Wednesday, September 11, 2013

WANAWAKE 26 KILA SIKU KUPOTEZA MAISHA TANZANIA

TWAKIMU za hivi karibuni zinaonesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya vifo votokanavyo na uzazi huku wanawake 26 hupoteza maisha kila siku ambapo vifo hivyo asilimia 19 vinachangiwa na utoaji wa mimba usio salama.

Takwimu hizo ziimetolewa na shirika lisilo la kiserikali Marie Stopes (MST) ambapo iliweka wazi kuwa asilimia 16 tu ya vijana ndio walio katika umri wa uzazi wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango


Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa shirika hilo Bw. Johnbosco Baso alisema takwimu zinaonesha vijana 8000 waliacha shule kwa sababu ya mimba za utotoni kwa mwaka 2010,hali inayopelekea kijana kupoteza dira ya maendeleo.

Alisema kuwa inatakiwa kuwaelimisha vijana  kuwa na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango ili kuepuka mimba katika umri mdogo ambapo itawasaidia kutimiza malengo na ndoto zao za baadae.

Baso alisema mimba za utotoni zimechangia kwa kiasi kikubwa utoaji wa mimba usio salama unaopelekea vijana wengi kupoteza maisha .

No comments:

Post a Comment