Tuesday, August 27, 2013

WAKAZI WA MIVINJENI WASHINIKIZA MALIPO YAO

 WAKAZI wa Mivinjeni Kurasini wanaotakiwa kuhama kupisha mradi wa  uwekezaji wa EPZ wamefunga barabara kuishinikiza Serikali kuwalipa hundi zao na si viwanja. Hali hiyo ilijitokeza leo jijini  Dar es Salaam Majira ya Saa tano asubuhi ambapo wananchi walijipanga barabarani na kuzuia magari kupita kuishinikiza serikali kuwalipa fidia ili waweze kuondoka katika eneo hilo.

Akizungumza katika eneo hilo  Katibu anayefutilia malipo ya wakazi hao Judith George alisema kuwa  wakazi hao wamelala  barabarani kutokana na serikali kuwapiga dana dana kulipwa hundi za nyumba zao ili waweze kuhama.

Alisema kuwa Viongozi wa Serikali pamoja na Mwekezaji  (EPZ) walifika katika eneo hilo March 13 mwaka huu na kufanya mkutano na wananchi kuhusu  uwekezaji katika eneo hilo.



Alisema kuwa Mwekezaji huyo alipozungumza nao walikubali kuhama kupisha ujenzi wa kiwanda katika eneo hilo la Mivinjeni na aliahidi kuwalipa fedha zao ili waweze kutafuta sehemu nyingine.

Aliongeza kuwa  mwekezaji huo alifuatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na kuahidi wakazi hao kuwapatia  Viwanja mbadala katika eneo la Kigamboni Uvumba Kibanda.

Alisema kuwa  baada ya hapo serikali ilishirikiana na Wilaya ya Temeke kufanya tathimini April mwaka huu ya nyumba zote za wakazi hao na kuweka x.

"Baada ya tathimini Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali kwa na mwekezaji walifanya tena tatahimini na kubaini kuna nyumba 60 zina matatizo  eneo la Shimo la Udongo Kurasini na kufanikiwa kuokoa sh Bilioni 1.4zilikuwa za usanii.

Aliongezea kuwa baada ya kufanyiwa tathimini walitangaziwa kwamba Agosti 26 mwaka huu wafike wilayani kwa jili ya kuchukua Hundi zao, lakini walipofika waliambiwa  zoezi la utoaji hundi limesitishwa.

Hata hivyo alisema kama zoezi la ulipaji wa fidia  limesitishwa kwa nini hawakutangaziwa kama walivyofanya mikutano mara ya kwanza ya kuambiwa eneo hilo linahitajika na mwekezaji.

Naye Mkazi Mwingine wa eneo hilo Mgeni Juma alisema  serikali imejaa usanii tu kutokana na mwekezaji kutoa fedha za kulipwa lakini wao wanasitisha bila kutoa taarifa kwa wananchi.

Alisema  kuwa kama serikali hiyo ikicheza 2015 hawaweze kupiga kura kutokana na kudanganya wananchi, tusije tukafanyiwa kama wakazi wa Kipawa walivyokuwa wanadanganywa mpaka leo.

Naye Rodi Panjo mkazi wa kurasini alisema  walipotangaziwa hundi zitaanza kutolewa  August 26 alisafiri kutoka Mbeya kuja kuchukua hundi yake lakini alipofika zoezi limesitishwa na ukizangatia nalala nyumba za wageni fedha ya kulipa nitapata wapi.

Mkazi mwingine Gerad Mahinya alisema  biashara zao zimefungwa kutokana na nyumba hizo kuwekwa alama ya x hali ambayo hawajui hatma ya maisha yao.

"Wakazi wengi wameshahama kutoka maeneo hayo na wengin walikopa kutoka  benki mbalimbali na kutafuta maeneo mengine ya kukaa huku wakitegemea kupata fedha zao ili kulipa  madeni ,"alisema.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke  Engelbert Kiondo aliwataka wakazi hao kuwa na subira na kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya saa nane ili kupata majibu ni lini watapewa  hundi zao.

Hata hivyo aliwataka wakazi hao kuwa wavumilivu na kuachia magari yaweze kupita ili alhamisi atawasilina na Waziri wa Ardhi aweze kwenda kuzungumza nao katika ofisi za serikali za mtaa wa kurasini.
 



No comments:

Post a Comment