Tuesday, September 7, 2010

MH: IDDI AZZAN AANZA MCHAKOTO WA NDANI YA CHAMA


Mh: Iddi Azzan ambaye ni mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya kinondoni, akiwa hutubia wanachama wa CCM katika mkutano wa ndani wa chama hicho. aidha alielezea dhumuni la mkutano huo nikuvunja makundi yote yalioyokuwa ya mejengwa katika kipindi cha kura za maoni, na kuwataka wanachama wote kuwa kitu kimoja ili kujiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 31 mwaka huu. Aidha Mh: Iddi Azzan aliwapongeza wale wote walioshiriki kugombea nafasi hiyo ya Ubunge kwa kuvunja makundi yao na kunadi kumuunga mkono na kushirikiana kikamilifu kuhakikisha ndani ya Wilaya hiyo viti vyote vya mafiga matatu wanachuku CCM kwa kura za manyoya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa DDC, Magomeni kondoa kata ya Ndugumbi


Mh: Iddi Azzan Akipokelewa na Mwinyikiti pamoja na Wajumbe mbalimbali alipo wasili katika ukumbi wa mkutano wa DDC. Magomeni kondoa kata ya Ndugumbi.
 
Wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya ndugumbi wilaya ya kinondoni wakiimba na kupiga makofi kumkaribisha Mgombe wao wa Ubunge Mh:Iddi Azzan wakati wa Mkutano wa ndani wa chama hicho.

            Mpoki Mwamburukutu  na  Mkuruma (MalcolmX)
Macdonald Lunyilija

Hawa ni baadhi ya walioshiriki katika mchakato wakura za maoni  wa kugombea kiti cha Ubunge kupitia chama cha Mapinduizi katika jimbo la kinondoni.

No comments:

Post a Comment