Tuesday, August 27, 2013
URUSSI YAONYA MASHAMBULIZI
Serikali za Urussi na Uchina, kwa mara nyingine tena zimetoa onyo dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa la Syria. Onyo hilo limetolewa huku Marekani na washirika wake wakijadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria, kujibu shambulio lililotokea wiki iliyopita.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urussi amesema, jaribio lolote la kutoshirikisha baraza la usalama la Marekani na kubuni kila alichokitaja kama visingizio ambavyo havina msingi, litakuwa na athari kubwa katika mzozo huo.
Utawala wa Moscow vile vile umeshutumu uamuzi wa Marekani wa kuhairisha mazungumzo ya kujaribu kutatua mzozo huo wa Syria. Wachunguzi hao wa Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kuendelea na uchunguzi wao hii leo kwa siku ya pili mfululizo, viungani mwa mji mkuu wa Damascus.
Jopo hilo la Umoja wa Mataifa lilishambuliwa kwa risasi hiyo jana na mtu mmoja ambaye aliwavizia Magharibu mwa Damascus. Shirika la habari la Serikali ya Uchina, Xinhua, limesema kuwa mataifa ya Magharibi, yamechukua uamuzi wa haraka kuhusu nani aliyehusika na utumizi wa silaha za kemikali nchini Syria hata kabla ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kukamilisha uchunguzi wao.
Hapo jana waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, alitoa matamshi makali kuhusu madai kuwa silaha za kemikali zimetumika nchini Syria na kusema kuwa waliohusika ni sharti wawajibishwe.
Labels:
news
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment