Thursday, September 5, 2013

BUNGE LAGEUKA UWANJA WA VITA

UKUMBI wa Bunge leo uligeuka kuwa ulingo wa ngumi baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kutunishiana misuri na askari wa bunge hilo ambapo Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe alipoamliwa kutoka nje na Naibu Spika Job Ndugai.

Hatua hiyo ilitokana baada ya wabunge hao kupiga kura za kukubali au kukataa kuhusu kupitishwa kwa kujadili Mswaada wa Katiba uliopelekwa Bungeni hapo na Serikali ili kuweza kujadiliwa na bunge hilo.

Wabunge hao wa kambi ya upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe walipinga matokeo hayo na kuamua kusimama na wakati huo huo Spika Ndugai aliwataka kukaa chini ili kuendelea na kuchangia hoja za msingi za kujadili mswaada huo.

Ndugai aliwataka wabunge hao kukubaliana na matokeo yaliyotokea na kwa pamoja waweze kujadili mswaada huo ambao ni faida kwa taifa lakini mbali na ombi hilo kambi ya upinzani walikaidi ndipo Spika alitoa dakika tano kwa za kiongozi huyo kutoka ili bunge liendelee,ambapo hata hivyo kiongozi huyo alikaidi amri hiyo.

Baada ya mabishano hayo ndipo Spika alipotumia kiti chake na kuwataka askari wamtoe kwa nguvu nje ya ukumbi wa bunge ,amri ambayo ilizua taflani na hekeheka kupelekea wabunge wa kambi ya wapinzani kuungana na kuwatunishia misuri askari hao wakimkingia kiongozi huyo kutolewa nje.

Tukio hilo lililochukua dakika zaidi ya 30 lilipelekea Bw. Job Ndugai kuwatolea macho askari hao akiwaamuru kutumia mabavu ili kuweza kumtoa nje ya ukumbi Bw. Mbowe.

Sakata hilo lilifanikiwa baada ya askari hao kutii amri ya Naibu Spika huo kwa kutumia mabavu kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzani ambapo aliungwa mkono na wabunge kutoka nje ya ukumbi na kususia kikao hicho.

Katika tukio hilo Mwenyekiti wa vyama vyenye wabunge wengi bungeni na Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjari Agustino Mrema alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge wezake si cha kungwa na na kinaleta fedheha kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema yeye kutokutoka kwake nje haimaanishi kuwa ni kibaraka wa CCM na si ndicho alichotumwa kufanya na wananchi wake,hivyo haungi mkono hata kidogo na haeleweke hivyo kuhusu msimamo wake.

"Hatoki mtu hapa nitakaa ndani ya bunge mpaka kieleweke na mnielewe kwamba mimi ndiye kiongozi wao vyama vyote tisa,hivyo nastahili kuheshimiwa na sikubaki humu ndani kwa sababu mimi ni kibaraka wa CCM bali kinachopiganiwa ni maslahi ya taifa na ndicho nilichotumwa na wananchi wangu sikutumwa nije kutoka nje au kususia bunge."alisema Mrema.

Naye, Mbunge wa Same Mashariki na Bi Anne Kilango Malecella aliitaka Serikali kusimama imara na isiogope vitisho vinavyotolewa na wasioitakiwa mema nchi katika kupigania maslahi ya taifa.

Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wapinzani bungeni hakina nia njema katika kupata katiba mpya na wajumbe 156 waliopiga kura wanavigenzo vya kuweza kuchangia Mswaada huo kujadiliwa.

Vurugu za bunge hilo ziliaza toka awali katika kipindi cha muongozo wa Spika ambapo vijembe,kashifa kwa wabunge kuzungumza bila kufuata utaratibu ilimradhimu Naibu Spika Job Ndugai kusimama mara kwa mara kujaribu kurejesha utulivu katika matukio yaliyotawala Ukumbini humo.

Mara baada ya kutolewa mwongozo ulioombwa na wabunge juzi wakidai Muswada wa Mabadiliko ya rasimu ya katiba umeingizwa vipengele kinyemele, na Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu, wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na wale wa CCM walikuwa wakituhumiana kusema uongo kuhusiana na hatua hiyo ya uandaaji wa mchakato wa Rasimu wa Katiba mpya.

