LEO ni kumbukumbu ya kuzaliwa Mzee Nelson Rolihlahla Mandela, ambapo anatimiza miaka 95 toka azaliwe, sherehe ya kuzaliwa kwa rais huyo zinafanyika leo hafla itakayoambatana na shughuli za kusaidia wasiojiweza ndani ya jamii na ulimwenguni kote.
Mandela leo anatimiza miaka 95 ingawa bado yupo mahututi katika hospitali mjini Pretoria, Afrika Kusini akisumbuliwa na matatizo ya kupumua.Shilika la Umoja wa Mataifa mwaka 2010 lilitangaza siku ya kuzaliwa kwake Mandela kwa kuadhimisha kila mwaka kama njia ya kuwahimiza watu kote ulimwenguni kufanya angalau saa moja ya mambo ya kutenda mema.
Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918. Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa
kidemokrasia nchini Afrika Kusini.
HISTORIA YA NELSON MANDELA
Jina la Nelson alipewa na mwalimu wake alipojiunga na shule ya wamisionari, awali alijulikana kwa jina la
Rolihlahla Mandela aliishi na baba yake kwa muda mfupi tu kwani mzazi wake huyo alifariki dunia mwaka 1930 na kuanzia hapo alilelewa na mpwa wa baba yake, David Dalindyebo ambaye pia alikaimu uongozi wa katika jamii ya Wathembu.
Alikuwa mcheza masumbi, ikiripotiwa kwenye baadhi ya mitandao inaonyesha kuwa Mandela aliwahi kuwa mwanamasumbi wakati akiwa chuo.Mwaka 1944, Mandela alibahatika kupata mke aliyejulikana kwa jina la Evelyn ambaye alijaliwa kupata mtoto wa kiume mwaka 1945 na kumwita Madiba Thembekile (Thembi kwa kifupi). Hata hivyo, mtoto huyo alifariki katika ajali ya gari mwaka 1969 wakati Mandela akiwa jela.
Mandela na Evelyn walijaliwa kupata watoto wengine watatu; Makaziwe mkubwa ambaye hata hivyo, alifariki dunia akiwa mchanga 1948, Makgatho Mandela aliyezaliwa 1950 na kufariki 2005 na Makaziwe mdogo mwaka 1953 ambaye kwa jumla ndiye anayesimamia shughuli na mali katika familia hivi sasa.
Mbali na mwanamke huyo Mandela ameoa mara tatu , ambapo alipotimiza miaka 80 ndipo alipooa mwanamke huyo wa tatu anafahamika kwa jina la Graca, moja ya sherehe aliyoifanya kwa kipindi hicho cha kutimiza miaka hiyo 80 ilikuwa ni kumuoa mwanamke huyo.
Desemba 1956 alikuwa mmoja wa washtakiwa wa kesi ya uhaini na wakati kesi hiyo ikiendelea alioana na
Nomzamo Winifred Madikizela mwaka 1958. Alibahatika kupata naye watoto wawili wa kike.
Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya ubaguzi wa rangi Apartheid Afrika Kusini. Mandela alitumikia kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi, Alifungwa katika kisiwa cha Robben.
Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano.Mnamo mwaka wa 1993, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
Mandela ni moja wa vijana walioanzisha madai ya uhuru kwa njia ya mapigano alikuwa na imani kuu juu ya haki sawa kwa watu wote, aliamini na anaamini kuwa binadamu wote ni sawa katika misingi ya ubinadamu, kwa haki na mahitaji.
Ni kwa imani na msukumo huo wa kudai uhuru na haki za watu wote wa Afrika Kusini, alikuwa tayari kudai haki hizo kama ingemlazimu kuyatoa maisha yake, kwa hakika imani juu ya haki sawa kwa watu wote ni funzo na changamoto kubwa kwa viongozi wote duniani.
Baada ya kuachiwa huru mwaka 1990 alirejea kwenye harakati za kudai haki za waafrika kusini walio wengi. Mwaka 1991 alichaguliwa rais wa 'African National Congress' ANC Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Afrika Kusini ya kidemokrasia mwaka 1994, alitumia muhula mmoja tu wa miaka mitano na mwaka 1999 kuacha mamlaka ya dola kuu kabisa kiuchumi bara Afrika.
No comments:
Post a Comment