Monday, September 20, 2010

MH:IDDI AZZAN ASEMA TANDALE ITAENDELEA KUJENGWA.

Mh: Iddi Azzan akitoa sera zake kwa wananchi wa kata ya Tandale kwenye uwanja wa Mkunguje, alisema yafuatayo;

1-Aliwaambia kuwa wanashughulikia suala la kujengwa kwa barabara hiyo ya Mkunguje na pia kurekebisha sehemu hiyo kuhusiana na suala zima la maji ya mvua kukaa hapo.

2-Katika suala la huduma ya afya katika kata hiyo teyari tumejenga Zahanati ambayo tunaipandisha hadhi na kuwa hospitali inayotumika kwa ajili ya wananchi wa kata hiyo, pia tumefanikiwa kuboresha na kupandisha hadhi Hospitali ya Mwananyamala kuwa Hospitali ya Mkoa, ikiwa pamoja na kujengwa Maabara ya kisasa, wodi mpya ya wazazi na watoto, na mengine mengi, na sasa matibabu yote yatakuwa yanapatika na pia madaktari bingwa watakuwepo hapo katika Hospital hiyo.

3-Pia alisema kuwa katika wakati wake alifanikiwa kuishawishi serikali kujenga shule na alifanikiwa kujenga shule tano katika Jimbo la Kinondoni chini ya uongozi wake uliopita kuanzia mwaka 2005 mpaka 2010, wakati kabla ya hapo kulikuwa na shule moja tu. pia alieleza kuwa suala la Walimu limeshashughulikiwa na kwa sasa Chuo kikuu cha Dodoma kitakuwa kina chukua wanafunzi takriban elfu tano ambao wanasomea uwalimu tu. kwa hiyo nimategemeo yake kuwa Vijana wengi watajitokeza ili kuchukua nafasi hizo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu la leo na kesho.

Mwisho aliwaomba wananchi wa mpe kura za ndio Mh: Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi ya Urais, Diwani wa kata hiyo Mzee Chilu Manga na yeye Mweneyewe katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kinondoni.
Diwani wa kata ya Tandale Ndugu Chilu Manga akimwaga sera zake kwa Wananchi wa kata hiyo wakati wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi zikifanyika katika Uwanja wa Mkunguje.
Diwani wa zamani wa kata hiyo ya Tandale Ndugu Mwilima akiwahutubia wananchi wa kata hiyo ya Tandale wakati wa kampeni za CCM zilizofanyika katika Uwanja wa Mkunguje.
Mh: Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la kinondoni na Diwani wa kata ya Tandale Ndugu Chilu Manga wakiangalia wasanii waliokuwa wakiburudisha wakati wa kampeni hizo zilizofanyika Uwanja wa Mkunguje.
Mh: Iddi Azzan akimwambia kitu Diwani wa kata ya Tandale Ndugu Chilu manga. ikiwa Mwenyekiti wa kata hiyo ya Tandale anasikiliza kwa makini.
 Mh: Iddi Azzan akiwa anaangalia wasanii waliokuwa wa kiburudisha jukwaani   
Mh: Iddi Azzan akimuelekeza kitu Ndugu Macdonald huku mtoto mdogo akienda kukaa karibu yake akiwa ameshikilia picha ya Mgombea huyo. hii nikuonyesha jinsi gani anvokubalika kwa jamii.
Wananchi kata ya Tandale wakiwa wanamsikiza sera za Mgomba Ubunge Mh:Iddi Azzan na Mgombea Udiwani Ndugu Chilu Manga wakati wa kampeni zilizofanyika Uwanja wa Mkunguje.
Viongozi wa Jimbo la Kinondoni, Viongozi wa kata ya Tandale na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni wa pili kutoka kushoto Mh: Iddi Azzan  pamoja na Mgombea Udiwani kata ya Tandale wa tatu Kutoka kushoto Ndugu Chilu Manga wakiwa wamewasili katika uwanja wa kampeni wa Mkunguje uliopo kata ya Tandale.
Wananchi wakiwa wanashagilia kwa kuwasili kwa Viongozi hao katika uwanja wa kampeni wa Mkunguje uliopo kata ya Tandale.
Wasanii wa Mizengwe Kushoto na Fataki kulia wakitoa burudani katika uwanja wa kampeni wa Mkunguje kata ya Tandale Jimbo la Kinondoni.

    
Picha nne za hapo juu zikionyesha mapokezi ya Mgombea Ubunge  wa jimbo la kinondoni Mh: Iddi Azzan  katika Uwanja wa kampeni wa Mkunguje uliopo kata ya Tandale
WATOTO WA MKUBALI MH: IDDI AZZAN.
Mh: Iddi Azzan akishangilia na watoto wakati alipowasili nyumbani kwake baada ya kutoka kwanye kampeni zake zilizofanyika uwanja wa Mkunguje kata ya Tandale.


No comments:

Post a Comment