Monday, July 29, 2013

Sakata dawa za kulevya: Mbunge CCM ajisalimisha Polisi, ataka achunguzwe


MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Idi Azzan, amejilisalimisha' polisi na kutaka jeshi hilo, kufanyia uchunguzi tuhuma za kuhusishwa na biashara za dawa za kulevya na iwapo itabainika anahusika, hatua za kisheria zichukue mkondo wake.

Mbunge huyo alifikia hatua hiyo jijini Dar es Salaam jana baada ya barua zilizoandikwa na watu wanaodai ni wafungwa wa Tanzania wanaotukia adhabu zao mjini Hong Khong, nchini China, kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimhusisha yeye (Azzan) kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo akiwatumia vijana hao. Wafungwa hao wanadaiwa kuwa wanatumikia adhabu zao baada ya kupatikana na makosa ya dawa za kulevya.

Mbunge huyo alisema alienda kutoa taarifa hizo mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaa.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainika na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azza, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana.

Azzan alibainisha kuwa ameamua kwenda kutoa taarifa polisi ili waanze uchunguzi wao. Alisema barua hizo ambazo hazina anuani ya eneo zilipotoka wala majina ya waandishi wake zina lengo baya dhidi yake na kutaka kuposha umma.

"Mimi sipo juu ya sheria itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza;

"Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao."

Mwishoni wiki hii katika mitandao mbalimbali ya kijamii ziliwekwa barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa waliokamatwa na dawa za kulevya nchini China zikimhusisha mbunge huyo na biashara hiyo.

Barua hizo pia zinawataja baadhi ya viongozi wa serikalini kuwa wanajihusisha na mtandao wadawa za kulevya, lakini hazikuainisha majina yao.


No comments:

Post a Comment