Sunday, October 31, 2010

MHE.IDDI AZZAN AKIPIGA KURA, HUKU ZOWEZI LA KUPIGA KURA LIKIENDELEA VIZURI KATIKA MAENEO MBALIMBALI, DAR ES SALAAM.

Mhe.Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia tiket ya CCM akiwasili katika kituo cha kupigia cha kura katika shule ya msingi ya Alhassan Mwinyi.

Msimamizi wa kituo cha kupiga kura akimuonyesha Mhe.Iddi Azzan Jina lake.

Mhe.Iddi Azzan akifuata taratibu za upigaji kura akionyesha kadi yake ya kupiga kura kwa Msimamizi.

Msimamizi akimkabidhi karatasi za kupigia kura Mhe.Iddi Azzan Mgomba Ubunge Jimbo la Kinondoni.
Mgombea Ubunge Mhe.Iddi Azzan akipiga kura yake kwenye chumba maalum kilicho andaliwa kwa kazi hiyo ya upigaji wa kura.

Akitumbukiza kura yake kwenye Sanduku la bluu ambalo ni la Mbunge.

Akitumbukiza kura yake kwenye Sanduku jeupe ambalo ni la Diwani.

Akitumbukiza kura yake kwenye sanduku Jeusi ambalo ni la Rais.

Msimamizi akimpaka wino Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni.

 Watu wakionekaniwa kwenye hali ya utulivu katika kituo cha kupiga kura kilichopo Sinza "A"

 Wananchi wakionekaniwa ni wenye kujitokeza kwa wingi katika vituo vya upigaji kura huko Sinza.

 Hali ya Upigaji kura ikionekaniwa ni ya utulivu sana katika maeneo yote ya vituo vya upigaji kura, hapa ni shule iliopo Tandale wananchi wakionekaniwa wakiangalia majina yao.

KILELE CHA KAMPENI CHAFIKIA MWISHO HUKU MHE.DK JAKAYA KIKWETE AKIFUNGA KAMPENI ZAKE VIWANJA VYA JANGWANI.

JK akipanda jukwaani kwa mbwembwe huku akicheza nyimbo ya bongo flava ya kizazi kipya kabla ya kuhutubia mkutano wake wa mwisho wa kampeni viwanja vya jangwani jijini Dar jana.
JK akimpa mkono mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kuhutubia huku mgombea mwenza Dk. Mohamed Ghalib Bilal, Katibu Mkuu wa CCM Mh. Yusuf Makamba, Makamu wa CCM (Bara) Mh. Pius Msekwa na marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mh. Benjamin Mkapa pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba wakisubiri zamu zao
JK akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni ya Jana.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
Rais Benjamin Mkapa akihutubia
Meza kuu ikimpongeza rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa kwa hotuba iliyotukuka
Rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa akiwa na mawaziri wakuu wastaafu Dk. Salim Ahmed Salim, Mh. Joseph Sinde Warioba na Mgombea mwenza wa JK , Dk. Mohamed Ghalib Bilal
Mheshima Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa 
Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani.
Dk.Jakaya Kikwete akipokelewa kwa nderemo alipowasili Jangwani
Nyomi haikuwa ya kawaida Jangwani.
Sehemu ya nyomi ya CCM Jangwano leo


Friday, October 29, 2010

MHE.IDDI AZZAN AFUNGA KAMPENI ZAKE KIGOGO.

Mhe.Iddi Azzan akiwahutubia Wananchi wa Kigogo wakati wa kufunga kampeni zake katika kata hiyo,akiendelea kunadi sera zake ikiwa ni kuendeleza kuleta maisha bora kwa kwata hiyo, akiwaomba Wananchi kufanya uchaguzi sahihi kwa kuwapigia kura viongozi wa CCM kuanzia Urais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, Ubunge Mhe.Iddi Azzan kwa Jimbo la Kinondoni na Diwani wa Kata Hiyo Ndugu Chambuso.
 Mgombea Ubunge Mhe.Iddi Azzan akimdani Mgombea Udiwani wa kata ya kigogo Ndugu Chambuso kwa niaba ya Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mhe.Iddi Azzan akimkabidhi kadi ya CCM bibi ambaye ameamua kujiengua chama cha Wananchi CUF.
 Mhe.Iddi Azzan akiomba ridhaa kwa Maelfu ya Wananchi waliohudhuria katika Mkutano wake wa Kufunga Kamepeni katika kata ya Kigogo.
 Mhe.Iddi Azzan akijadili kitu na ndugu Ahmed Zein ambaye ni kada wa CCM pamoja na Diwani wa Kata ya Kigogo Ndugu Chambuso.
Mmoja wa wanachama wa CCM akiwa anasikiliza kwa makini sera za mgombea Mhe.Iddi Azzan
 Wananchi wakisikiliza kwa makini sera za Mhe.Iddi Azzan
Umati Wa Wananchi walifurika katika viwanja hivyo vya kata ya kigogo.
 kikosi Cha Kampeni kikiwa pamoja.
 Kikosi cha Kampeni kikiwa na Mhe.Iddi Azzan
Mhe.Iddi Azzan akiwa na Kikosi chake cha Kampeni.

