Friday, September 3, 2010

WAZIRI MKUU, MZENGO PINDA ATAWAKILISHA GHANA

Picture
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) akizungumza na Rais wa Ghana John Atta Mills kwenye Ikulu yake mjini Accra.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda yupo Accra, Ghana kwa niaba ya Raisi Jakaya Kikwete, akiwakilisha Taifa kwa kuhudhuria mkutano wa siku tatu wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo barani Afrika.

Mkutano huu utakuwa chini ya wenyekiti wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annan.

Hii ni mara ya nne kwa mkutano kufanyika kwa ajili ya kujadili mapinduzi ya Kilimo barani Afria ambapo ni mwendelezo wa mikutano mingine mitatu ambayo ilikuwa ikifanyika jijini Oslo, Norway katika miaka ya 2005, 2007 na 2008, unatarajiwa kushirikisha wakuu wa nchi za Afrika, Mawaziri, Wawekezaji, Wakulima, Taasisi za kifedha, Taasisi binafsi zinazojishughulisha na kilimo, Asasi zisizo za Kiserikali (AZISE) na Wanasayansi.

Mkutano wa sasa umelenga katika kuinua uwekezaji katika kilimo kwa kupitisha sera ambazo zitasaida kuongeza tija katika kilimo na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima barani Afrika bila kuathiri mazingira. Mambo makuu matano yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni kuangalia fursa za uwekezaji, mazingira ya kisera, kupunguza gharama, kuongeza tija na mbinu za kuwanufaisha wakulima kifedha.

Waziri Mkuu
anahudhuria na kuiwakilisha Taifa kwa niaba ya Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment