Mh: Iddi Azzan akizungumza na wanachama wa CCM wa kata ya Mwananyamala awataka wachague mafiga matatu ambayo ni Mh: Jakaya Mrisho Kikwete (Nafasi ya Urais), Mh: Iddi Azzan (Nafasi ya Ubunge) na Mwisho wamchaguwe Songoro Mnyonge (Nafasi ya Udiwani) ili kuendelea kuboresha kata hiyo, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Vijan hostel, Kinondoni.
Mh: Iddi Azzan akiwapa mikono wajumbe baada ya kumaliza kuongea na wa wanachama wa CCM kata ya Mwananyamala.
Mwenyekiti wa Jimbo la Kinondoni Mzee Yussuph Sisiyamoto katikati akiongoza mkutano na Kushoto kwake Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni.
Katikati ni Songoro Mnyonge Mgombea udiwani kata ya Mwananyamala akisikilza kwa makini.
Kada wa CCM na Mkufunzi wa mawakala wa usimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni Faustina Malema akitoa maelekezo mafupi kuhusu suala zima la upigaji kura mwezi October 31. dhumuni kubwa ni kuwataka wanachama wa CCM wasifanye makosa katika upigaji kura huo.
Macdonald ni mmoja kati ya washiriki walioshindwa katika kinyanga' nyiro cha kugombea kiti cha ubunge Jimbo la Kinondoni akiwahamasisha wanachama wa CCM wa kata ya Mwanayamala Kumuunga mkono Mh: Iddi Azzan.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mwananyamala wa kimkaribisha Mh: Iddi Azzan katika ukumbi wa mkutano. Vijana Hostel, Kinondoni.
Wanachama wakimkaribisha Mh: Iddi Azzan alipowasili katika ukumbi wa mkutano wa Vijana hostel, kata ya Mwananyamala.
Mh: Iddi Azzan akipata picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jimbo la Kinondoni Mzee Yussuph Sisiyamoto wa tatu kutoka kushoto na Katikati ni Mcdonald na wakwanza kulia ni kijana wa Chuo kikuu ambaye anahamasisha vijana katika kampeni za Jimbo la kinondoni za Mh: Iddi Azzan
Mh: Iddi Azzan na M/kiti wa Jimbo la Kinondoni Mzee Yussuph Sisiyamoto wakipata picha ya pamoja na Vijana wa Vyuo vikuu ambao pia ni wanaharakati wa Chama Cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment