Mhe.Asha Baraka ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azza katika Mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Bwawani kata ya kijitonyama.
Mhe.Iddi Azzan akihutubia Wananchi wa kata ya Kijitonyama katika Viwanja vya Bwawani, aliwatoa wasiwasi wafanyabiashara kwa kuwaambia serikali inawatambua na kwamba sehemu yao inashughulikiwa na itakapo malizika watakabidhiwa wenyewe, alisema atasimamia imara sehemu hiyo ilikuhakikisha walewote wanaostahiki ndio wanapewa kipaumbele.
Mwisho aliwaomba wananchi hao wahakikishe wanakipigia kura Chama Cha Mapinduzi ili kupata Viongozi bora wanaojali maslahi ya Umma. kuanzia Urais,Ubunge na Udiwani.
Katibu wa wilaya ya Kinondoni akimnadi Mgombea Udiwani wa kata ya Kijitonyama Ndugu Bulembo kwenye uwanja wa kampeni wa Bwawani.
Mgombea Udiwani kata ya Kijitonyama Ndugu Bulembo akiomba ridhaa kwa Wananchi wa kata hiyo Kumchagua yeye awe diwani, pamoja na Mbunge na Rais wote kutoka CCM ifikapo tarehe 31/10/2010 .
Ndugu Omari Kimbau ambaye ni diwani anaemaliza muda wake katika kata hiyo ya Kijitonyama akiwaomba Wananchi wakichague Chama Cha Mapinduzi CCM.
Ndugu Nyakia ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu akiwatoa hofu Wananchi na WanaCCM kwa kuwaambia kuwa CCM ina wanachama wengi sana Vyuoni ambao wamejipanga imara kuhakikisha CCM inarudi madarakani.
Katibu wa Wilaya akigawa kadi kwa Wanachama wapya wapatao kumi katika Uwanja wa kampeni wa Bwawani uliopo kata ya Kijitonyama.
Wanachama wapya wakila kiapo cha kukikubali na Kukilinda Chama Cha Mapinduzi, katika uwanja wa Kampeni wa kata ya kijitonyama
Mhe.Iddi Azzan akiwa kwenye tabasamu kubwa.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akipigamakofi baada ya kuvutiwa na wasani waliokuwa wakiburudisha hapo.
Nyakia Mwanafunzi wa Chuo kikuu akiwa nyuma ya meza kuu pamoja na Viongozi na makada wa CCM.
Chipukizi Mohammed akitoa ujumbe kwa Wananchi wa Kata ya Kijitonyama katika Viwanja vya Bwawani.
Wananchi na Wana CCM walikuwa wengi kusililiza Sera za Wagombea.
Wananchi wakisikiliza sera za Chama Cha Mapinduzi.
Biashara kwa ajili ya kukisaidia Chama cha CCM.
Mzee wa mipango Mng'ombe kushoto pichani akiwa na Hassan na binti ambaye ni mwanacham wa chama cha CCM. wakiwa wanajadili kitu.
Timu ya mipango ya Ushindi ikiwa imetulia Juu ya Gari wakiangalia Utaratibu unavoendelea.
Wasanii wanao chipukia wakiburudisha jukwaani.
Wasanii wachanga wakiwa wanatumbuiza kwenye uwanja wa kampeni.
Mhe.Iddi Azzan akiwaaga Wananchi kwa kuwapatia mkono baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni.
Watoto waki sukumana ili wapate kumsalimia Mhe.Iddi Azzan.
Mhe.Iddi Azzan akisalimiana na watoto baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni.
Mhe.Iddi Azzan akiwa Ofisi ya kata ya Kijitonyama kwa ajili ya kutia saini kabla ya kuelekea kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kata hiyo.
Mhe.Iddi Azzan akitoka katika ofisi ya kata baada ya kutia saini ya kuwasili katika kata hiyo.
Mhe.Iddi Azzan na Ndugu Bulembo wakielekea kwenye mkutano baada ya kutoka kwenye ofisi ya kata hiyo ya kijitonyama.
No comments:
Post a Comment