Saturday, October 16, 2010

MH.IDDI AZZAN NA BUJUGO WA UNGURUMA KATA YA MAGOMENI.

Mh.Iddi azzan aliwaeleza wananchi wa kata ya Magomeni kuwa Chama Cha Mapinduzi kinapo ahidi kinatekeleza, alisema kuwa kwa sasa karibu kata zote zimejengwa shule ili kuwa saidia watoto wetu waweze kupata masomo kwa urahisi zaidi.

Aligusia pia suala la hospitali ya Mwananyamala kuwa kwa sasa imeshapandishwa hadhi kutoka Hospitali ya wilaya na Kuwa Hospitali ya Mkoa, aidha aliwaambia wananchi kuwa Hospitali hiyo imekuwa ikitibia wagonjwa wengi sana kuvuka uwezo wake, wamelishughulikia suala hilo kwa kujenga Zahanati kwa kila kata na kuna kata ambazo teyari zijangwa na zilizokuwa bado wanazitafutia maeneo ya kujenga Zahanati hizo.

Aliwaomba wananchi ridhaa yao wampe kura tena kipindi hichi ili aendelee kuwaletea maisha bora, kwani ilani ya Chama Cha Mapinduzi ni ilani inayotekelezeka amabayo inamtakia maisha bora kila Mtanzania.

Pia aliwataka wapinzani kuacha kusema maneno yasiyokuwa na maana, nikimnukuu "Wapinzani wanasema kuwa CCM haijafanya kitu" aliwajibu kwa kuwa inamaana hao wapinzani hawaoni barabara, Shule, Zahanati zilizojengwa na Sacos zilizoanzishwa vyote hivyo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania wapate maisha bora, wanaposema CCM haijafanya kitu wamuogope Mungu.

Mwisho aliwaomba wananchi wa kata hiyo kuchagua Mafiga matatu siku ya tarehe 31th October 2010 ikiwa kuanzia Ngazi ya Urais Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, Ngazi ya Ubunge kwa Jimbo la kinondoni Mh.Iddi Mohammed Azzan na Ngazi ya Udiwani kwa kata hiyo ya Magomeni.
 Mh.Iddi Azzan akiwa anainadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi mbele ya wanachi wa kata ya Magomeni. 
Mwenyekiti wa Wilaya akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan wa kati wa Mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya magomeni mtaa wa Idrisa.
Mgombea Udiwani kata ya Magmeni Ndugu bujugo akiwahutubia wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa kampeni uliofanyika mtaa wa Idrisa.
 Viongozi mbalimbali wakionekaniwa katika Meza kuu wakati wa mkutano wa kampeni.
Wananchi na Wana CCM wakiwa wamekaa kwa utulivu wakisiliza sera.
Kijana Mwenye uwezo wa kuiga sauti za Viongozi akionyesha kipaji chake juu ya jukwaa, aliiga sauti ya Makamba, JK, na Mwl Nyerere.
Kija wa kundi maarufu la fataki, Saidi akitoa maneno yake juu ya kwaa.
Mtoto Chipikizi Mohamed akitoa mashairi mazito ambayo yalimgusa kila mtu.
Wasanii maarufu wa mizengwe walikuwa wakiburudisha juu ya jukwaa.
Mototo akiwa amevishwa chata la CCM.

Wananchi wakiwa wametulia.....
Watoto walijaa njia yote ilifungwa na Umati wa watu.

No comments:

Post a Comment