Monday, September 27, 2010

Mh:Iddi Azzan awaomba wananchi wa kata ya Kijitonyama wamchague yeye katika nafasi ya Ubunge na wamchague Diwani Bulembo pamoja na Mh:JK katika nafasi ya Urais.

Mh:Iddi Azzan mgombea Ubunge Jimbo la kinondoni akiwa amekaa pamoja na Mgomea Udiwani wa kata ya kijitonyama.
Mh:Iddi Azzan akiwapungia mkono wa salamu wananchi wa kata ya Kijitonyama katika Mkutano wa kampeni uliofanyika Alimaua kata ya Kijitonyama. aidha aliwataka wananchi wamchague yeye mwenyewe katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kinondoni na wamchague Mgombea udiwani wa chama cha Mapinduzi Ndugu Bulembo Abdallah  ili waendeleze yale waliokuwa hawayajamaliza katika kipindi kichopita. pia aliwaomba kumpigia kura Mh: Jakaya Kikwete kwa kuwa ni rais mwenyesifa na vigezo vyote vyakuendelea kuiongoza nchi hii.
Mgombea Udiwani Ndugu Bulembo akieleza sera zake kwa wananchi wa kata ya Kijitonyama na kuwataka wachague mafiga matatu.
Mh: Mgeni rasmi ndugu Msabah akiwaombea kura Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni Mgombea Ubunge Mh:Iddi Azzan na Mgombea Udiwani Ndugu Bulembo Abdallah pamoja na Mgombea Urais Mh:Jakaya Mrisho Kikwete. katika uwanja wa Alimaua, kata ya Kijitonyama.
Wananchi walikuwa wengi sana.


No comments:

Post a Comment