Monday, July 29, 2013

Ajali ya basi yawaua 38 nchini ItalyWaokoaji kusini mwa Italy wamesema kuwa takriban watu 38 wameuawa baada ya basi moja waliokuwa wakisafria kutumbukia mita thelathini ndani ya mtaro.

Abiria wengine walipelekwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya.


Basi hilo lilikuwa limebeba abiria waliokuwa wakirudi mjini Napoli kutoka jimbo la kusini la Campania.

Hatahivyo haijabainika kiini cha ajali hiyo iliohusisha magari kadhaa.

Basi hilo liligonga magari kadhaa kabla ya kuanguka ndani ya mtaro mjini Avellino.

Takriban watu 10 wamejeruhiwa baadhi wakipata majeraha mabaya sana, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Italia.

Basi hilo liliwa limewababa abiria hamsini ikiwemo watoto waliokuwa wanarejea Naples baada ya kufanya hija.

Picha zilionyesha miili ya watu iliyokuwa imetapakaa kando ya barabara pamoja na magari yaliyokuwa yameharibiwa kwenye ajali hiyo.

Dereva wa basi hilo ni miongoni mwa wale waliofariki.

Waathiriwa kadhaa hata hivyo hawakuweza kutambulika , kwa mujibu wa msemaji wa polisi akisema kuwa wangali wanatoa miili katika magari yaliyoharibiwa.

No comments:

Post a Comment