Wednesday, September 22, 2010

MH:IDDI AZZAN, CHENGULA PAMOJA NA JK HAWANA MPINZANI KATA YA KIGOGO!!!

Mh: Iddi Azzan akiwaeleza sera zake wananchi wa kata ya Kigogo katika uwanja wa kigogo mwisho uliopo katika kata hiyo, mkutano huo ulikuwa wa aina yake kwa siku ya jana.
Mwenyekiti wa Jimbo la Kinondoni Mzee Sisiyamoto akiwaombea kura Viongozi wote wa chama hicho pamoja na Kumtambulisha Mgombea Ubunge Mh: Iddi Azzan na Mgombea Udiwani Ndugu Chengula. katika uwanja wa kampeni wa kata ya kigogo.
Mgombea Udiwani ndugu Chengula wa kata ya kigogo akitoa sera zake katika uwanja wa kampeni zilizofanyika katika uwanja wa kigogo mwisho ndani ya kata hiyo ya kigogo.
Mwenyekiti wa Kata ya kigogo akifungua mkutano wa kampeni uliofanyika katika kiwanja cha Kigogo Mwisho ndani ya kata hiyo.
Ndugu Mwinyikheri amabye alikuwa Chama cha CUF Jimbo la Kinondoni sasa arudi tena CCM akiwa hutubia wananchi wa Kigogo, asema kuwa wapinzani ni waongo hawana Mipango ya kuwasaidia wananchi.
Ndugu Maulid Selemani Mkwanju alikuwa katibu wa Vijana Wilaya kinondoni katika chama cha CHADEMA akieleza kwa nini aliondoaka ndani ya chama hicho. na kujiunga na chama cha CCM. asema kuwa viongozi wa chama hicho wote sio waaminifu.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mh: iddi Azzan aliyesimama akiwapungia mikono wananchi kwa dhumuni la kujitambulisha baada ya kikundi kimoja cha wasanii kutaka afanye hivyo. 
Diwani wa kata ya kigogo Ndugu Richard Chengula akipungia mikono wananchi baada ya kuambiwa kufanya hivyo na moja ya kikundi cha wasanii.
Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge jimbo la kinondoni akiwa na Ndugu Richard Chengula mgomea Udiwani wakiwa wanafurahi kwa pamoja kutokana na vituko vya wasanii.

Wananchi walivyofurika katika mkutano huo wa kampeni huko kata ya kigogo.

Wasanii wamakundi mbalimbali wakiburudisha katika uwanja huo wa kampeni ikiwa pamoja na makundi maarufu kundi la Fataki na Mizengwe. 
Palikuwa hapatoshi waliokaa juu ya nyumba, juu ya magari.
Watoto wakitaka kumsalimia Mh:Iddi Azzan na upande wa kulia Jamaa aliyeshika bango lenye ujumbe kwa jamii na pia amejichora jina la Azzan Kichwani kwake pamoja na la diwani Chengula. 
Umati wa watoto picha ya kushoto wakimzunguka Mh Iddi Azzan wakitaka kumsalimia. na Picha ya kulia ni umati wa watu wakimsindikiza kwenye gari Mh: Iddi Azzan.

Picha ya Kushoto Mgombea Ubunge Mh: Iddi Azzan na Mgombea Udiwani Ndugu Chengula wakiwa katika gari la wazi juu wakiwapungia mikono wannchi wao na Picha ya pili kulia ni wasanii wa Mizengwe wakiwa ndani ya gari na msafara wa Mh: Iddi Azzan wakati wa kuelekea kwenye kampeni.

No comments:

Post a Comment