Wednesday, September 11, 2013

ASILIMIA 23 YA WANAUME WAKIRI KUBAKA

Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu unyanyasaji dhidi ya wanawake imesema takriban robo ya wanaume wamekiri kubaka japo mara moja.

Hata hivyo kulingana na ripoti hiyo mwanaume mmoja kati ya 10 amekiri kumbaka mwanamke ambaye si rafiki yake. Kwa mujibu wa BBC, Wanaume 10,000 kutoka nchi sita walishiriki katika utafiti huo, nchi hizo ni pamoja na Bangladesh, Sri Lanka, Cambodia, China, Indonesia na Papua New Guinea.


Huo ni utafiti wa kwanza kuhusu nchi nyingi kuchunguza jinsi unyanyasaji unavyoongezeka dhidi ya wanawake na sababu zinazosababisha. Kwa wale waliokiri kubaka walio chini ya nusu walisema wamefanya hivyo zaidi ya mara moja, hata hivyo kiwango cha ubakaji kinatofautiana kati ya nchi na nchi.

Nchi ya Papua New Guinea, zaidi ya wanaume sita kati ya 10 waliofanyiwa utafiti walikiri kuwalazimisha wanawake kufanya ngoni





No comments:

Post a Comment