Monday, September 27, 2010

Wanachama 34 kutoka CHADEMA na Mmoja Kutoka CUF wajiunga na CCM wakipokewa na Mh:Iddi Azzan,Kinondoni shamba.


Mh:Iddi Azzan awapongeza wanachama waliorudisha kadi na kukubali kuwa chama cha Mapinduzi ndio chama kinacho stahiki kupewa kura na kuendelea kuiongoza Tanzania kwa sera zake za maendeleo. pia alisema atahakikisha anisimamia sheria ya watoto  ya mwaka (2009) kuwa watoto lazima wapewe haki zao zote za msingi. Mwisho aliendeleae kutilia mkazo wananchi wasifanye makosa tarehe 31 na kuwataka waachague mafiga matatu yote ya CCM.
Mh:Iddi Azzan akimnadi Mgombea Udiwani Bi Husna na kuwaomba wananchi wampe kura ili waweze kushirikiana na yeye katika kuleta maendeoleo ya kata hiyo.
Kadi zilizorudishwa na wanachama 35 kutoka Chama Cha CHADEMA na Mmoja akitokea CUF. katika uwanja wa kampeni wa kinondoni Shamba.
 Mh:Iddi Azzan akimkabidhi nguo za CCM Ndugu Mgendi baada ya kurejesha kadi yake ya CHADEMA.
Mh:Iddi Azzan akimpa nafasi ya kujielezea Mwanachama aliyerejesha kadi ya chama cha CHADEMA na kuhamia chama cha Mapinduzi hapo jana katika uwanja wa kinondoni shamba.
 Mh:Iddi azzan akiwa na mjuu kuu wa Mgombea udiwani Bi husna. ambaye amekaa upande wakushoto.
Wasanii wa Wafataki wakitoa burudani kwa wananchi wa kinondoni shamba
Kikundi cha Mizengwe ambacho kinashugulika na maswala ya uigizaji, wa kifanya igizo fupi katika uwanja wa mkutano wa kampeni.

Mtoto mdogo akionyesha kipaji chake cha kucheza mbele ya Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi. katika uwanja wa kampeni wa kata ya kinondoni.
Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa kampeni kinondoni shamba.
Wananchi pamoja na makada wa CCM wakiwa wamenyosha mikono wakiashiria kukubali kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment