Sunday, October 31, 2010

MHE.IDDI AZZAN AKIPIGA KURA, HUKU ZOWEZI LA KUPIGA KURA LIKIENDELEA VIZURI KATIKA MAENEO MBALIMBALI, DAR ES SALAAM.

Mhe.Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia tiket ya CCM akiwasili katika kituo cha kupigia cha kura katika shule ya msingi ya Alhassan Mwinyi.

Msimamizi wa kituo cha kupiga kura akimuonyesha Mhe.Iddi Azzan Jina lake.

Mhe.Iddi Azzan akifuata taratibu za upigaji kura akionyesha kadi yake ya kupiga kura kwa Msimamizi.

Msimamizi akimkabidhi karatasi za kupigia kura Mhe.Iddi Azzan Mgomba Ubunge Jimbo la Kinondoni.
Mgombea Ubunge Mhe.Iddi Azzan akipiga kura yake kwenye chumba maalum kilicho andaliwa kwa kazi hiyo ya upigaji wa kura.

Akitumbukiza kura yake kwenye Sanduku la bluu ambalo ni la Mbunge.

Akitumbukiza kura yake kwenye Sanduku jeupe ambalo ni la Diwani.

Akitumbukiza kura yake kwenye sanduku Jeusi ambalo ni la Rais.

Msimamizi akimpaka wino Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni.

 Watu wakionekaniwa kwenye hali ya utulivu katika kituo cha kupiga kura kilichopo Sinza "A"

 Wananchi wakionekaniwa ni wenye kujitokeza kwa wingi katika vituo vya upigaji kura huko Sinza.

 Hali ya Upigaji kura ikionekaniwa ni ya utulivu sana katika maeneo yote ya vituo vya upigaji kura, hapa ni shule iliopo Tandale wananchi wakionekaniwa wakiangalia majina yao.

No comments:

Post a Comment