Wednesday, September 18, 2013

MSEMAJI WA BROTHERHOOD AKAMATWA


Msemaji rasmi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood amekamatwa nchini Misri. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali. Gehad al-Haddad alikamatwa akiwa na mwanachama mwingine mmoja wa vuguvugu hilo katika nyumba moja mjini Cairo.

Serikali ya Misri imekuwa ikifanya msako dhidi ya makundi ya kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi Julai.Bwana Haddad aliwahi kuhudumu kama afisa wa ngazi ya juu wa naibu mkuu wa majeshi, Khairat al-Shater, wa vuguvugu hilo na kawaida alizungumza na vyombo vya habari vya kigeni.

Awali, mahakama ya uhalifu mjini Cairo, iliamua kuwa mali zote za viongozi wa vuguguvu hilo pamoja na lile la Gamaa Islamiya kupigwa tanji. Viongozi wa mashtaka waliwaekea vikwazo maafisa wa ngazi ya juu wa Brotherhood akiwemo, Mohammed Badie, Shater na wengine wengi mnamo mwezi Julai.

Wengi wao wamezuiliwa kuhusiana na madai ya kuchochea ghasia na mauaji. Mamia ya watu wanataka Bwana Morsi kurejeshwa mamlakani , wengi wakiwa wanachama wa Brotherhood .Aidha makabiliano yaliyotokea mwezi jana kati na polisi na wafuasi wa Morsi yalisababisha vifo vya wanachama wengi pale polisi walipovamia kambi zao mbili walipokuwa wanataka Morsi kurejehswa mamlakani.

No comments:

Post a Comment