji wa wanajeshi 7 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliokuwa wanalinda amani Darfur, Sudan wauwaa baada ya kushambuliwa na waasi wa Sudani.

Mbali na vifo hivyo askari wengine 14 wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la kushtukiza lililofanyika na kundi la waasi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, msemaji wa jeshi hilo Kanali Kapambala Mgawe, alisema wanajeshi hao walivamiwa wakati wakiwa kwenye msafara wa kuwasindikiza waangalizi wa amani ambao walikuwa wanatoka eneo la Khor Abeche kwenda Nyara Darfur.

Saturday, July 13, 2013

ABIRIA WA BODA BODA MJINI


Nyani amezoeleka kuonwa kwenye misitu lakini hii ni jambo la kushangaza kwa wapita njia baada ya dereva wa bodaboda kumpakiza nyani kama abiri 

ZAIDI YA WATANZANIA 250 WAKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA NJE YA NCHI


KAMISHINA wa tume ya kuratibu na kuthibiti madawa ya kulevya Christopher Shekiondo amebainisha kwamba watanzania wengi wanaokamatwa na dawa za kulevya nchi za nje adhabu zao mara nyingi zinakuwa kunyongwa au kifungo cha maisha jela.

Akizungumza kwa simu jana Kamishina huyo alisema, kwa kipindi cha muda wa mwaka mmoja anakumbuka zaidi ya watanzania zaidi ya 250 wamekamatwa katika nchi mbalimbali na dawa za kulevya.

Friday, July 12, 2013

MAANDAMANO ZAIDI KUFANYIKA MISRI LEO


Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi wanajiandaa kwa maandamano makubwa mjini Cairo, huku waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimisha Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadan.

Wafuasi wa Bwana Morsi wanatarajia kuwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo, wataendelea kuunga mkono wito wao wa kutaka Bwana Morsi kurejeshwa madarakani.

Wapinzani wa rais huyo wa zamani ambao waliandamana hadi rais huyo akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika katika medani ya Tahrir.

Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa.

Mwandishi wa BBC mjini Cairo, Jim Muir anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood huenda liliwatenga raia wengi wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi wa nchi hiyo hawataki jeshi kuingilia masuala ya siasa.Marekani kutuma ndege za kivita Misri

Siku ya Alhamisi serikali ya Marekani, ilitoa wito kwa utawala mpya wa Misri, kusitisha harakati zake za kuwakamata wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood na kuonya dhidi ya kulenga kundi lolote.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon vile vile ameonya utawala huo wa Misri kutotenga chama chochote cha kisiasa katika harakati za kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa hilo.

Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney amesema, utawala wa Washington hauamini kuwa ni lazima isitishe misaada yake ya Misri.

Marekani inatarajiwa kupeleka ndege nne za kivita aina ya F-16 nchini Misri, lakini haijathibitisha kuwa msaada huo utatolewa lini.

Serikali ya Marekani imesema, inachunguza ikiwa aumuzi huo wa jeshi la Misri kumuondoa madarakani rais Morsi ni mapinduzi ya Kijeshi kwa kuwa sheria za Marekani inazuia serikali kutoa misaada kwa nchi yoyote ambayo kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ataondolewa kupitia mapinduzi.

Wafuasi wa rais Morsi wamekuwa wakiandamana wiki nzima karibu na kambi ya kijeshi iliyoko Mashariki mwa mji mkuu wa Cairo, ambako wanaamini kuwa kiongozi wao anazuiliwa na maafisa wa kijeshi tangu alipoondolewa madarakani.

YALIYOJILI SIKU YA MATUMAINI

 Muimbaji Flora Mbasha akitumbuiza uwanja wa taifa siku ya Matumaini
 Kipa wa timu ya Simba mbunge Iddz Azzan akiingia uwanjani
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Bongo Movi akiwemo Ray wakijiandaa kuingia uwanjani

YALIYOJILI MECHI YA TAMASHA LA MATUMAINI

 Baadhi ya wabunge wa timu ya Yanga wakifanya mazoezi kabla ya mechi iliyochezwa hivi karibuni uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Tamasha la Matumaini
 Baadhi ya timu ya wabunge wa Simba na Yanga wakiingia uwanjani hapo kwa ajili ya mechi hiyo ambapo timu ya Yanga iliweza kuchukua kombe la ushindi kwa goli la penati