Monday, August 5, 2013

WATUHUMIWA WATESWA NA POLISI

Washtakiwa wanne wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa kutumia silaha wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutokuwa na imani na afya zao kutokana na mateso waliyoyapata kwa polisi wa kituo cha Oysterbay wakati wa kuchukuliwa maelezo.

Washitakiwa hao ni Ally Hashimu, Donald Nzwenka, Michael Pascal, Kulwa Adamson na Yohanna, watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wiki iliyopita na baada ya kusomewa makosa yao mawili yanayowakabili mbele ya wakili wa serikali Flora Massawe mbele ya Hakimu Aloyce Katemana

Walidai kwa Hakimu Katemana kuwa hawana imani na afya zao kwani walipigwa na polisi hao wakati wa kuchukuliwa maelezo na kulazimishwa kukubali makosa wasiyoyafanya na mmoja wa washtakiwa hao, alisema kuwa ameingizwa msumari sikioni hivyo hasikii vizuri pamoja na kumkata na panga kwenye ncha za vidole vya miguu.



Kabla ya washitakiwa kudai hayo walisomewa mashtaka yao na wakili Massawe, alidai alidai kuwa washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la wizi kwa kutumia silaha kosa walilolitenda Julai 12, mwaka huu katika eneo la Mbezi Jet lililopo wilaya ya Kinondoni.

Hata hivyo washitakiwa hao walikana makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana na upelelezi upande wa jamhuri haujakamilika.

Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuwaambia washitakiwa kuwa watapatiwa matibabu

No comments:

Post a Comment