Hali hiyo ilipekea wabunge hao kuchambua vipengelee mbali mbali vya sheria vya kutafasili kanuni za bunge kwa wabunge ambao wanasema uongo bungeni ambapo msemaji wa Kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu alisema Kanuni ya 61 A inawataka wabunge kutotoa taarifa zisizo na ukweli bungeni huku kipengele 63 (3)kinamtaka mbunge mwingine anayeweza kusimama nakusema mbunge aliyesema kabla yake alisema uongo hivyo Tundu Lissu alisema mwenyekiti wa Katiba juzi alisema uongo kuwa wazanzibar wametoa maoni katika kamati ya katiba.

Lissu alisema yeye akiwa ni mmoja wa wanakamati waliambiwa kamati haiwezi kwenda zanzibar kwa sababu za kiusalama hivyo mwenyekiti huo amelidanganya bunge.

Muongozo huo ulipelekea Waziri Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Sera wa shughuli za Bunge William Lukuvi kutaka kiti cha Spika kichukue hatu zidi ya wanaotumia bunge ambalo ni chombo cha sheria kudanganya na fitirisha pamoja na kutumia jina la rais kwa dhihaka.

Alisema kuwa msemaji huyo wa kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu ameshawishi wabunge na wananchi kuamini uongo kuwa uteuzi wa rais katika uundwaji wa kamati ya maoni ya katiba amelenga watu anao wafahamu kwa maslahi yake na si kwa maslahi ya watanzania.

Lukuvi alifafanua kuwa uteuzi wa rais katika uundwaji wa tume hiyo umezingatia matakwa ya sheria kwa kushirikisha mapendekezo ya kila Sekta ikiwemo vyama vya hiari,walemavu,taasisi za dini,vyama vya maendeleo ya Jamii na vyama vya Siasa kikiwemo Chadema ambapo kati ya majina yaliyopendekezwa ni pamoja Tundu Lissu hakuchaguliwa kwa sababu hakuwa na sifa ya kumzidi Professa Baregu kati ya majina yaliyopendekwaza na Chama hicho.

Akiomba ufafanuzi muwasilisha wa mjadala huo bungeni Ally Hamisi Seif aliomba hoja ya kuondolewa kwa msaada huo wa sheria kwakua hakuna ushirikishwaji wa kutosha kwa wazanzibar katika mchakato wa kuandaa rasmu ya Katiba mpya kutokana na kamati kutokupokea maoni ya wananchi wa zanzibar.

Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Freem Mbowe lililohoji kuwa msaada huo una maeneo makubwa yatakayoleta ufa nchini , hivyo yakafanyiwe malekebisho kabla ya mswaada wake kujadiliwa bungeni.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu swali hilo alisema kuwa hakuna haja ya mswaada huo kuondolewa kwani kabla ya kuletwa bungeni kulikuwa kunafursa kwenye kamati mbalimbali,na tofauti zilizopo zinazungumzika ili uweze kujadiliwa.

Naye, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia alishauri Serikali umuhimu wa majadiliano hayo kufanyika kwa uwazi kabla ya kisheria ili kusaidia maana halisi ya kuunda dola kwani kura ya maoni ya zanzibar inaeleza wazi mgogoro wa kikatiba uliopo ambapo ulipelekea hata mamlaka ya kugawa ardhi aliyonayo rais wa Tanzania hufanywa na rais wa zanzibar katika ardhi ya zanzibar.

Akijibu swali hilo Pinda alisema hana tatizo na ushauri wa Mbatia ila ungekuwa na nafasi endapo katiba mpya isingekuwepo kwani ndiyo itakayofuta tofauti zilizopo.

Hata hivyo Sakata hilo liliaza Juzi jioni wakati wabunge wa Chadema na Cuf kuwa kitu kimoja na kuamua kutoka nje baada ya Tundu Lissu kuwsiliha maoni ya kambi hiyo huku akieleza kuwa wananchi wazanzibar hawakushirikishwa kwenye maoni ya rasmi ya katiba mpya.

No comments:

Post a Comment