Tuesday, September 24, 2013

BENDI YA KALUNDE KUVAMIA TEGETA, BOKO


BENDI ya muziki wa dansi nchini inayokuja kwa kasi ya Kalunde, ikiwa katika harakati zake za kuipua albamu yake ya tatu, sasa itakuwa ikitumbuiza katika viwanja vya Tegeta na Boko.Kalunde kwa sasa iko kambini ikijiandaa na albamu yao ya tatu, baada ya zile za Hilda na Imebaki stori ambazo zinatesa katika anga za muziki nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana Rais wa bendi hiyo, Deo Mwanambilimbi alisema wameamua kucheza na viwanja vya Tegeta na Boko kwa kuwa kwa sasa wapo kambini kujiandaa na albamu hiyo mpya. "Tunataka kuwapa vitu adimu wakazi wa maeneo ya Tegeta na Boko kwa kuwa wengi wao wanashindwa kuja katika shoo zetu kutokana na umbali, lakini sasa wana kila sababu ya kujidai," alisema Mwanambilimbi.

Alisema kila Alhamisi kwa sasa watakuwa wanatumbuiza katika Ukumbi wa Hisege ulioko Boko Magengeni na kila Jumamosi uhondo utapatikana kwenye Ukumbi wa Nyama Chabisi Tegeta.


Rais huyo alisema bendi yake itakuwa inapiga nyimbo mchanganyiko katika kumbi hizo zikiwemo zilizomo kwenye albamu za Hilda, Imebaki stori na mpya ambazo zitaingia kwenye albamu mpya.

Alisema katika albamu ya Hilda watapiga nyimbo za Itumba Ngwewe, Kiliokilio, Fikiria na Nakata kuzaa na wewe, wakati Imebaki stori zitapigwa Njoo tucheze, Mama yangu, Sisee na nyingine.

No comments:

Post a Comment