Thursday, October 21, 2010

MHE.IDDI AZZAN AMKARIBISHA MHE.AZZAN ZUNGU KATA YA TANDALE.

Mhe.Zungu Mgombea Ubunge Jimbo la Ilala akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la kinondoni Mhe.Iddi Azzan wakati wa kampeni zilizofanyika katika viwanja vya kata ya Tandale.
Mhe.Iddi Azzan akihutubia umati wa watu katika kampeni zake zilizofanyika katika kata ya Tandale.
Mgombea Udiwani kata ya Tandale Ndugu Chilumanga akitoa sera zake baada ya kunadiwa na Mhe.Zungu ambaye pia ni mgombea Ubunge kwa Jimbo la Ilala hapo akiwa kama Mgeni waalikwa.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwasalimia wananchi na Wana CCM wakati alipowasili katika kampeni zake zilizofanyika katika kata ya Tandale.

Watoto Chipikizi wakitoa mkono wa salamu kwa mgeni rasmi pamoja na viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi baada ya kuwahamasisha Wananchi wakichague chama cha CCM.
Mgeni wa Heshima Ndugu Zungu akikabizi kadi ya CCM kwa mzee ambaye alivutiwa na utendaji na ilani ya  Chama  cha Mapinduzi hivyo kuamua kujotoa katika chama cha CUF na kujiunga na CCM.
Wananchi na Wana CCM wakiwa katika hali ya utulivu wakisikiliza sera za Wagombea.
Mzee wa mipango Ndugu Mng'ombe akiwa amtulia na baadhi ya watu akiangalia jinsi shughuli inavyo kwenda.
 Wasanii wa mizengwe wakiburudisha umati wa watu.
 Palikuwa hapatoshi.
 Watu walifurikaaa.
Vibajaji vikiongoza Msafara wa Mhe.Iddi Azza.

No comments:

Post a Comment