Mh: Iddi Azzan akielezea sera zake kwa wananchi wa Kata ya Ndugumbi, aidha aliwaeleza wananchi wa Ndugumbi kuwa atahakikisha wanapata maisha bora akishirikiana na Mgonja ambaye ni Diwani wa kata hiyo pamoja na Mh: Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi.
Mh:Salum Londa ambaye ni mjumbe wa halimashauri kuu akimtambulisha Mh:Iddi Azzan baada ya kupanda kizimbani muda mfupi tu kabla ya kupewa nafasi ya kueleza sera zake.
Mgombea Udiwani kata ya Ndugumbi kupitia chama cha CCM Ndungu Mgonja akielezea sera zake kwa wananchi wa Ndugumbi wakati wakampeni za Jimbo la Kinondoni, kampeni hizo zilianza jana katika viwanja vya kata ya Ndugumbi.
Ndugu Mgonja mgombea Udiwani kupitia chama cha CCM akiwapa mikono viongozi baada ya kumaliza kutoa sera zake kwa wananchi wa Ndugumbi.
Mjumbe wa Halmashauri kuu Ndugu Asha Baraka akiwaombea kura viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM ambao ni Mh: Jakaya Kikwete katika nafasi ya Urais, Mh: Iddi Azzan katika nafasi ya Ubunge Jimbo la Kinondoni na Mgonja katika nafasi ya Udiwani kata ya Ndugumbi wakati wa kampeni zilizofanyika katika Viwanja vya Ndugumbi.
Mgombea Ubunge Jimbo la kinondoni Mh: Iddi Azzan na Mgombea Udiwani kata ya Ndugumbi Ndugu Mgonja wakipokelewa na Umati wa watu wakati wa kampeni zilizofanyika katika viwanja vya Ndugumbi.
Mh: Iddi Azzan na Ndugu Mgonja wakikaribishwa katika uwanja wa kampeni wa Ndugumbi. wana wandugumbi wakiimba kwa shangwe wakati wa makaribisho hayo.
Wanachama na wananchi wa Ndugumbi wakishangiri na kucheza huku wakiwa teyari kwa kumpokea Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni na Mgonja Mgombea Udiwani kata hiyo ya Ndugumbi.
Wananchi wakishangaa chereko chereko za Upokezi wa Mgombea Ubunge Mh: Iddi Azzan na Mgombea Udiwani Ndugu Mgonja. katika uwanja wa Ndugumbi.
Wanachama wakiwa teyari kuwapokea wagombea
Gari likiwa limerembwa na Picha za Viongozi wa Chama Cha Mapinduizi CCM, hili ni Moja ya magari yaliyokuwepo katika msafara wa kuelekea kwenye kampeni za Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni na Mgombea Udiwani Kata ya Ngumbi.
No comments:
Post a Comment