Thursday, October 28, 2010

MHE.ALI HASSAN MWINYI AMNADI MBUNGE WA KINONDONI.

Mhe.Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu akisiitiza kwa Wananchi kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi na Kumchagua Mgombea Urais Mhe.Jakaya Kikwete Gari kubwa, Mbunge na Madiwani katika Mkutano wa kampeni uliofanyika Magomeni makuti viwanja vya CCM. 
Rais Mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan katika kata ya Mgomeni(Uwanja wa Nyumbani) ndiko anakotokea Mhe.Iddi Azzan.
Mgomba Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwahutubia Wananchi na kuwaeleza sera zake ikiwa ni kuboresha Vituo vya Afya,barabara,Elimu,Maji na kujenga Zahanati kwa kila kata. Pia akiwaomba Wananchi Kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi kuanzia Urais Mhe.Jakaya kikwete, Mbunge kwa Jimbo la Kinondoni yeye mwenyewe Mhe.Iddi Azzan na Madiwani wote wa kata zote za Jimbo hilo.
Rais mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi akiwani Wagombea Udiwani kuanzia (Kulia) Mgonja kata ya Ndugumbi, Husna Kata ya Kinondoni na Mwisho (kushoto) Bulembo kata ya Magomeni, akiwaomba Wananchi wa wachague ili waweze kushirikia na Mbunge na Rais.
Mhe.Iddi Azzan akimpa mkono Rais Mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi baada ya kumaliza kuhutubia Wananchi waliohudhuria Mkutano huo wa kampeni.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea ubunge Mhe.Iddi Azzan.

 Mtu nyomiiii.
Wananchi wakiwa wametulia kusikiliza yaliyo anadaliwa.
 Waigizaji wa Mizengwe wakiburudisha...!
 Chipukizi Mohammed akiwaburudisha Wananchi kwa Sera zake za kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi
Kikundi cha wa kina dada kikiburudisha jukwaani kwa nyimbo ya alajiiiii.




DR.GHARIB BILALI AFANYA KAMPENI KIJITONYAMA,DAR

Mheshimiwa DR.Mohammed Gharib bilali akiwahutubia Wananchi katika Viwanja vya Shule Kijitonyaama,sera yake ilikuwa inahusu kutengeneza vitabu vya Sayansi mashuleni ili kuwapa urahisi Wanafunzi kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Pia alimuombea kura Mgombea Urais Mhe.Dr.Jakaya Kikwete, Wabunge na Madiwani. Wote wa CCM.
Mgombea Mwenza Dr.Gaharibu Bilali akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan katika Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Shule Kijitonyama.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwasalimia Wananchi na kugusia sera zake za kuboresha makazi, huduma za afya na Elimu. Aidha aliwaomba Wananchi ridhaa ya kumchagua tena ili kuendelea kuwaletea maisha bora.
Mhe.Dr.Mohammed Gharib Bilali akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Kijitonyama Ndugu Bulembo ili kuweza kuiongoza kata hiyo.
Mke wa mgombea Mwenza, Bi-Zakia Bilali akiwaombea kura Viongozi Wote Wa CCM Kuanzia Urais DR.Jk , Wabunge na Madiwani Wote.
 Bi-Zakia Bilali akiwa amekaa karibu na Mwenyekiti wa Wilaya ya kinondoni wakimsikiliza Mgombea Mwenza Mhe.Dr.Mohammed Gharib Bilali.
Mhe.Iddi Azzan akiwa meza kuu akisikiliza kwa makini Hotuba ya Mhe.Dr.Gharib Bilali.
Wananchi wakisalimiana na Mhe.Iddi Azzan baada ya kumalizika kwa mkutano.
Baadhi ya Vijana wakimweleza kitu Mhe.Iddi Azzan.
Mhe.Iddi Azzan akionekaniwa mwenye furaha wakati akisalimia na Wananchi huku Mhe.Asha Baraka akionekaniwa mwenye kushanga kitu,baada ya kumalizika kwa mkutano wa kamepeni za Mgombea
 mwenza zilizofanyika katika viwanja vya shule Kijitonyama.