MSANII wa filamu nchini Single Mtambalike 'Richi Richi' amekuwa kivuto katika uzinduzi wa filamu ya Foolish Age uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, baada ya kupanda jukwaani na 'kummwagia' kitita cha fedha msanii mwenzake Elizabety Michael 'Lulu'.
Richi alijikuta akivutiwa na msanii Lulu mara baada ya kuimba kibao cha Yahaya kilichoimbwa na muimbaji Lady Jaydee, mara baada ya kumaliza kuizindua movi yake hiyo ambapo alitoa fursa kwa mashabiki wake waliohudhuria uzinduzi huo kuiangalia kwa dakika 10.
Richi alishindwa kuvumilia mara baada ya kusikia msanii huyo anaimba nyimbo ambayo kwa upande wake inamvutia, hali iliyopelekea kupanda jukwaani na kumwagia kitita cha fedha huku akionyesha kuifurahia nyimbo hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mara baada ya kushuka jukwaani aliweka wazi kuwa hakufikiria kama msanii huyo angeweza kuimba jukwaani hapo hususani nyimbo hiyo.
"Kiukweli Lulu anakipaji na pengine anavipaji vingi tofauti kikiwemo hicho cha uwimbaji, kilichonivutia ni jinsi alivyoweza kulimiliki jukwaa hilo na kuifanya nyimbo hiyo kama ya kwake' alisema Richi.
Alisema kuwa baada ya kuisikia ile sauti hakuweza kuitambua kama ni ya Lulu, aliitambua na kupatwa na mshtuko alipomuona msanii huyo ndiye anayeimba jukwaani hapo hali iliyompelekea kwenda kumtunza kiasi alichonacho.
Aliongezea kuwa wasanii wanatakiwa kumuunga mkono msanii huyo ili aweze kukuua zaidi ya hapo alipo na kutimiza malengo yake.
No comments:
Post a Comment