Friday, September 13, 2013

OMBAOMBA, MACHANGUDOA WAKAMATWA

Ombaomba zaidi ya 200 na wasichana wanaofanya biashara ya ngono maarufu kama ‘dada poa’  usiku wa kuamkia jana walikamatwa kwenye operesheni maalumu ya kuwaondoa katika maeneo mbalimbali ya jiji,iliyofanywa kwa ushirikiano wa Polisi na askari wa jiji.

Ombaomba na kinadada hao walikamatwa kwenye Manispaa ya Kinondoni na Ilala ambapo baadaye walihifadhiwa kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa(Sabasaba) kabla ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Jiji kwa makosa ya uzurulaji.


Ombaomba hao baada ya kufikishwa mahakamani hapo  walitakiwa kurudi katika makazi yao kuanzia leo  ili wasichukuliwe hatua za kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick alipohojiwa alisema,operesheni hiyo,imebaini zaidi ya asilimia 70 wanatoka mikoani .

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kukamatwa kwa ombaomba hao na kueleza kuwa zoezi hilo ni endelevu.

No comments:

Post a Comment