Monday, August 5, 2013

AUWAWA BAADA YA KUMNYONGA MKE WAKE

Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Kisangwa kata ya Mcharo wilaya ya Bunda mkoa wa Mara, Batule Masanja anadaiwa kumuua mkewa wake kwa kumnyonga shingo kwa kutumia mikono yake kisha na yeye kuuwawa na wananchi wenye hasira kali.

Tukio hilo lilithibitishwa na polisi wilayani hapo, lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Kisangwa kata ya Mcharo kwenye sherehe ya ufunguzi wa nyumba ya ndugu yao.


Afisa mtendaji wa kata hiyo  Waziri Kingi alimtaja mwanamke aliyeuwawa kwa kunyongwa na mumewe kuwa ni Paulina Samson Misinzo.

Kingi alisema Masanja naye aliuwawa baada ya kukamatwa na wananchi hao wenye hasira kali mlimani alikokimbilia kujificha.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo Masanja aliyekuwa ametengana na mkewe kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia, alimfuata mke wake huyo kwenye sherehe hiyo usiku.

Inadaiwa kuwa baada ya kufika nyumbani hapo huku akiwa na watoto wao wawili alimuita mkewe huyo aliyekuwa akicheza muziki na kumpeleka nyuma ya nyumba ambako inadaiwa alimuua kwa kumnyonga kwa kutumia mikono yake hadi kufa.

Inaendelea kudaiwa kuwa baada ya kitendo hiko  alibeba  mwili wa mkewe huyo na kuutupa pembezoni mwa nyumba ya jirani.

Mashuhuda walidai kuwa baadaye Masanja alikimbilia mlimani na kukamatwa siku iliyofuatwa asubuhi na wananchi hao waliokusanyana kwa kupiga yowe.

Wanadai mashuhuda hao kuwa wananchi hao walimkamatwa Masanja baada ya kumsaka na kumshambulia kwa kipigo hadi kufa.

No comments:

Post a Comment