Thursday, October 28, 2010

DR.GHARIB BILALI AFANYA KAMPENI KIJITONYAMA,DAR

Mheshimiwa DR.Mohammed Gharib bilali akiwahutubia Wananchi katika Viwanja vya Shule Kijitonyaama,sera yake ilikuwa inahusu kutengeneza vitabu vya Sayansi mashuleni ili kuwapa urahisi Wanafunzi kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Pia alimuombea kura Mgombea Urais Mhe.Dr.Jakaya Kikwete, Wabunge na Madiwani. Wote wa CCM.
Mgombea Mwenza Dr.Gaharibu Bilali akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan katika Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Shule Kijitonyama.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwasalimia Wananchi na kugusia sera zake za kuboresha makazi, huduma za afya na Elimu. Aidha aliwaomba Wananchi ridhaa ya kumchagua tena ili kuendelea kuwaletea maisha bora.
Mhe.Dr.Mohammed Gharib Bilali akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Kijitonyama Ndugu Bulembo ili kuweza kuiongoza kata hiyo.
Mke wa mgombea Mwenza, Bi-Zakia Bilali akiwaombea kura Viongozi Wote Wa CCM Kuanzia Urais DR.Jk , Wabunge na Madiwani Wote.
 Bi-Zakia Bilali akiwa amekaa karibu na Mwenyekiti wa Wilaya ya kinondoni wakimsikiliza Mgombea Mwenza Mhe.Dr.Mohammed Gharib Bilali.
Mhe.Iddi Azzan akiwa meza kuu akisikiliza kwa makini Hotuba ya Mhe.Dr.Gharib Bilali.
Wananchi wakisalimiana na Mhe.Iddi Azzan baada ya kumalizika kwa mkutano.
Baadhi ya Vijana wakimweleza kitu Mhe.Iddi Azzan.
Mhe.Iddi Azzan akionekaniwa mwenye furaha wakati akisalimia na Wananchi huku Mhe.Asha Baraka akionekaniwa mwenye kushanga kitu,baada ya kumalizika kwa mkutano wa kamepeni za Mgombea
 mwenza zilizofanyika katika viwanja vya shule Kijitonyama.

No comments:

Post a Comment