Saturday, October 16, 2010

MH.IDDI AZZAN AMWAGA SERA KATA YA KINONDONI.

Mh.Iddi Azzan awaambia Wananchi wa kata ya Kinondoni kuwa viongozi wapo wengi ila wananchi wanatakiwa kuchagua kiongozi bora na kiongozi bora hatoki kokote isipokuwa Chama Cha Mapinduzi, kwa hiyo anawaomba Wananchi na Wana CCM kukipigia kura Chama Cha CCM ifikapo tarehe 31th Oct 2010.

Pia aliwaahidi Wananchi kuwa atasimama imara kuhakikisha Watoto wadogo wanapata haki zao za msingi kupitia sheria ya Watoto iliyoundwa Mwaka 2009.

Mwisho aliwaomba Wananchi wote kuwapa kura za ndio viongozi wote wa CCM, Kuanzia Urais,Ubunge na Udiwani ili kuweza kakimisha mafiga Matatu
Katibu mwenezi wa Mkoa Ndugu Juma Simba akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan katika Mkutano wa Kamepni zilizofanyika kata ya Kinondoni.
Mgombea Udiwani wa kata ya kinondoni Ndugu Husana akiwaomba ridhaa Wananchi kumchagua katika Nafasi ya Udiwani ifikapo tarehe 31 Oct 2010, pia alisema kuwa atasimama imara kuhakikisha eneo hilo la kisiwani miundo mbinu inaboreshwa na kupeleka maji safi katika eneohilo ili wananchi waweze kupata kupata huduma zilizobora.
Ndugu Juma Simba ambye ni Katibu Mwenezi wa Mkoa Wa Dar es Salaam akimnadi Mgombea Udiwani Ndugu Husan wakati wa mkutano wa kampeni.
Mwenyekiti wa Wilaya ya kinondoni Mzee Sisiyamoto akifungua mkutano huo wa Kampeni uliofanyika katika kata ya Kinondoni.
Kada wa CCM Ndugu Macdonald akiwafanyia kampeni Wagombea, ikiwa ni Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzan, Mgombea Udiwani kata ya Kinondoni Ndugu Husana na Mgombea Urais Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
Kundi maarufu la fataki likiwa juu ya jukwaa wakiburudisha Wananchi.
Wananchi na Wana CCM wakimkaribisha Mh.Iddi Azzan katika Mkutano wa Hadhara.
Wananchi wakiburu dika baada ya Mkutano kufungwa.

No comments:

Post a Comment