Monday, July 15, 2013

KUNDI LA 'TNG' LAJA KIVINGINE, WAMSHIRIKISHA ROSE NDAUKA KWENYE 'SINGLE' YAO MPYA


HATIMAYE msanii wa filamu nchini Rose Ndauka ameamua kuugeukia muziki wa kizazi kipya kwa kuingiza sauti kwenye nyimbo aliyoshirikishwa inayojulikana kwa jina la 'Crazy Man'.

Rose ameshirikishwa 'single' hiyo na kundi linalojulikana kwa jina la TNG, baada prodyuza wa muziki huo  Paul Matthysse  'P- Funk Majani', kubaini kipaji chake hicho kwenye upande wa kuimba.

Kundi hilo limeundwa na wasanii wawili akiwemo Agustino John 'Latino Man' pamoja na Maliki Bandawe ambaye anamahusiano ya kimapenzi na Rose Ndauka.


Akizungumza jijini Dar es Salaam mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Maliki aliweka wazi kuwa prodyuza wa nyimbo hiyo ndiye alibaini kipaji cha Rose ambapo aliweza kuingiza sauti huku akiinogesha single hiyo.

Kwa upande wake Rose Ndauka aliweka wazi kuwa chanzo cha yeye kujikuta akishirikishwa kwenye nyimbo hiyo ni wivu wa kimapenzi aliokuwa nao, hali inayomfanya kuwa na mpenzi wake kila mahali.

"Wivu wangu huo ndio uliosababisha nijikute naingiza sauti yangu kwenye nyimbo hiyo, kwani napenda kuongozana na mpenzi wangu kila mahali na ndipo nilijikuta nipo studio 'Bongo record', bila ya kutarajia kumbe P Funk aligundua kipaji changu na kunishawishi kuingiza sauti kwenye nyimbo hiyo, " alisema Ndauka.

No comments:

Post a Comment