Friday, September 3, 2010

Mh: Iddi Azzan, mgombea ubunge jimbo la kinondoni kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi "CCM" amezindua kampeni zake rasmi katika viwanja vya Mwinjuma



Mh: Iddi Azzan akihutubia wananchi wakati wa ufunguzi wa kampeni zake katika kata ya makumbusho Mwanayamala. katika hotuba yake alizungumzia mambo aliyofanikiwa kuyafanya ndani ya miaka yake mitano ya ubunge iliyopita, aliboresha elimu, miundombinu na vituo vya afya ikiwa pamoja na kuibadisha hospitali ya mwanyamala kutoka hospitali ya wilaya na sasa kutambulika kuwa ni hospitali ya mkoa wa kinondoni, ikiwa ujenzi wa maabara ya kisasa na wodi ya wazazi vinaendelea kujengwa katika hospitali hiyo na mwisho aliahidi kuendeleza yaleyote yaliyokuwa hayajakamilika katika kipindi chake kilichopita


Wagombea Udiwani katika kata kumi za wilaya ya kinondoni wakiwa katika uzinduzi wa kampeni kinondon
Muhammed kapelo akiwa na mwanachama mwezake wakimsubiri  mbunge wa jimbo la kinondoni
Mheshimiwa Iddi Azzan.


Wanachama wa chama cha mapinduzi wakiwa wanasubiri kumpokea Mgombea ubunge wa jimbo la kinondoni katika Ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya kinondoni"

No comments:

Post a Comment